Sarakasi za Fr. Kitima na Maoni ya watu kwenye Msiba wa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo

Mimi sijaona wala kusikia sarakasi zozote kutoka kwa Kitima, amempa Rais nafasi ya kipekee kutoa mkono wa pole na baada ya hapo Rais ameondoka kuendelea na mishe zake na wala siyo amesusa. Naona watu mnataka kukuza mambo tu, kuna kitivii kimoja uchawara kimeweka heading eti Kitima atoa maneno ya shombo kwa Rais, huu ni uandishi uchawara kabisa.
 
Mama mwenyewe kaenda msibani kanuna. 😁
Katoa salamu kinafiki, huyo chap kaondoka zake.
Mheshiniwa Raisi muungwana hanuni kwa mashavu msibani. Hutaki usingeenda kabisa. Tuma mwakilishi.

Nje ya mada: Hilo la kumweka Kitima MC, ni la kimkakati sana.
 
Weka msiba wako wewe, umpe heshima anayostahili huyo Muuaji.
 
Swaumu siku zote inalegeza mwili, alikuwa anasinzia mara kwa mara.
 
pamoja na kwamba Fr.kitima ni miongoni mwa mapadre wa hovyo sana ndani ya kanisa katoliki, binafsi sijaona dosari yoyote kwenye ibada ya misa takatifu ya kumuombea hayati kadinali Pengo.

unafiki na ufahari kidogo ulioonekana kwenye baadhi ya matukio, kwangu mimi haukua na athari yoyote kwa wenye imani thabiti licha ya jitihada za baadhi ya mapadre na maaskofu kuligawa kanisa kanisa katoliki kadiri ya mirengo yao ya kisiasa.
 
Hapo kwenye namba 2 umeandika uongo,
 
Nukuu kutoka Somo lililosomwa kabla ya Neno la Injili

"Ukamwambie (Mfalme)

ukisema: Bwana asema hivi, Je, umeua ukatamalaki? Nawe utamwambia ukisema: Bwana asema hivi, mahali pale mbwa walipoilamba damu ya Nabothi, mbwa watailamba na damu yako, naam, damu yako"
 
Padre KITIMA ni MZIMU.

Mlitaka KUMUUA.


Hata akijenga CHUKI kwa asilimia BILLION, mimi NAMUUNGA mkono.

Na MIZIMU yote ya kina SATIVA, KITIMA na LISSU mliojaribu KUWAUA mkafeli, itawasumbua sana.
 
. Siku ya kutoa salamu za rambirambi ni siku ya mazishi ambayo ni leo
Sijaona lolote la maana ndani ya mada hii.
Nadhani ulikosa jambo la kufanya, akili ikageukia kuingia JF na kubwabwaja tu!

Kuna ndugu yako hata wa mbali aliyeuliwa kikatili Oktoba 29? Ingekupa nafasi nzuri sana kukaa kimya na kumkumbuka ndugu yako huyo aliyekatishwa maisha yake.
Muda huo ungeutumia kwa njia hiyo ingesaidia kidogo kusafisha mawazo yaliyovurugika kama inavyoonyesha katika maandishi yako haya.
 
Kutambulika na kitima au?..kama na kitima basi kitima alimtambua kama rais kwa kauli zake
kama unavyotambulika wewe kuwa 'nguruwe' mfugwaji na huyo "rais' Feki? Hii nayo ni heshima ya kujivunia?

Hapo alipo Samia mwenyewe anajuwa siyo rais, ni mhalifu anayesubiri kuwajibishwa. Kama huamini nenda kamuulize atakapokuletea makombo ya mezani kwake huko zizini anakokufugia wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…