VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Niko Tabora hapa. Nimekuwa kwenye uwanja wa kampeni tangu kampeni zianze. Nimekuwa nikiwafuatilia na wagombea wengine wa Urais. Nimejiridhisha kuwa wagombea ambao bado wana 'pumzi' na upinzani ni wetu Dkt. John Pombe Magufuli na wa watani zetu wa jadi CHADEMA Tundu Lissu. Wagombea hawa wamekuwa gumzo kwenye uwanja wa uchaguzi; kwenye kampeni zao. Wanachuana kwelikweli.
kwa miaka mitano ya Rais Magufuli (mgombea wetu wa CCM), Watanzania wamekuwa 'wakidanganywa'. Wamekuwa wakidanganywa kimaneno na kimatendo. Wameaminishwa kuwa Dkt. Magufuli anakubalika kuliko yeyote aliyewahi kuwa Rais nchi hii. Amekuwa akiimbiwa mapambio yenye mbio kuwa ni mbunifu, msikivu, mnyenyekevu, mwerevu, mchaMungu, msemaukweli, mtekelezaji na kadhalika. Sifa zote tamutamu amemiminiwa Serikalini na chamani. Na Bungeni.
Ilitarajiwa, kwenye uchaguzi huu na kwakuwa Mgombea wetu ameyasema na kuyatenda yaliyo mema kwa kila mtanzania, Dkt. Magufuli atumie nguvu ndogo mno kuomba kuongezewa miaka mingine mitano ya Urais wake. Angeonesha tu mazuri yake na mazuri yake yangembeba. Huku kwenye uwanja wa kampeni za Urais, mambo ni moto. Mambo ni magumu kuliko saumu/swaumu lakini kupambana muhimu.
Ni kama watanzania hawajamuelewa. Wanataka mgombea wetu aanze upya kuwaeleza bila kuwaliza. Aanze upya kuwaahidi kabla ya Eid kuhsu nini hasa kitafanyika hasa katika kupunguza makali ya maisha yao. Hata wahudhuriaji kwenye kmikutano yetu 'hutengenezwa' na Serikali na chama katika sehemu husika. Majombo huchanga; wilaya huchanga na hata mikoa huchanga wahudhuriaji. Kwanini iwe hivi? Kwanini watanzania ni wagumu wa kuyaona tuliyoambiwa kwa miaka mitano?
Huku uwanja wa kampeni, nguvu kubwa inatumika. Kinyume na ilivyotarajiwa. Kinyume na ilivyosaidikiwa. Kinyume na tulivyoaminishwa kukubalika, kuuzika, kupendwa na kuaminiwa kwa mgombea wetu na kujiandaa na ushindi wa kimbunga bila kupiga ukunga. Mambo ni tofauti kama mkaa na taa; tofauti kama gari na wali. Kampeni zinaendelea, kamepni zimepamba moto na si za kitoto. Picha, mabango ya viwango na matangazo yenye ujazo yaongezwe. Hadi watanzania waelewe.
Mikwara yaweza kuleta hasira na hasara!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Tabora)