Sasa chumba chako, ofisi, nyumba vyaweza kupambwa na rangi kwa manjonjo namna hii

Ni kwamba, kwa aina ile ya rangi ya mapambo, kopo 1 linaweza kupiga ukuwa wa sqm 15 za mraba. kwa wale wanaoendelea kuuliza maswali kuhusu rangi, ni kwamba tumebobea kwenye uchanganyaji wa rangi, lakini pia tunauandaa ukuta au eneo linalo hitaji kupigwa rangi kitaalam tofauti na upigaji uliozoeleka. Jambo lingine garama zetu za ufundi ni za kawaida, isipokuwa aina za rangi zinatofautiana kwa garama.

Hivyo tutakuhudumia kulingana na uwezo wako. Kukutembelea na kukushauri ni garama zetu, tafadhali usisite kutuita tukupambe.

Je sehemu ambazo zina dalili za chumvi chimvi zinazofanya rangi ibanduke mapema (ndani ya mwaka 1 au 2) mnaweza kusaidia nini kifanyike na rangi gani ipigwe? je gharama kwa chumba kimoja cha kawaida ni bei gani kwa rangi na maandalizi mtakayopendekeza?
 
Asante ndugu kwa swali, tumetoa uhuru mpana, tutakutembelea na kukushauri hulipii chochote, garama ni kwetu. ila ni kwa wakazi wa Dar tu. vinginevyo ni pm email yako nitakupa maelekezo sahihi. Kama hauko Dar au umebanwa na ratiba.
 
Picha utaziona katika page ya kwanza. kumbuka tangazo hili sasa lina page 3. karibu sana.
 
Karibuni wadau, picha zinapatikana katika tangazo hili kwenye page ya kwanza.
 
Safi sana na huu ndio ubunifu.Hakika mkuu nikiwa na kazi nitakutafuta.

Nakushauri uwe na catalogue ya kazi zenu na uziwekee brand name isiyofutika kiurahisi . Hii itasaidia kumuonyesha mteja kazi zenu.

Kila la kheri na Mungu abariki kazi ya mikono yenu.
 
Nakushukuru ndugu kwa ushauri mzuri, naishukuru sana Jf kwani tayari tumepata kazi 2 kupitia tangazo hili, na wengine wanatuahidi, namshukuru Mungu tunapata mkate, nikipata kazi na vijana wenzangu wanafurahi kwani maisha yanaenda. Tuite tukupambe.
 
Mkuu kuna zile plaster za unga (sijui wanaita pre-mixed plaster), mnao utaalam nao? Na mnapiga bei gani kwa sq meter moja?
 
Ndugu hizo tunapiga, tozo kwa sqm inategemea na jinsi ukuta ulivyo andaliwa. Mafundi wengi wanaopiga plaster huwa wanafanya kazi kwa kukidhi hitaji lao, pasipo kuacha fasi ya mpigaji wa rangi. hivyo ukuta unakuwa na mawimbi mengi matokeo yake kunakuwa na kazi kubwa katika kuuandaa ukuta kwa namna ya kupigwa rangi. kwa namna hiyo tunapendekeza tukutembelee na tukushauri, hulipii chochote garama ni kwetu. karibu sana tukupambe.
 
s
Sawa mkuu, ngoja niweke mambo sawa then ntawasiliana nawe.
 
Back
Top Bottom