Sasa nimeelewa vizuri tofauti kati ya uongozi wa Rais Magufuli na Rais Samia

NI kweli. Lakini tusi deny kwamba uongozi wake uliumiza wanasiasa wa upinzani. Ila sasa angalau alikuwa na hizo 50% za uzuri na 50% za ubaya, tofauti kabisa na sasa, ambapo tunaweza kusema uzuri ni 20% na ubaya 80%. Bado inamfanya Magufuli kuwa bora zaidi.
Alimuumiza kiongozi yupi wa upinzani? Weka na ushahidi
 
Basi Magufuli alikuwa bora zaidi, alifanya kila awezalo kwa ajili ya watanzania wote.
Ndio maana bado anakumbukwa na wengi. Uongozi wake wa miaka mitano tu amefanya kazi nzuri kuzidi marais wote waliotangulia kwa pamoja.
Wabongo wengi wana roho za kwanini hata huku mitaani mtu akiwa na hali nzuri kidogo utaona baadhi ya majirani wanaanza kumchukia na siku ikitokea limempata tatizo watafurahi sana japo kinafiki anakuja kukupa pole kumbe moyoni ana furaha tele,sasa kile kitendo cha kufukuza watu kazi kwa madai ya vyeti feki,matajiri kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi na kuwekwa ndani,kuchukuliwa pesa zao benki hayo ndiyo mambo yaliyokuwa yakiwafurahisha watu lakini hakuna cha maendeleo wala nini.
 
Kila mwanadamu ana mema na mabaya, sasa malaika wa humu JF ni kama hawajawahi kukosea kwa chochote katika maisha yao
Mkuu, kuna makosa mengine hayavumiliki na yanatoka kuwa katika makosa ya kawaida ya mwanadamu. Ndio maana hata trafiki kuna makosa atakuambia nenda usirudie, mengine lazima ulimwe fine. Katika baadhi ya nchi, kuna makosa lazima ulale ndani siku moja ukatolee fine mahakamani, mengine police anakupa fine hapo hapo. Sasa katika siasa kuna makosa ya kibinadamu, na mengine ni kwamba ni uongozi umeoza haufai
 
Alimuumiza kiongozi yupi wa upinzani? Weka na ushahidi
Watu wenye comment kama hizi zako huwa tuna wa-ignore tu. Unajua denialism ni ugonjwa wa akili? Ulishasikia mke anapewa mkong'oto hadi hospitali halafu anasema siwezi kuondoka kwa mume ilitokea tu siku hiyo mume wangu hakuamka vizuri, kwa kawaida ni mume mwema sana. Na tena kesho anapigwa, na anarudia kusema ni bahati mbaya tu kanipiga naona nilimkosea sana. Ndio wewe sasa. Sijui umeolewa?
 
Wala sihitaji kuandika thread ndefu juu ya hili, kwa sababu linapaswa kuwa wazi sana kwa mtu yeyote mwenye akili. Kuna tofauti kubwa sana kati ya serikali ya Raisi Magufuli na serikali ya Raisi Samia iliyopo madarakani sasa.

Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, alikuwa tayari kufanya lolote lile, na narudia, lolote lile, kwa ajili ya nchi ya Tanzania. Alikuwa tayari kuvunja baadhi ya vipengele vya Katiba ya Tanzania kwa kile alichoona ni maslahi ya Watanzania, ambao yeye alikuwa beneficiary mmoja wao.

Samia, akiwa raisi wa Tanzania, yuko tayari kufanya lolote lile, na narudia lolote lile, kwa ajili ya uongozi na CCM. Yuko tayari kuvunja baadhi ya vipengele vya Katiba ya Tanzania kwa kile anachoona ni kulinda maslahi ya uongozi na CCM, ambao yeye ni beneficiary mmoja wao.

Sasa hiyo ndio tofauti kubwa ya uongozi wa Raisi Magufuli na Raisi Samia.
Wote ni wauaji wanastahili kutupwa katika jehanam ya milele
 
solution ya yote ni katiba iheshimiwe. sema wananchi hufurahia katiba inapovunjwa na aliyeivunja kaivunja kufanya jambo linalowafurahisha kwa muda huo huku mkisahahu hilo litamfanya mwingine aivunje katika kufanya jambo ambalo haliwafurahishi.
iwe kwa wema au ubaya katiba iheshimiwe bila hivyo haina maana hata ya kuwepo.
 
Bonge la pwenti.
 
Watu wenye comment kama hizi zako huwa tuna wa-ignore tu. Unajua denialism ni ugonjwa wa akili? Ulishasikia mke anapewa mkong'oto hadi hospitali halafu anasema siwezi kuondoka kwa mume ilitokea tu siku hiyo mume wangu hakuamka vizuri, kwa kawaida ni mume mwema sana. Na tena kesho anapigwa, na anarudia kusema ni bahati mbaya tu kanipiga naona nilimkosea sana. Ndio wewe sasa. Sijui umeolewa?
Empty set kabisa...
 
