kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 735
Hakuna kundi wala wafuasi wa Magufuli ndani ya CCM.
Wanasiasa huangalia manufaa yao binafsi na ndio maana Kinana alipita kwa 100%.
Mwanasiasa pekee aliyeangalia masilahi ya umma ni Magufuli tu.
Kwani Kuna kiongozi yeyote ambae hakuwafanyia chochote wananchi waliomchagua? Hakuna kiongozi ambae hakuwahi watendea mazuri wananchi wake na ndio maana hata jpm mwenyewe hakuwahi kubisha kuwa hakuna mazuri yeyote yaliyofanywa na watangulizi wake licha ya yeye na wafuasi wake akuponda utwala tangulizi kwake na kuyafanyia kazi Yale aliyoyaona yy yakuwa mazuri huku nae akiyafanya mazuri yake na mabaya yake ambayo wafuasi wake hawataki yaongelewe kwa Sasa Kama ambavyo awamu ya tano ilivyoyaongelea mabaya ya awamu zilizotangulia hata kuuaminisha umma kuwa akina kikwete,Ben,mwinyi hawakuwahi fanya lolote zuri kwa wananchi zaidi ya ufisadi na kujijali wao tu.
Hoja yangu kubwa ni kwamba kiongozi ahukumiwe kwa haki kutokana na matendo yake na sio kuangalia sura kwamba huyu yasemwe mazuri tu Ila kwa yule yasemwe mabaya, kiufupi awamu ya tano inanyolewa na wembe ule ule na ulitumika na jpm kuwanyolea watangulizi wake. Acha awamu ya sita nayo iinyoe vya kutosha awamu ya tano kwakuwa ndio tabia zetu tulizojipa Sasa.