Sasa imekuwa wazi, kanda ya ziwa ina watanzania asilimia 25 tu

Tantarira nyingi, mbona hukuiandika mara ya Kwanza ulipanga kumpotosha nani
 
Tantarira nyingi, mbona hukuiandika mara ya Kwanza ulipanga kumpotosha nani
Nilipotosha kitu gani? Omissions inaweza kutokea kwa bahati mbaya. Ungeweza kusema kuwa nimepotosha kama ungeona hiyo Tanga labda nimeiweka Kanda ya Ziwa au Nyanda za juu Kusini au kwingineko kokote. Na hata ningekuwa nimeiweka kwenye Kanda ambayo siyo sahihi, bado ungeweza kueleza kama mtu mwenye utulivu wa akili, kwa kueleza wazi kuwa umekosea, mkoa huu haipo katika Kanda uliyoiweka, bali upo kwente kanda hii, kama wengi humu JF wanavyofanya.

Tatizo lako ni kutokuwa mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja. A gentleman with good brain, haiwezi kuona tendo la kuusahau mkoa mmoja, ni upotoshaji.

Ukiendelea kuwa kama ulivyo, huwezi kudevelop na wala huwezi kutoa mchango wowote katika mijadala.
 
Bunda yote nusu ni wasukuma
 
15m lakini majimbo ya uchaguzi hayafiki 40. Zanzibar wakaazi chini ya 2m wana majimbo ya uchaguzi 50.

Tunahitaji katiba itakayotibu haya maradhi.
Kwa maana hiyo Mwenyekiti wa Mtaa upande wa Tanganyika ni Mbunge upande wa Zanzibar kwa kigezo Cha idadi ya watu au...???
 
15m lakini majimbo ya uchaguzi hayafiki 40. Zanzibar wakaazi chini ya 2m wana majimbo ya uchaguzi 50.

Tunahitaji katiba itakayotibu haya maradhi.
Majimbo ya uchaguzi yapo 47 kwenye hiyo mikoa, wewe hiyo Pungufu ya 40 umeitoa wapi.
KAGERA 9
MWANZA 9
MARA 10
SHINYANGA 6
SIMIYU 7
GEITA 6

MIKOA MIDOGO KABISA KIENEO KWA TANZANIA NI
1. DAR ES SALAAM
2. KILIMANJARO
3. MTWARA

Mikoa hiyo ina idadi kubwa ya majimbo pengine kuliko MWANZA au Sawa na Mwanza

DAR MAJIMBO 10
MTWARA 10
KILIMANJARO 9

Kuna vigezo mahsusi katika kugawa majimbo ya uchaguzi, sio Population tu.
 
Nafikri kwenye hii hoja watu wanatofautiani kwenye mitizamo! Kuna kundi wanaitizama Kanda ya ziwa kimgawanyo wa kiselikali au tuseme kiutawala. Kundi hili litasema Kanda ya ziwa ni Mwanza, kagera, Geita Simiyu na Mara tu
Lakini kundi Jingine wanaitizama Kanda za ziwa Kama Eneo lenye watu wenye mahusiano ya kihasili au wanaoshabihana kitamaduni na kimitizamo. Hili kundi litaunganisha mikoa ya Kagera,Kigoma,Katavi,Tabora,Shinyanga,Mwanza,Geita, Simiyu na Mara.
Kwasababu Siasa ni imani au mitizamo ambayo inaendeshwa na Asili au makuzi ya mtu fulani hivyo basi ukitaka kuzichanga karata zako vizuri kisiasa lazima watu wa kundi la pili uwaweke kundi moja uwaite wote ni Kanda ya ziwa. Maana hulka,tamaduni, aina ya maisha na mwingiliano wa kimaisha unafanana katika mikoa yote Tisa. Hivyo basi Ukienda Mwanza ukawaambia nitawajengea Daraja Busisi mtu wa Kagera, Geita, Kigoma atalichukua Kama lake maana wananufaika pia moja kwa moja. Au Ukienda Shinyanga Ukasema Nitawanufaisha wakulima wa Pamba na wachimbaji wa Madini. Mikoa yote ya Tabora, Shinyanga Geita, Mwanza, Simiyu na Mara watalichulia ka lao.

Mwisho: Kumbuka Muha akiongea anaelewana na mtu wa Katavi na Kagera, Pia Msukuma na mnyamwezi ni mtu na ndugu yake, Mkurya na Mhaya ni mtu na Babu yake wao wanaitana (Sokoro), Wajita, Wakerewe, Wazinza na Wahaya hao wote mpaka tamaduni wanafanana.Yapo mengi lkn tuishie hapo.
 
