Sasa adui wa Taifa la Tanzania si ujinga bali ni upumbavu

Ongezea bora ahangaikie tunda kimasihara kuliko kupoteza mda kuhangaikia taifa la wenyewe
 
Aisee nawaza sana kuhusu uchawi uliotumika kumroga Mtanganyika.
Mtu mwenye vyeti vya mashaka, mwenye tuhuma za mauaji leo hii anamtetemesha DED mwenye Masters.
Mkuu
lile likibatari linalowashwa na kuzimwa kila mwaka kama tukio la Kitaifa ndilo ramli yenyewe ya kudumu.

Hebu fikiria Mwenge unanasibishwa na Uhuru wa Tanganyika. Tulitafuta uhuru si wa kukimbiza mwenge kila mwaka, bali tuwe huru kweli kweli kimaendeleo, kiuchumi, kiafya, kielimu, kiteknolojia na mambo yanayofanania na hayo...

Piga picha namna ambavyo nchi nzima unakimbizwa mwenge kama sanamu.... hatutaweza asilani kunasuka hapo hadi tukubali kupiga hatua halisi
 
Kwa taarifa tu ndugu mleta mada pamoja na kwamba ,mada yako imekaa kinoko sana ,yaani kimbeya mbeya ni hivi ,serikali iliyomwajiri huyo mkurugenzi Ambae wewe unamuona ni mkubwa sana inaongozwa na chama Cha mapinduzi🤣na huyo mkurugenzi ni zao la uvccm!
 
Huo upumbavu na hayo mnayoyalalamikia ni matokeo ya upumbavu uliowajaa wasomi wetu. Mmepata elimu, lakini mmeshindwa kuitumia hiyo elimu kuikomboa jamii, wala kutatua matatizo na changamoto zinazoikabili jamii! Kwa mujibu wa tafsiri yako, huo ndio upumbavu wenyewe.
Laiti wasomi wetu wangetumia elimu zao kutatua matatizo na changamoto za jamii zilizo kwenye maeneo yao ya utumishi, hayo ya kuitwa kwenye mikutano ya kisiasa wala yasingekuwepo.
Sasa kwa kuwa wasomi wetu ni wapumbavu, kwa mujibu wa tafsiri yako, acha waendelee tu kuitwa kwenye mikutano ya kisiasa.
 
Bora Mjinga kuliko Mpumbavu maana Mjinga anaweza kuelimishwa,kuambiwa na akawa smart, ILA Mpumbavu ni kama cancer level 4,haitibiki na mbaya zaidi nchi imejaa wapumbavu wengi mno kuliko wajinga
 
Upambavu ni kiwango cha juu kabisa cha kutokujua kitu!

Mtu Mpumbavu haelimiki!

Hakuna Shule inayoweza kuondoa Upumbavu!

Shule inaondoa UJINGA*(Stupidity) lakini haiwezi kuondoa UPUMBAVU(foolishness).

Kwa hivo unaweza kuanza tena kujenga hoja yako vizuri!

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Mpaka daktari anaacha wagonjwa hospital kwenda kumsikiliza katibu mwenezi.
Hiyo ni high level of foolishness
 
wanaogopa mamlaka yao iliyowateua na kunyanganywa ulaji. Hata ingekuwa mimi ningefanya hivyo,siyo wapumbavu kwa muktadha huu ni werevu.
 
Nafikiri ni upumbavu zaidi kufikiri chama kinachoisamimia serikali hakina nguvu kuliko serikali,yaani anayesimamiwa hapaswi kuhojiwa na anayemsimamia.Leo makonda hana nguvu ya kumuhoji waziri ,mb,mkurugenzi ,RC ,DC ambao wote ni CCM? huu ndio upumbavu zaidi kufikiri ANAYESIMAMIWA anayo nguvu kuliko MSIMAMIZI
 
nchi ishakuwa ngumu
 
Nadhani ujui mifumo ya nchi chama ndio Dola.
Bossi wa mkurugenzi ni mwenezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…