Umslopagazi
JF-Expert Member
- May 16, 2013
- 1,675
- 903
Wamevunja familia za watu wengi, ndoa nyingi, wamefarakanisha ndugu, wamewafanya wateja wao kuwa misukule yao, wanakatazwa kuzika hata majirani, kushiriki shughuli za kifamila, wanawaambia wao wameshatenga na mizimu Yao hivyo waachane na dunia hii, eti wanaandaliwa dunia mpya ya hapa sio Yao! Kifupi manabii hawa wameleta majanga Sana kwenye ndoa, na wako tayari wakae na kuwafungia wake za watu hata mwezi bila mawasiliano na ndugu wanawapeleka maporini eti kutafuta kondoo, watu wanakonda, wanakuwa kama vichaa, na Sisi watanzania tunaangalia tu!! Kwa kweli hawa manabii wafungiwe kabisa, la sivyo kuna hatari mbele.Hongeni muwezavyo na Rogeni muwezavyo ila Nguvu ya Mitandao haijawahi Kushindwa na Wapuuzi Duniani.
Tofauti yenu na huyu Kiboko ya Wachawi mi ndogo sana ila nyote tu mnaogelea Bahari moja.
Tumewachoka na hatuwataki Tanzania kwani mmeharibu mno Akili za Watanzania na kuwazidishia Umasikini huku mkiendelea tu Kuwarubuni.
Tumeanza na huyu Mwenzenu na tukimaliza tunakuja Kwenu na bahati nzuri nyie ni wa hapo hapo Nyumbani Tanzania hivyo Mafaili yenu Mabaya tunayo na yapo.
Tumewavumilieni vya Kutosha Okay?