We jamaa, Busisi inamuhusu nini mtu wa KIGOMA??? Mbona mnajitoa akili hivi??
 
We jamaa, Busisi inamuhusu nini mtu wa KIGOMA??? Mbona mnajitoa akili hivi??
Kumbe wewe ndo mwenye shida.Sasa mtu anayetoka mwanza kwenda kakonko,kibondo,kasulu na kigoma napitia wapi?Wewe mtu unayajua mabasi yanayoitwa Saratoga,yehove yere,adventure, yehunge ??Basi kma hauyajui basi wewe sio mweji wa kanda ya ziwa jitahidi kukaa kimya.
 
Ondoa kagera na Mara ambao hawana huo ushenzi ushenzi wa usukumagang
 
Hivi kwani kuna kanda ngapi Tanzania? Maana asilimia 25 ni robo ya wananchi wote sasa robo tatu zilizobaki zimejigawaje katika kanda zilizobaki?
 
Mleta Mada ameiacha tabora kwa makusudi
Wakati wanakaa Wasukuma na Wanyawezi ambao ni jamii sawa na watu wengine wa kanda ya Ziwa
 
Kuna vigezo mahsusi katika kugawa majimbo ya uchaguzi, sio Population tu.
Ni vigezo gani hivyo mahsusi vilivyofuatwa kutoa majimbo 9 kwa mkoa wa kusini Pemba nami nivifahamu!
 
We jamaa, Busisi inamuhusu nini mtu wa KIGOMA??? Mbona mnajitoa akili hivi??

Nakuongezea hii hapa watu wa Tabora, kigoma, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, katavi makao yao makuu ni Mwanza halafu mikoa hiyo wanaishi wasukuma wengi na wanamwingiliano mkubwa na hata shopping wote hufanyia mwanza, sasa chukua muha ni mtani wa mkurya na muhaya ( wanaitana sokuru na nyakuru) msukuma na mnyamwezi, mtu na mjomba wake, mkurya na muhaya watani hawa, muhaya ni mtani wa mzinza, mkerewe, muikizu, halafu muhangaza wa ngara anakuja kua mdogo wa muha, halafu kigoma na katavi ni watani na wako karibu mno, na mikoa yote tajwa hapo wanafika mwanza masaa 4 hadi 8 , ni rahisi sana taarifa ikianzia mwanza kufika mikoa hiyo tajwa maana wasipofika mwanza kutafuta pesa, basi kusoma au kutibiwa bugando hivo jicho la siasa limekaa hivi inaitwa kanda ya ziwa magharibi, tunakuja kanda nyingine kubwa kisiasa kwenye kura nyingi Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, na Ruvuma hapo kinara kwenye hii block ni Mbeya yaani watu wote niliotaja hapo kutoka mikoa mingine hufanya manunuzi yao mbeya au hufika kutibiwa mbeya au hutafutia pesa Mbeya, sasa kahesabu block ya Mbeya na Block ya mwanza utapata idadi ya kura zote ndio maana kanda hizo ni karata muhimu kwa wanasiasa siku zote
 
Block nyingine kisiasa ni Dodoma na Singida na manyara hizi hua ni za kawaida tu, halafu Block nyingine ni Tanga, Arusha na Kilimanjaro hiyo ni block ambayo haiwatishi sana wanasiasa washazoea kukosa kura huko toka uhuru, Block nyingine ni Dar, Pwani na Morogoro hii pia ni block muhimu kwa wanasiasa maana hua ina kura za kutosha, tunamaliza na block ya Lindi na Mtwara hii hata kwenye uchaguzi hua wnasiasa wanaenda mwishomwisho maana ni block isiyo na kura nyingi na haziwezi kuamua ushindi
 
Kwahiyo kuna block tatu za kuamua ushindi wa kisiasa na Tanzania ukikosa hizo block umekwisha ni Block ya Mwanza ndio yenye kura nyingi, Block ya Mbeya ina kura nyingi na Block ile ya Dar pia ina kura nyingi, waliobaki wakupe wasikupe hawawezi kuathiri ushindi wako kama wewe ni mwanasiasa na hizo block ndio hata kampeni huwapasua vichwa wanasiasa maana hizo block tatu wanabadilika muda wowote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…