Uchaguzi 2020 Sasa ni dhahiri: Kwa miaka mitano tumekuwa tukidanganywa. Uwanjani mambo ni magumu, hayako kama tulivyoambiwa

Uchaguzi 2020 Sasa ni dhahiri: Kwa miaka mitano tumekuwa tukidanganywa. Uwanjani mambo ni magumu, hayako kama tulivyoambiwa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Niko Tabora hapa. Nimekuwa kwenye uwanja wa kampeni tangu kampeni zianze. Nimekuwa nikiwafuatilia na wagombea wengine wa Urais. Nimejiridhisha kuwa wagombea ambao bado wana 'pumzi' na upinzani ni wetu Dkt. John Pombe Magufuli na wa watani zetu wa jadi CHADEMA Tundu Lissu. Wagombea hawa wamekuwa gumzo kwenye uwanja wa uchaguzi; kwenye kampeni zao. Wanachuana kwelikweli.

kwa miaka mitano ya Rais Magufuli (mgombea wetu wa CCM), Watanzania wamekuwa 'wakidanganywa'. Wamekuwa wakidanganywa kimaneno na kimatendo. Wameaminishwa kuwa Dkt. Magufuli anakubalika kuliko yeyote aliyewahi kuwa Rais nchi hii. Amekuwa akiimbiwa mapambio yenye mbio kuwa ni mbunifu, msikivu, mnyenyekevu, mwerevu, mchaMungu, msemaukweli, mtekelezaji na kadhalika. Sifa zote tamutamu amemiminiwa Serikalini na chamani. Na Bungeni.

Ilitarajiwa, kwenye uchaguzi huu na kwakuwa Mgombea wetu ameyasema na kuyatenda yaliyo mema kwa kila mtanzania, Dkt. Magufuli atumie nguvu ndogo mno kuomba kuongezewa miaka mingine mitano ya Urais wake. Angeonesha tu mazuri yake na mazuri yake yangembeba. Huku kwenye uwanja wa kampeni za Urais, mambo ni moto. Mambo ni magumu kuliko saumu/swaumu lakini kupambana muhimu.

Ni kama watanzania hawajamuelewa. Wanataka mgombea wetu aanze upya kuwaeleza bila kuwaliza. Aanze upya kuwaahidi kabla ya Eid kuhsu nini hasa kitafanyika hasa katika kupunguza makali ya maisha yao. Hata wahudhuriaji kwenye kmikutano yetu 'hutengenezwa' na Serikali na chama katika sehemu husika. Majombo huchanga; wilaya huchanga na hata mikoa huchanga wahudhuriaji. Kwanini iwe hivi? Kwanini watanzania ni wagumu wa kuyaona tuliyoambiwa kwa miaka mitano?

Huku uwanja wa kampeni, nguvu kubwa inatumika. Kinyume na ilivyotarajiwa. Kinyume na ilivyosaidikiwa. Kinyume na tulivyoaminishwa kukubalika, kuuzika, kupendwa na kuaminiwa kwa mgombea wetu na kujiandaa na ushindi wa kimbunga bila kupiga ukunga. Mambo ni tofauti kama mkaa na taa; tofauti kama gari na wali. Kampeni zinaendelea, kamepni zimepamba moto na si za kitoto. Picha, mabango ya viwango na matangazo yenye ujazo yaongezwe. Hadi watanzania waelewe.

Mikwara yaweza kuleta hasira na hasara!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Tabora)
 
Aisee kama kuna chama kinachotumia nguvu kubwa na ya ajabu basi CCM! Wengi tumebaki midomo wazi, kwanza pamoja na kufanya kampeni peke yao miaka yote mitano lakini bado imebuma, sasa wanahangaika kupita tena kila kona, wametapanya viongozi wastaafu na waandaamizi wameunda timu sasa zinafika 5 wametawanyika karibu nchi nzima lakini wapi!

Wamekusanya umati wa wasanii wote maarufu ili kutembelea nyote yao lakini wapi! Wamenunua magari ya kampeni ya kila aina wamejaribu kutawanyika nayo, lakini imebuma na sasa nao wameiga kutumia chopa wakati ni wiki 1 tu imepita Polepole alidai wanafanya kampeni kisayansi na hawatatumia chopa, vipi imekuwaje? Miradi yao ya mireli, midaraja na mibarabara yote ipo nchi kavu wao wameruka angani, si waitumie hiyoiyo nchi kavu ili iwe raihis kuinadi?
 
We we ni zero brain!
Chama Kama CCM Hakuna ugumu wowote kinakutana nazo kwenye kampeni za mwaka huu!

Kwa taarifa yako nguvu ya CCM ni kubwa mno na ushindi unaotafutwa ni wa kuweka rikodi Mpya ya angalau 89% au 90%

Wewe na hao wanafiki wenzako mnaojifariji kwamba CCM hii inapata ugumu endeleeni kuamini hivyo!

Matokeo ya kura yatawashangaza mwaka huu!
 
Mwenzako ni mjumbe wa halmashauri kuu, na yupo kwenye kampeni

Na ni mmoja wa Watu ambao wanakula posho za kampeni

Sasa ww umekaa tu kwenu kilindi huko unaanza kubisha bisha tu
 
Kama ni kweli usemavyo kuna haja gani ya kuwasumbua Wazee Wastaafu waliokwisha maliza muda wao?? Kuna haja gani kuwaita Marais wa nchi za Jirani kuja kumsaidia kuomba kura?? Ktk awamu zilizopita uliwahi kushuhudia kitu kama hicho??

Ukweli ni kwamba Mzee pumzi imekata(Batery Low). Na hivi sasa kabakiza kuwafokea na kuwatisha Wapiga Kura. Nalo litamkwamisha pia.
 
Umeshindwa kuvumilia na sasa mambo yalivyo magumu umeamua kujifunua wazi zaidi mzee wa kijenge chini.....
 
Mwenzako ni mjumbe wa halmashauri kuu, na yupo kwenye kampeni

Na ni mmoja wa Watu ambao wanakula posho za kampeni

Sasa ww umekaa tu kwenu kilindi huko unaanza kubisha bisha tu
Vitoto vya dot com ndio vilivyo, wanavamia tu jukwaa macho juu bila kujuwa back ground ya members humu, au previous thread zao.
 
Back
Top Bottom