Uchaguzi wowote Tanzania unaamuliwa na kanda inaitwa Great Lake Zone ambapo kinara hua ni Mwanza inakuaga hivi Mwanza, simiyu, shinyanga, Mara , Geita, Kagera, Kigoma, Katavi na Tabora hao watu wa mikoa hiyo wanajijua kabisa wao ni kanda ya Ziwa yaani upande mmoja ziwa Tanganyika na upande mwingine ziwa Victoria na ndio maana mwingiliano kwenye hiyo mikoa ni mkubwa yaani watu wote wanafunga mzigo wa Duka mwanza kwa asilimia kubwa na siasa za hiyo mikoa zinafanana sana ndio maana ukihesabu hata ziara za viongozi kwenye hiyo mikoa utaona mwitikio wa wingi wa watu na viongozi huko hua hawakauki, lakini pia kwa CCM inajua kabisa kanda nyingine kura zinatabirika ukitoa Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na siasa za mbeya hua ni ngumu sana ukienda kwa pupa unaweza kutangazwa umeshinda na ushirikiano hutopata milele kikubwa usiwaudhi tu, kuna kanda ambayo wao hawafahamu hata siasa ni nini lindi, ntwara wao lolote sawa tu, Ruvuma huko kijani wanajibebea kura kwenye magunia, ukija kuangalia kiuchaguzi great lake zone ina watu wengi ingekua sio hivo kamwe wanasiasa wasingewekeza macho yao huko.