Wala sihitaji kuandika thread ndefu juu ya hili, kwa sababu linapaswa kuwa wazi sana kwa mtu yeyote mwenye akili. Kuna tofauti kubwa sana kati ya serikali ya Raisi Magufuli na serikali ya Raisi Samia iliyopo madarakani sasa.

Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, alikuwa tayari kufanya lolote lile, na narudia, lolote lile, kwa ajili ya nchi ya Tanzania. Alikuwa tayari kuvunja baadhi ya vipengele vya Katiba ya Tanzania kwa kile alichoona ni maslahi ya Watanzania, ambao yeye alikuwa beneficiary mmoja wao.

Samia, akiwa raisi wa Tanzania, yuko tayari kufanya lolote lile, na narudia lolote lile, kwa ajili ya uongozi na CCM. Yuko tayari kuvunja baadhi ya vipengele vya Katiba ya Tanzania kwa kile anachoona ni kulinda maslahi ya uongozi na CCM, ambao yeye ni beneficiary mmoja wao.

Sasa hiyo ndio tofauti kubwa ya uongozi wa Raisi Magufuli na Raisi Samia.
Mungu akubariki sana kwa huu uzi. Yaani umegongelea penyewe kabisa. Unajua Dkt Samia ukiangalia kwa jicho la kifisadi unaona kabisa yupo pale kwa ajili ya kulinda wezi na mafisadi. Ila akitokea mtu kamtishia tu nafasi yake au mfumo wa uongozi wake anawatoa haraka haraka ila siyo kwa maslahi ya watanzania maskini na wanyonge. Tumeshuhudia kauli zake zenye viashiria, mfano kula kwa urefu wa kamba, kutukana neno stupid, kutamka walipokutana na aliosoma nao wanasema wanachukua mil mbili kila weekend za kutumia etc, na ukiangalia hajawahi kumwajibisha mteule wake kwa ufisadi wala wizi (sijui kama kuna ushahidi wa yeye kufanya hivyo ila mi sijawahi ona). Kwa ufupi kwenye nafasi ya urais yupo kama vile kulipa fadhila za hao waliosema wazuri hawafi na walipomchoka Dkt Magufuli wakasema basi na akafa
 
We ulipoteza tu ada ya mama yako shuleni, sidhani kama una baba. Utakuwa una malezi ya single mother.
Wrong. Believe me, kuna watu wengi sana wenye malezi ya single mother wana akili sana kukuzidi, kama hii ndio namna yako ya kujibu hoja. In fact baba yangu alikuwa ananiambia JF ni kama kokoto la samaki baharini, kuna viumbe utakuta kwenye wavu vinatia hata kinyaa kuangalia - kama baadhi ya members wa JF wenye comments zinatia hadi kichefuchefu kusoma, kama hii yako!
 
Mungu akubariki sana kwa huu uzi. Yaani umegongelea penyewe kabisa. Unajua Dkt Samia ukiangalia kwa jicho la kifosadi unaona kabisa yupo pale kwa ajili ya kulinda wezi na mafisadi ila wakitishia tu nafasi yake au mfumo wa uongozi wake anawatoa haraka haraka ila siyo kwa maslahi ya watanzania maskini na wanyonge. Tumeshuhudia kauli zake zenye viashiria, mfano kula kwa urefu wa kamba, kutukana neno stupid, kutamka walipokutana na aliosoma nao wanasema wanachukua mil mbili kila weekend za kutumia etc, na ukiangalia hajawahi kumuwajibisha mteule wake kwa ufisadi wala wizi (sijui kama kuna ushahidi wa yeye kufanya hivyo ila mi sijawahi ona). Kwa ufupi kwenye nafasi ya urais yupo kama vile kulipa fadhila za hao waliosema wazuri hawafi na walichomchoka Dkt Magufuli wakasema basi.
Umenena vema sana, hata narudia maneno niliyosema hapo juu, "Kuna sababu moja tu hivi sasa kwa nini Raisi Samia anaungwa mkono na kusifiwa kila siku na viongozi waandamizi wa CCM katika nafasi zao za ndani ya chama na serikalini.......anawaruhusu watumie urefu wa kamba zao bila kuwabugudhi. Lakini si kwa sababu anaongoza nchi vizuri kwa maslahi ya mbele ya Tanzania. Hilo nitakataa katakata."
 
Wote ni wauaji wanastahili kutupwa katika jehanam ya milele
Nakuelewa. Siku moja niliweka thread hapa JF kwamba, hakuna atakaebisha Hitler alichangia sana maendeleo ya Germany, na uwezo mkubwa wa technology wa sasa wa Germany vyanzo vyake ni uongozi wa Hitler, kutia ndani chanzo cha gari za VW, Volks Wagen, gari ya watu, alipowaamuru mainjinia watengeneze gari mbayo kila Mjerumani angemudu kununua - beetle. Germany chini ya Hitler ilikuwa na nguvu ya kuichumi na kijeshi kuliko taifa lolote duniani, ndio maana iliweza kukabili karibu dunia nzima kwenye vita, Allies. Kama ingekuwa ni vita ya Germany na UK peke yake, au USA peke yake, haya mataifa yangepigwa kama mtoto.

