Ndiyo, nimelelewa na wazazi wangu wote wawili. Kwa hilo umepatia. Lakini kusadiki kwamba sikupewa fursa ya kuwatembelea ndugu zangu umechemsha sana.
Ndugu nimewatembelea sana. Wao wametutembelea sana. Na kinyume kabisa na watu wengi waliozaliwa Dar, mimi Kisukuma nakitwanga kile cha Ntuzu kabisa na haikutokea tu ikawa nakijua. Ni matokeo ya wazazi kuhakikisha kwamba asili yangu ninaijua ipasavyo pamoja na ukoo wa pande zote pili.
Vile vile kwetu tumeishi na watoto wa shangazi wawili pamoja na watoto wawili wa mama wadogo tofauti. Kwa hiyo nakijua ninachokiongelea hapa. Sibahatishi.
Ndiyo, yapo mengi mazuri kwa mabaya kama vile yalivyo mengi mazuri kwa mabaya kwenye familia ambazo hazilei watoto wa ndugu. Sasa sijui hoja yako ni nini hapo!!
Hoja dhaifu kabisa hii. Dhaifu kwa sababu kuna watoto hufanyiwa yote hayo na wazazi wao wa kibaiolojia kabisa. Mara ngapi tunasoma kwenye magazeti, kusikia redioni, na kuona kwenye runinga ukatili dhidi ya watoto ambao hufanywa na wazazi wao?
Au mwenzetu wewe unaishi chini ya mwamba na hivyo kupitwa na habari kama hizo?
LMAO....well, nimezingatia ushauri wako wa kufanya utafiti japo kidogo kidogo na nimekutana na hiki kisa kilichotokea huko Mbeya ambapo mama mzazi wa mtoto alimfanyia mwanae wa kumzaa unyama wa kutisha. Narudia tena, mama mzazi alimfanyia mwanae unyama wa kutisha. Bofya
hapa upate habari kamili.
Na mimi nikupe mifano zaidi ya wazazi kuwafanyia unyama watoto wao wa kuwazaa? Maana ninayo mifano lukuki hapa na hata picha nnazo vile vile.
Hapana, siyo kweli. Wapo wajomba, mama wadogo na wakubwa, baba wadogo na wakubwa wenye upendo wa kweli. Usitumie matendo ya baadhi ya ndugu kuwarundika ndugu wote kwenye fungu moja.
Hofu yako ni unfounded. Kwa sababu kama ni ukatili tu mbona matukio hayo yapo hata kabla hatujajua DNA ni kitu gani? Mbona yapo tu na mengine yanafanywa na mama wazazi kabisa? Una irrational fear tu wewe.
Hapa unasadiki tu kwa sababu kuna watoto wenye baba na mama nyumbani na hukimbia (runaways) wenyewe tu kwa sababu mbalimbali mojawapo hiyo ya ugumu wa maisha uliyoitaja.