Sasa kupima DNA muhimbili ni 100,000 tu

Sasa kupima DNA muhimbili ni 100,000 tu

mchlmmnl2

Senior Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
168
Reaction score
54
Bei za kupima DNA muhimbili hospitali zimepungua na kufikia shs laki moja hivyo kama huna uhakika na mtoto ulienae kama ni wako unaweza kuondoa utata.
 
Bei za kupima DNA
muhimbili hospitali zimepungua na kufikia shs laki moja hivyo kama huna
uhakika na mtoto ulienae kama ni wako unaweza kuondoa utata.

Tatizo ni ulasimu, nasikia eti hadi upitie polisi au mahakamani, sio kujiendea tu kama anayepima malaria.
 
Hicho kipimo hakitakiwi kabisa' acha tu tulee watoto wa wenzetu kuliko kuvuruga malezi ya mtoto
 
Kwa nini upitie huko kote?

ili uvunjike moyo na hatimaye usahau kabisa kuhusu DNA.nilichowahi kuambiwa serikari haitaki idadi ya machokoraa iongezeke.waliopo wanatosha.ndg yangu alifatilia sana,lakini kwa urasimu aliokumbana nao ikabidi tu akubari yaishe kiroho safi na kuendelee kulea mtoto.japo mpaka leo hana imani na mtoto ni wake.
 
wakiondoe hicho kipimo!

kitazidi kutuongezea watoto wa mitaani tu na vibaka!

ifikie kipindi serikali iangalie maamuzi nyeti kama hayo yawe yanafanywa kwa vigezo maalum vikali!

tena kama wakigundua kama mtoto si wa familia hiyo, basi haina haja ya kumpa majibu, kwa sababu hii itaongeza tatizo!

mpaka mzazi kwenda kupima dna ina maana hatokuwa na amani na mwanae endapo atagundua kuwa huyo si mwanawe!
 
Bei za kupima DNA muhimbili hospitali zimepungua na kufikia shs laki moja hivyo kama huna uhakika na mtoto ulienae kama ni wako unaweza kuondoa utata.
kaka hebu kaulizie vizuri,kupima DNA Lazima uende kwa mkemia mkuu,upeleke Ripoti ya polisi,pia unatakiwa uende nae huyo mwenzako pale kwa mkemia kutoa vipimo.
PALE MUHIMBILI TELL ME IDARA? Mi najua hakuna.
 
Bei za kupima DNA muhimbili hospitali zimepungua na kufikia shs laki moja hivyo kama huna uhakika na mtoto ulienae kama ni wako unaweza kuondoa utata.

Ishu sio bei ndugu, ukitaka kupima hiko kipimo ni lazima utokee mahakamani, muwe na kibali cha mahakama ili ipate uwezo wa kutoa judgement katika kesi ya wanandoa (Si rahisi kabisa)!
 
Nafikiri kwasababu za kiusalama zaidi unaweza kwenda kupima mtoto huko, ukakuta sio wako ukatoka huko ukaenda kumchinja mtu.
 
Bei za kupima DNA muhimbili hospitali zimepungua na kufikia shs laki moja hivyo kama huna uhakika na mtoto ulienae kama ni wako unaweza kuondoa utata.
Kama kweli ni bora, najisikia vibaya sana nikisikia baba anasema amesingiziwa mtoto.
 
kama wakina nani hao
Wababa kwa wamama, ukienda kupima jibu lolote utakalopata lazima lilete mpasuko ndani. Kama mtoto ni wako lazima mama atakujia juu kuwa ulikuwa humwamini kuna mmoja alipopima akakuta mtoto kweli ni wake mke akabeba vilivyovyake akaondoka hawezi ishi na mme asiyemwamini. Na kwa mtoto kama amekuwa kidogo lazima itamsumbua anaweza akaondoa upendo kwa wazazi. Bora majibu yawe kweli mtoto si wako.
 
wakiondoe hicho kipimo!

kitazidi kutuongezea watoto wa mitaani tu na vibaka!

ifikie kipindi serikali iangalie maamuzi nyeti kama hayo yawe yanafanywa kwa vigezo maalum vikali!

tena kama wakigundua kama mtoto si wa familia hiyo, basi haina haja ya kumpa majibu, kwa sababu hii itaongeza tatizo!

mpaka mzazi kwenda kupima dna ina maana hatokuwa na amani na mwanae endapo atagundua kuwa huyo si mwanawe!

Huko MBELE wanapima dna kwa kila mtoto anaezaliwa. Faida ni;
1. Kuongeza thamani ya mtoto kwa mzazi. Baba anakuwa na uhakika na mtoto anaelea kuwa ni mwanae. Hatoleta mchezo ktk malezi.
2. Kuzidi kumpenda mkeo kwa kuwa mwaminifu
3. Baba unajiamini kuwa we ni mzazi halisi na jukumu lililo mbele ni kulea
4. Kumbukumbu za undugu inapotokea ajali mbaya au moto.
5.Nk

Hiki kipimo kinatakiwa kuwa bure tena bila urasimu. Shame on our gvt!!
 
That is pig Latin to some of these folks!
 
Back
Top Bottom