Sasa ni wakati wa kuianika mikataba yote ya Magufuli kama wao walivyoanika mkataba wa Bandari ya Bagamoyo na mingineyo

Sidhani kama serikali inahitaji kufanyia kazi maneno ya mitandaoni,na kama wewe ni mmoja ktk viongozi yamkini ni mbunge tutaenda kusema bungeni huko

Tunachojua JPM alikua kiongozi shupavu na tutamkumbuka,hatuamini kama aliweza kua na makando kando

Nje na hivyo utakua unatupigia kelele tu
 
Lazima tuipitie kwa masilahi ya Taifa.
 
Tena huyu ndiye kasaini mikataba lukuki bila hata bunge kuridhia. Ifumuliwe yote hasa ile itakayobainika kuwwumiza wananchi.
Ifumuliwe yote - tuanze na kufumua ukuta wa Mererani, ukuta wote uondolewe na matofali wawagawie wananchi. Baadae tufumue SGR yote maana ujenzi wake umeumiza wananchi, barabara ya mbezi ibaki lane moja tu, wote waliovunjiwa majumba warudishwe wajenge sehemu zao, wagawiwe kifusi kitakacho toka kwenye lane nyingine zitakazo vunjwa.
Ndege zipigwe mnada zote, maana ni maendeleo ya vitu si watu! Tusiishie kufumua mikataba tu tufumue vyote vilivyojengwa na hiyo mikataba. Tuanze alifu! Demokrasi itakuwa imetamalaki!
 
Hilo ni sawa
 
Niliuwaga muumini mzuri wa Upinzani,baadae niliona ni Usanii mtupu umewajaa! Sasa hivi JK kageuka kuwa Malaika kwao. Kweli JPM aliwanyoosha.
Upinzani wa kweli haujawahi kumjadili au kumuabudu mtu bali walijikita kwenye matendo yao.
 
maoni yako ni sahihi kwa kiasi kikubwa ila unakosea kusema walivunja mkataba wa Bagamoyo kwani ule mkataba ulikuwa jaujakamilia kisheria. Serikali baada ya kuangalia terms za mktaba huo ndipo ikajitoa: siyo kuwa walivunja mkataba uliokuwa umekukwisha pita, bali waliamua kutokuusaini mkataba huo.
 
Magufuli alikosea sana kuziweka zile details za mkataba wazi... It was a blow in the asss kwa JK...

Sasa zamu yake imefika.. Sadly enough he is gone. Hamtaamini nawaambia.
 
Magufuli alikosea sana kuziweka zile details za mkataba wazi... It was a blow in the asss kwa JK...

Sasa zamu yake imefika.. Sadly enough he is gone. Hamtaamini nawaambia.
Zile details hazikuwa na privacy yoyote na wala hakukuwa na implications yoyote kwa Kikwete, kwani zilikuwa bado ni proposals tu kabla ya kufikia makubaliano. Inawezekana kabisa kuwa hata Kikwete mwenyewe angezikataa!!
 
Mkuu umeandika mengi ila ni upupu mtupu. Hao unaosema wamejitokeza ni kutaka kuhakikisha kuwa mweli kaondoka.

Ile misafara yote na mitutu ya bundiki haikuwa kitu mbele ya kifo. Alifikiri walinzi wote wale wangeweza kumkinga na kifo. Ninyi ndiyo mjitafakari ktk hilo.

Aliwananga sana watangulizi wake juu ya mikataba. Sasa tunahitaji mikataba yake nayo iwe wazi ili tuchekeche. Je alikuwa na uhalali wa kuwananga watangulizi wake??
 
Siku hizi hamna chochote mnachojua bali ni uchawi tu.
Labda msubili huyu mama kama atakwama mpate pa kupumlia
Mbona mnatoa povu?? Kwani ni vibaya kujua alichofanya mzalendo wetu,shuja wetu!!. Ni wakati sahihi kuwajua wanufaika wa utawala iliopita kama ulivyofanya utawala wake kuwatumia kina msiba kuwatanaza kina makamba jr kwamba n majizi. Vivyohivyo tunataka kujua ukwel wa mikataba hiyo ni haki yetu.
 