Leo hii ukinunua VW au kupanda ukaisifia, Tuareg, Tiguan, Polo, Combi, Golf, Jetta, nk, kumbuka chanzo chake ni uongozi wa Hitler! Lakini sasa, leo hii, hatuimbi uzuri wa Hitler, bali ubaya wa Hitler, pamoja na yote mazuri aliyoifanyia Germany.
 
Uongo wake ni kuwa kawatofautisha hao watu wakati ni wamoja.

Wote wawili wanafanya hivyo kwa maslahi ya CCM na hata Magufuli hakufanya kwa maslahi ya Taifa bali chama chake CCM.
Technically yes, Magufuli alifanya hivyo pia kwa maslahi ya CCM. Tofauti inakuja kwamba Magufuli alifanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya CCM kwa ajili ya Tanzania, wakati Samia anafanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya CCM kwa ajili ya uongozi. Ndio maana Magufuli aliwasulubu hata viongozi wa CCM mafisadi, wakati Samia hafanyi hivyo hata wafanyeje. Kama umegundua, watu wengi wa CCM wanaotumbuliwa na CCM sio kwa ajili ya ufisadi, bali kutamka jambo ambalo linawaumiza CCM, hata liwe la kweli. Niambie kigogo wa CCM alietumbuliwa na Samia kwa ajili ya ufisadi ni nani? Anaishia tu kusema najua mnakula, msile hadi mvimbiwe. Disgusting!
 
Wala sihitaji kuandika thread ndefu juu ya hili, kwa sababu linapaswa kuwa wazi sana kwa mtu yeyote mwenye akili. Kuna tofauti kubwa sana kati ya serikali ya Raisi Magufuli na serikali ya Raisi Samia iliyopo madarakani sasa.

Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, alikuwa tayari kufanya lolote lile, na narudia, lolote lile, kwa ajili ya nchi ya Tanzania. Alikuwa tayari kuvunja baadhi ya vipengele vya Katiba ya Tanzania kwa kile alichoona ni maslahi ya Watanzania, ambao yeye alikuwa beneficiary mmoja wao.

Samia, akiwa raisi wa Tanzania, yuko tayari kufanya lolote lile, na narudia lolote lile, kwa ajili ya uongozi na CCM. Yuko tayari kuvunja baadhi ya vipengele vya Katiba ya Tanzania kwa kile anachoona ni kulinda maslahi ya uongozi na CCM, ambao yeye ni beneficiary mmoja wao.

Sasa hiyo ndio tofauti kubwa ya uongozi wa Raisi Magufuli na Raisi Samia.
Kazikwe pembeni ya kaburi lake ukiwa hai kuonyesha umemwelewa sana.
 
Uongo wake ni kuwa kawatofautisha hao watu wakati ni wamoja.

Wote wawili wanafanya hivyo kwa maslahi ya CCM na hata Magufuli hakufanya kwa maslahi ya Taifa bali chama chake CCM.
100% perfect. Tena sio maslahi ya ccm ni maslahi ya kikundi kidogo tu ndani ya ccm.
 
Technically yes, Magufuli alifanya hivyo pia kwa maslahi ya CCM. Tofauti inakuja kwamba Magufuli alifanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya CCM kwa ajili ya Tanzania, wakati Samia anafanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya CCM kwa ajili ya uongozi. Ndio maana Magufuli aliwasulubu hata viongozi wa CCM mafisadi, wakati Samia hafanyi hivyo hata wafanyeje. Kama umegundua, watu wengi wa CCM wanaotumbuliwa na CCM sio kwa ajili ya ufisadi, bali kutamka jambo ambalo linawaumiza CCM, hata liwe la kweli. Niambie kigogo wa CCM alietumbuliwa na Samia kwa ajili ya ufisadi ni nani? Anaishia tu kusema najua mnakula, msile hadi mvimbiwe. Disgusting!
Unajaribu kumtofautisha lakini Hesabu zinakataa.
 
Hee, uongo unakuwaje katika maoni? Nenda shule kaongeze elimu uwe na uwezo wa kuelewa mambo. NI nimesema watu wenye akili wataelewa, obviously wewe sio mmoja wao.
Hii tabia ya kujifanya una akili kuliko wote huwa inaboa hapo ilitakiwa umweleze vipengele gani Magufuli alivunjwa kwa ajili ya Taifa letu na vipengele gani Samia amevunja kwa ajili ya CCM na uongozi.
 
Back
Top Bottom