Sasa ni zamu ya influencer, Kila mtu atafikiwa na Utawala Batili wa CCM

Sasa ni zamu ya influencer, Kila mtu atafikiwa na Utawala Batili wa CCM

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Ni swala la muda.. Kila mtu atatoa mlio.. Walijua Machawa wapo sallama. Muuaji hana rafiki.

Tuliwaasa, achaneni na CCM kwani washapoteza uelekeo. Akili za wanaccm sasa hivi ni kuua, kuteka, kubambikiza kesi, Vitisho, unyanyasaji na ufisadi.

Watu walijua hii kitu inawahusu CHADEMA, sasa kila mtu ataimba wimbo wa mabadiliko.

Tanzania hakuna amani kama wewe si fisadi. Wanaotetea mfumo wa CCM ni wanaonufaika na mfumo. Hakuna mlalahoi anaiunga mkono CCM bila vitisho.

Kila siku tunawaambia changieni Tonetone hamtaki mwisho wa siku CHADEMA ndo inawaletea mawakili wa kuwatetea bila kujali vyama vyenu na dharau zenu. Muulizeni Niffer.

Anayejiita Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Patrobas Katambi ametangaza wito wa kikao maalum na baadhi ya wasanii maalum waliochaguliwa na wasanii hao watatakiwa waripoti Central Police kesho saa 4:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wito huo unawahusu Gift Stanford 'Gigy Money', mwanamitandao Dotto Kito, Burton Mwemba 'Mwijaku', Juma Lokole, Maimartha Jesse, Anko T pamoja na wengine.

Waliotajwa wametakiwa kufika kituoni hapo saa mbili asubuhi.

Waziri Katambi ameeleza kuwa baadhi ya ajenda zitakazojadiliwa ni za kiserikali na zitaendelea kujulikana kesho, Septemba 2, 2026.
 
Viongozi wa serikali wakiona mtu anapata umaarufu au ushawishi katika jamii halafu hajapitia katika mikono yao wanajaa wivu na wanamhofia. Ama watajaribu kumuweka karibu au watamnyamazisha kwa njia watakayoona inafaa.
 
Serikali ikiwajibisha watu kama inatakiwa kupogezwa hawa ni tatizo kwenye kioo cha jamii matendo yao ni ya ovyo huo ndo ukweli mchungu
 
Back
Top Bottom