Uchaguzi 2020 Sasa ni dhahiri: Kwa miaka mitano tumekuwa tukidanganywa. Uwanjani mambo ni magumu, hayako kama tulivyoambiwa

Uchaguzi 2020 Sasa ni dhahiri: Kwa miaka mitano tumekuwa tukidanganywa. Uwanjani mambo ni magumu, hayako kama tulivyoambiwa

We we ni zero brain!
Chama Kama CCM Hakuna ugumu wowote kinakutana nazo kwenye kampeni za mwaka huu!
Kwa taarifa yako nguvu ya CCM ni kubwa mno na ushindi unaotafutwa ni wa kuweka rikodi Mpya ya angalau 89% au 90%
Wewe na hao wanafiki wenzako mnaojifariji kwamba CCM hii inapata ugumu endeleeni kuamini hivyo!
Matokeo ya kura yatawashangaza mwaka huu!
Sijaelewa umekanusha nini na umeeleza nini. Kama hakuna ugumu wowote, kwanini kutumia nguvu kubwa kutafuta ushindi?
 
We we ni zero brain!
Chama Kama CCM Hakuna ugumu wowote kinakutana nazo kwenye kampeni za mwaka huu!
Kwa taarifa yako nguvu ya CCM ni kubwa mno na ushindi unaotafutwa ni wa kuweka rikodi Mpya ya angalau 89% au 90%
Wewe na hao wanafiki wenzako mnaojifariji kwamba CCM hii inapata ugumu endeleeni kuamini hivyo!
Matokeo ya kura yatawashangaza mwaka huu!
Hawa wanasemaje?View attachment 1576158
IMG_20200920_232447.jpeg
 
Niko Tabora hapa. Nimekuwa kwenye uwanja wa kampeni tangu kampeni zianze. Nimekuwa nikiwafuatilia na wagombea wengine wa Urais. Nimejiridhisha kuwa wagombea ambao bado wana 'pumzi' na upinzani ni wetu Dkt. John Pombe Magufuli na wa watani zetu wa jadi CHADEMA Tundu Lissu. Wagombea hawa wamekuwa gumzo kwenye uwanja wa uchaguzi; kwenye kampeni zao. Wanachuana kwelikweli.

kwa miaka mitano ya Rais Magufuli (mgombea wetu wa CCM), watanzania wamekuwa 'wakidanganywa'. Wamekuwa wakidanganywa kimaneno na kimatendo. Wameaminishwa kuwa Dkt. Magufuli anakubalika kuliko yeyote aliyewahi kuwa Rais nchi hii. Amekuwa akiimbiwa mapambio yenye mbio kuwa ni mbunifu, msikivu, mnyenyekevu, mwerevu, mchaMungu, msemaukweli, mtekelezaji na kadhalika. Sifa zote tamutamu amemiminiwa Serikalini na chamani. Na Bungeni.

Ilitarajiwa, kwenye uchaguzi huu na kwakuwa mgombea wetu ameyasema na kuyatenda yaliyo mema kwa kila mtanzania, Dkt. Magufuli atumie nguvu ndogo mno kuomba kuongezewa miaka mingine mitano ya Urais wake. Angeonesha tu mazuri yake na mazuri yake yangembeba. Huku kwenye uwanja wa kampeni za Urais, mambo ni moto. Mambo ni magumu kuliko saumu/swaumu lakini kupambana muhimu.

Ni kama watanzania hawajamuelewa. Wanataka mgombea wetu aanze upya kuwaeleza bila kuwaliza. Aanze upya kuwaahidi kabla ya Eid kuhsu nini hasa kitafanyika hasa katika kupunguza makali ya maisha yao. Hata wahudhuriaji kwenye kmikutano yetu 'hutengenezwa' na Serikali na chama katika sehemu husika. Majombo huchanga; wilaya huchanga na hata mikoa huchanga wahudhuriaji. Kwanini iwe hivi? Kwanini watanzania ni wagumu wa kuyaona tuliyoambiwa kwa miaka mitano?

Huku uwanja wa kampeni, nguvu kubwa inatumika. Kinyume na ilivyotarajiwa. Kinyume na ilivyosaidikiwa. Kinyume na tulivyoaminishwa kukubalika, kuuzika, kupendwa na kuaminiwa kwa mgombea wetu na kujiandaa na ushindi wa kimbunga bila kupiga ukunga. Mambo ni tofauti kama mkaa na taa; tofauti kama gari na wali. Kampeni zinaendelea, kamepni zimepamba moto na si za kitoto. Picha, mabango ya viwango na matangazo yenye ujazo yaongezwe. Hadi watanzania waelewe.

Mikwara yaweza kuleta hasira na hasara!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Tabora)
Watu walifika wengi, na hasa vijana akina mama, zaidi kuwaona wanamziki. Hawakumwona Diamond, japo walitangaziwa kuwa atakuwepo. Viparata Tabora ni kero kubwa kwani mkuu wa wilaya anawaamuru waajiri wa maduka, bar, migahawa na mamalishe kuwanunulia viparata watumishi wao. Tatizo la hospital ya Kitete kuwatoza wazazi sh 50000 na 45000 kujifungua watoto wa kiume na kike hakulijibu. Huenda ni kuongeza mapato ya serikali, kumbuka anawahimiza wanawake kuzaa zaidi.
 
Ngoja Lumumba wenzio watoke lunch, leo haki ya nani utabaki mapepe mtupu!
 
Utakuta hadi Lisu akisoma hapa anachekelea kwamba mambo ni magumu sana kwa ccm na atashinda kiulani sana
 
We we ni zero brain!
Chama Kama CCM Hakuna ugumu wowote kinakutana nazo kwenye kampeni za mwaka huu!
Kwa taarifa yako nguvu ya CCM ni kubwa mno na ushindi unaotafutwa ni wa kuweka rikodi Mpya ya angalau 89% au 90%
Wewe na hao wanafiki wenzako mnaojifariji kwamba CCM hii inapata ugumu endeleeni kuamini hivyo!
Matokeo ya kura yatawashangaza mwaka huu!
Ushindi wa 90 - 100% kwa uwizi? Sawa.
 
We we ni zero brain!
Chama Kama CCM Hakuna ugumu wowote kinakutana nazo kwenye kampeni za mwaka huu!
Kwa taarifa yako nguvu ya CCM ni kubwa mno na ushindi unaotafutwa ni wa kuweka rikodi Mpya ya angalau 89% au 90%
Wewe na hao wanafiki wenzako mnaojifariji kwamba CCM hii inapata ugumu endeleeni kuamini hivyo!
Matokeo ya kura yatawashangaza mwaka huu!
Punguza mahaba ya kichama,Mara nyingine hurodhurika kusema ukweli,mtaani Mambo ji magumu Sana.
 
Mwenzako ni mjumbe wa halmashauri kuu, na yupo kwenye kampeni

Na ni mmoja wa Watu ambao wanakula posho za kampeni

Sasa ww umekaa tu kwenu kilindi huko unaanza kubisha bisha tu
Huyo hana ujumbe wowote k,wenye Chama! Ngoja niingie chimbo nimfahamu vizuri na nitamuweka wazi hapa
 
Kwa taarifa yako tu
Yy yuko kwenye msafara wa rais magufuli

So Wala usipate shida ya kuingia chimbo, huyo Mtu humuwezi na humfikii hata kwa dhambi zake
Kama yuko kwenye msafara ni sababu nyengine ya kumsaka , yeye ni msaliti ni lazima atafutwe!
 
Hahaha! huyu mzee bhana, eti 'ushindi wa kimbunga bila kupiga ukunga!'
 
Back
Top Bottom