Natumai sote tumeshapitia zile ndoto zinazohusisha mapambano kama kupigana, kufukuzwa na mnyama, kujamiiana, kubishana nk.
Sasa kunakipindi mimi nilikuwa nashindwa kirahisi nikiwa napambana nikiwa ndotoni. Jambo hili huwa linaniumiza sana maana huwa sipendi kushinda, haijalishi ni wapi.
Katika kutafuta mwarubaini nikaambiwa kuwa ukiwa umelala huku umejikunja unaweza kupigwa kirahisi na adui, na ukiwa umelala kwa kinyooka basi utashinda pambano kirahisi mno.
Kwa kipindi kirefu nikawa napuuzia dhana hii, lakini kitendo cha Mimi kushindwa battle pindi nikiwa ndotoni kikanisukuma kujaribu kile kinachosemwa.
Wakuu, baada ya kuanza kulala kwa kujinyoosha kama mlingoti, nimeanza kuona matokeo chanya kwani Kila nifanyalo ndotoni basi kinakuwa upande wangu.
Yaani sasa nikikutana na jambazi namnyoosha vilivyo, nikiwa na demu namfikisha kileleni bila wasi tofauti na huko nyuma, nikikimbizwa na Simba hanikamati maana nina speed kama kombora la kibalistiki, hata nikiwa nabishana kijiweni basi napangilia hoja hadi ninaitwa profesa.
Dah ni raha tupu yaani!
Monetary doctor,
Dr am 4 real PhD.