Sasa ni dhahiri kuwa CHADEMA si Mbowe, Dr. Slaa, Lissu wala Lema. CHADEMA ni imani na haitakufa kirahisi!

Bora umekiri Dr. Slaa alikubali kuingia kwenye mfuko wenu, natumai wale wasiosikia sasa atleast wataanza kuelewa kwamba Dr. Slaa alifika bei ya CCM wakamchukua.
 
Nasikia Dr. yupo town kuisambaratisha CDM kwa mara ya pili.
 
Bora umekiri Dr. Slaa alikubali kuingia kwenye mfuko wenu, natumai wale wasiosikia sasa atleast wataanza kuelewa kwamba Dr. Slaa alifika bei ya CCM wakamchukua.
yule mzee mkewe anamtesa sana, kabadilisha hadi itikadi na msimamo kisa the 2nd wife..laah

wengi alikuwa ni mentor wetu ila baada ya hapo tukaona mzee kakengeuka.
 
Kuhusu Chadema kuwa ni itikadi na falsafa ya haki, amani, na upendo uliojengeka miongoni mwa watanzania nakubaliana nawe.

Kwa ule ushahidi unaotolewa mahakamani na kina Adamoo na wenzake, uminywaji wa haki unaofanywa na jaji wa ile kesi, vinazidi kuipandisha juu Chadema.

Inshort CCM wanaendelea kuzidi kuifanya Chadema ipate wafuasi kila siku, ndio maana licha ya zuio la mikutano ya siasa, na CCM wakiendelea kuzurura nchi nzima peke yao bado Chadema inaendelea kuwasumbua kila dakika.
 
Kwa kweli 2020 ubunge tulipigwa Arusha, afadhali Lema mara 100 kuliko huyu wa sasa.

#kaziiendelee
 
Hoja imesimama kwa miguu kumi na 12 na imepita mkuu
 
Lakini sio bila kuwepo TUME HURU
 
Amen
 
Ukweli ni mchungu sana... bado sijaona uvccm wakija na kusema kuwa umechanganyikiwa na unazeeka vibaya wewe mzee.. utaambiwa pumzika ule mafao yako siasa hii haikuhusu na hujui kitu.. na bado utaambiwa unaoayuka payuka... hawachelewi watasema unaumwa ugonjwa wa akili na n.k.

Binafsi napenda sana mtu anaejipambanua kwa kusema ukweli... ukweli unatabia sawa sawa na haki... haki hubaguwa watu vivyo hivyo na ukweli utenganisha watu.
Ukweli haufutiki milele hata kama unafichwa kiasi gani na haki haipotei kamwe hata kama aliekunyang'anya ananguvu kama tembo au simba huko polini.
Siipendi kesi hii ya ugaidi toka inaanza mpaka sasa.
Japo naamini kwa wale ccm maslahi kama alivyosema mzee TUPA TUPA. Wao hawajisikii vibaya wanachotaka ni zamu yao ifike na sio ikatikie njiani.
Walianza mapema kuonesha nia zao toka awamu ya tano ilipoingia madarakani jambo hili likapata nguvu..
Kesi na kupotezana kwa kupitia ushauri wa uongo.. mnukuu hayati JPM akiwa anatoa husia kwenye msiba wa MAALIMU SEIF.
Nukuu isiyo rasmi " Nilikuwa nakataliwa kukutana nae na kuambiwa ni mtu mbaya sana na kumbe sio kweli nimekaa naye kwa muda mfupi ni mtu mwenye mawazo mazuri yenye kujenga nchi na kwa kweli alikuwa mwenye kuipenda na kuwapenda sana wazanzibari na Tanzania kwa ujumla"

Kwa kifupi ukiwa kiongozi ogopa kurithi maadui ambao uliwakuta wakiwa na ugomvi na watangulizi wako.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo kwanza wafuasi wao wamejazwa ges muda ukifika andiko lako litapata majibu
 
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Leo umekuwa muwazi kweli. Heshima kwako mkuu.

Andiko lako linastahili 'rejoinder' yenye nguvu za hoja. Pengine tutapata muda na nguvu kuitendea haki mada yako hii mhimu huko mbele ya safari.

Kuna watu, tuliipenda sana CCM kikiwa chama cha wakulima na wafanya kazi; sasa kimekuwa chama ambacho ni adui mkubwa wa taifa letu! CCM kimegeuka kujiona kuwepo kwacho ni muhimu zaidi kuliko uwepo wa taifa letu, ndiyo maana wamejiingiza kwenye kulihujumu taifa hili.

Nyinyi wanachama wachache mliobaki huko mnaoona udhaifu huu wa chama chenu mmeshindwa kuwa na msaada wa kubadili mwelekeo wa chama chenu huko ndani kwa ndani; kwa hiyo iliyobaki ni hukumu ya wananchi tu, na wala siyo hukumu ya vyombo vya ulinzi wala taasisi zingine zilizotekwa na chama chenu ziwatumikie nyinyi.

Pamoja na kusema CHADEMA si viongozi, lakini ukweli ni kwamba bila ya uwepo wa hao wachache waliokataa kuisujudia CCM, chama hicho kingesambaratika vibaya na lengo la CCM lingetimia.

Sasa hivi uwepo wa Mbowe, Lissu. Msigwa, Sugu. Henche, Mnyika na wengi wengine inawezekana isiwe muhimu sana kama ilivyokuwa huko nyuma kwa vile wananchi wa nchi hii hata wasiokuwa wanachama wa chama chochote cha siasa wametambua uovu wa CCM, na wapo tayari kushirikiana na vyama kama CHADEMA kuiondoa CCM bila kujali ni nani anakiongoza chama hicho, kama ilivyokuwa huko siku za nyuma; mradi tu viongozi hao wawe na uwezo wa kuwaunganisha wananchi kutimiza wajibu wao wa kuilinda nchi yao dhidi ya adui huyu mkubwa CCM.

Hawa viongozi ni lazima wawepo ndani ya CHADEMA kuweza kuendesha harakati hizi mpya za ukombozi wa nchi yetu.
 
Chadema inafanywa kama ilivyofanywa CUF na hautokuja amini hizo iman kama zitaendelea kuwepo.
 
Walianza mapema kuonesha nia zao toka awamu ya tano ilipoingia madarakani jambo hili likapata nguvu..
Hapana.
Hujuma zilianza toka zamani, hata Kikwete kwa njia zake kahujumu upinzani kwa kiasi kikubwa. Mkapa naye hivyo hivyo, hata kama haikuwa kwa kiasi kilichoonekana wakati wa Magufuli.
 
Na iwapo wapinzani watasusia chaguzi zote iwapo hakuna mabadiliko ya tume ya uchaguzi na katiba mpya, vituo vya kura havitakuwa na wapiga kura tena hasa vijana, kwani
"Iwapo wapinzani watasusia"?
Nashukuru kwamba huko mwishoni umerekebisha kauli hii...,"Hivyo CCM ijiandae kung'olewa madarakani kwa machafukoivyo"

Sioni kamwe ni kwa jinsi gani chama kama CHADEMA kitashiriki tena uchaguzi wa aina yoyote ile bila ya uwepo wa Tume huru ya Uchaguzi.
 
CCM siku waweke uchaguzi wa majaribio wapime kina cha maji kwa miguu. Naamini siku iyo ndio itakua siku ya zama
 
Eti kuna watu wanamfananisha Nyerere na Jiwe 😡
 
huyo ndiye Vua nkuvue ametema cheche
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…