Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Amani iwe nanyi wadau!
Kabla ya kwenda kwenye mada napenda kuwapongeza sana Jamii Forums. Pamoja na vikwazo na changamoto zote napenda kusema ni chombo pekee Tanzania ambacho kwenye uchaguzi huu kimejaribu kweli kusimama kwenye Haki na Kweli. Mijadala yote ya CCM na CHADEMA inajadiliwa kwa kiwango kizuri ingawa Kuna changamoto ndogo za hapa na pale.
Baada ya kusema haya napenda nirudi kwenye mada.
Zikiwa zimebaki siku kama 4 tu watanzania kufanya maamuzi kuna mambo matatu nimeyaona, napenda kusema ni kielelezo tosha kuwa CCM iko na hali mbaya sana mwaka huu. Mambo hayo ni
1. CCM kutumia silaha yake ya kujaribu kuleta mgogoro ACT Wazalendo katika hatua ya lala salama bila mafanikio.
Kwa wajuzi wa siasa za Tanzania suala la CCM Kuanza kuwaonesha mamluki wake wote waliopo ACT kabla hata kura hazijapingwa ni kielelezo tosha kuwa CCM wamebanwa sana mwaka huu na wameona ni bora watoe tu silaha zake zote. Alianza Membe na wamejitokeza wengine. Hii imewaonesha Watanzania kuwa kweli CCM kwenye uchaguzi huu hawakujiandaa kihoja. Suala la Maalim na Zitto kumuunga mkono Lissu limewashtua sana CCM na imefika sasa hawana namna yeyote zaidi ya kujaribu kete ya mwisho ya kuharibu ACT. Hali ya Zanzibar na Bara kwa CCM ni mbaya sana na hawajui wafanyaje kupata ushindi.
2. Vyombo vya Habari nguli vya Tanzania kutorusha Habari za Tundu Antiphas Lissu kwa muda wa siku mbili mfululizo.
Hili jambo ni kielelezo kingine kuwa sasa hali ya CCM na serikali yake sio Nzuri. Baada ya kampeni za Tundu Lissu za lala salama kuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi na huku zikiungwa mkono na Sheikh Ponda, kiongozi wa dini anayeaminika zaidi na kukubalika zaidi na waislamu wa Tanzania imeonekana kuwa CCM wameona tu watumie mbinu kufanya vyombo vya Habari vya Tanzania vikongwe visitangaze tu kampeni za lala salama za Tundu Lissu.
Wasichokijua CCM ni kuwa hili limezidi kuwapa hasira zaidi watanzania na wengi wao wameoneka leo walivyokisema chombo kimoja cha Habari baada ya kutoonesha mikutano ya Tundu Lissu kwenye taarifa yake ya Habari ya saa mbili usiku.
3. NEC kutoka hadharani na kuanza kuomba Poo!
Baada ya mbinu chafu zote za wizi wa kura ikiwemo kuongeza vituo hewa na wapiga kura hewa kubumbuliwa mwaka huu huku NEC ikiwa imewaonea sana wapinzani kwa kuwaengua kwenye majimbo mbalimbali na kukataa kuwaapisha wasimamizi wa uchaguzi ikiwemo kuwasimamisha kufanya kampeni wagombea wao, Leo mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi ameona tu aanze kutengeneza mazingira kutengeneza huruma kama NEC wanasingiziwa. Kwa mbinu hizi zote inaonekana dhahiri CCM wameshazidiwa sana mwaka huu na hali si hali huko kwao.
Niliwai sema mwanzoni mwaka huu kuwa hakuna uchaguzi mgumu kwa CCM Kama wa mwaka huu na mwaka huu inyeshe mvua liwake jua, CCM hawawezi shinda uchaguzi wa mwaka huu, sasa baada ya haya yote nimeamini kuwa mwaka huu CCM inaenda kuanguka rasmi kuwa Chama tawala Tanzania.
Hongereni wapinzani kwa kujiandaa vyema mwaka huu, hongera sana Tundu Antiphas Lissu.
Mungu awasimamie kweli