Zile details hazikuwa na privacy yoyote na wala hakukuwa na implications yoyote kwa Kikwete, kwani zilikuwa bado ni proposals tu kabla ya kufikia makubaliano. Inawezekana kabisa kuwa hata Kikwete mwenyewe angezikataa!!
Zilichapwa kwenye magazeti au kuwa posted mtandaoni!??

They were deeply private.. Na ndo maana Magu alizitumia kupatia kiki... Kila akijisikia tu anaisoma..

Zamu yake imefika.
 
Hapo ndo Uwezo wenu wa kufikiria ulipoishia, wengi mnajiona mmesoma na kuelewa kumbe ni mateka wa fikra za elimu ya kidhalimu ya mkoloni.

Wengi wenu Barabarani Mnaonekana wenye utimamu wa akili kumbe kwa Ubungo ni empty minded, idiots & fools.

Mnajua kutamba nyuma ya keyboards but on the ground ZEROS.

Acheni Magufuli apumzike kwa Amani kwa Kazi Kubwa aliyoifanya Just for 5' yrs Consecutivelly.
 
Vipi kuhusu familia ya saa8, Azory, Mawazo, Lissu Akwilina, waliopotea??? Nchi ilipalaganyika machache mkawa na sauti yakuamua mambo nyeti ya Nchi bila utaratibu wananchi tunahitaji mtu atakae-harmonize upepo huo kurudisha umoja na upendo. Sgr,hospital, Barbara havina maaana kama hakuna haki na upendo.
 
Niliuwaga muumini mzuri wa Upinzani,baadae niliona ni Usanii mtupu umewajaa! Sasa hivi JK kageuka kuwa Malaika kwao. Kweli JPM aliwanyoosha.
Kma ulikua upinzani basi ulikua liability..... Shida ya upinzani na JPM ni kuzuia mawazo mbadala kupitia vyama vya upinzani na media shida ilianzia hapo. Ni sawa na Rwanda tu kagame amepiga kazi kuliko hata JPM ila anachukiwa sababu tu ya kutumia mabavu kwenye kila kitu. Kwa staili hii utawapa watu maendeleo huku ukijenga chuki kubwa na baadhi yao.

Sasa kma ww hukuona hilo tatizo basi niseme tu ulikua liability upinzani maana kule ni ideology sio ushabiki.
 
Zilichapwa kwenye magazeti au kuwa posted mtandaoni!??

They were deeply private.. Na ndo maana Magu alizitumia kupatia kiki... Kila akijisikia tu anaisoma..

Zamu yake imefika.
Ninaishi Marekani takriban miaka 30 sasa. Serikali za huku (federal na state) zinafanya mikataba mingi sana na makampuni, taarifa inayotoka kwa waalipa kodi ni kuhusu malengo ya mradi, muda wa kukamilisha mradi huo, gharama za mradi wenyewe, na contractor aliyepewa mradi. Na ni kwamba contractor akimaliza kudeliver, kimsingi anaondoka labda anabaki kwa muda ule wa warranty tu!

Mradi wa Bagamoyo ulikuwa na washirika watatu, jambo ambalo ndilo lilikuwa baya kabisa; ilitakiwa kuwe na washirika wawili tu, yaani serikali na contractor, ile yule mshirika wa kati yaani financier alikuwa anaharibu kabisa maana ya mikataba ya miradi ya ujenzi!
 
Hapo ndo Uwezo wenu wa kufikiria ulipoishia, wengi mnajiona mmesoma na kuelewa kumbe ni mateka wa fikra za elimu ya kidhalimu ya mkoloni.
Mind you huyo JPM alisoma elimu ya mkoloni hadi kupewa PhD.... Na hata hyo pacemaker aliyowekewa ni kupitia elimu na vifaa vya mabeberu!!

Open Governance Initiative na hata rasimu ya warioba zina ruhusu mikataba iwe wazi kwa ajili ya review bungeni on behalf ya wananchi. Sasa mnapopinga wanaohoji mikatana tuwaeleweje? Yaani mnajiita wazalendo afu mnapinga uwajibikaji? Au ndio mnataka kumfanya JPM hakuwa erroneous hta kipunje?
 
Mikataba sawa na manunuzi yote pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…