mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Wakati CHADEMA kikiwa kime susa mara kadhaa katika muhimili wa Bunge sasa kimeamua kwenda kuonyesha umaahili huo katika muhimili wa pili ambao ni mahakama. Tabia hii au sera hii kwa chama hicho kikubwa cha upinzani huko bungeni ilikuwa kususa na kuweka plasta midomoni. Sera hii ambayo labda imeonyesha mafanikio makubwa huko bungeni sasa inapikwa hili isogezwe kwa pilato naye apambane nayo.
Taarifa hizi zimetufikia sikuchache baada ya Ndugu Godbless Lema kusema kuwa hana imani chombo hicho na Mbowe akifika mahakamani anyamaze kimya yaani apige plasta kama zote kama ameg'olewa taya. Wakati huo huo kiongozi mwingine mwandamizi wa chama hicho John Mlema yeye alitweeti na kuonyesha kukosa imani na mawakili wake akimtaja Kibatala. Kwa mimi ambaye sijui sharia, sijui mahakama itachukua maamuzi gani hilo zoezi likianza kwani kule bungeni walikuwa wakitolewa nje tu sijui huku.
Hata hivyo taarifa hizi zimepokelewa kwa hisia tofauti kwa wadau wa siasa za Tanzania kwani juzi tu viongozi hao walisikika wakiipongeza mahakama kwa kutenda haki kwa hukumu ya Sabaya kutolewa ambapo Sabaya alikula mvua ya miaka 30. Bado wadau wengi wanajiuliza ni wakati gani mahakama inatenda haki na wakati gani mahakama haitendi haki.
Huko nyuma nakumbuka mahakama ilimiminiwa misifa kwa kutenda haki na viongozi waandamizi wa CHADEMA kwa mahakama kumpa haki Esta Bulaya kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo la Bunda na kumwangusha Mzee Steven Wasila. Chombo hicho cha mahakama kilimiminiwa misifa hiyo lakini hakijawai kupokea sifa au kukataa sifa hata mimi sijiu.
Lakini katabia haka ka kukaa kimya au kususa kuongea huku kwetu kanisani aliwai kukafanya bwana wetu Yesu Kristo kule kwa Pilato yule Mrumi ambapo hata hivyo Yesu aliishia kusurubishwa msalabani. Najaribu kuwa wazi zaidi kwani hata mimi sijui sharia ilitoka wapi hata kuwa inakata kote haibakizi.