Sasa nina hakika CHADEMA haitakufa tena kwa matakwa ya binadamu

Nimefatilia mlolongo wa njia ilizopitia CHADEMA nikagundua iliwekewa mitego mingi Sana ili ife lakini haikufa.

Iliondokewa na viongozi wake nguli walioiinua kwa mikono,jasho na damu zao lakini haikufa....
CHADEMA ni mpango wa Mungu, yeyote, narudia tena yeyote atakayejaribu kuiua hakika ATAKUFA.
 
Nimefatilia mlolongo wa njia ilizopitia CHADEMA nikagundua iliwekewa mitego mingi Sana ili ife lakini haikufa.

Iliondokewa na viongozi wake nguli walioiinua kwa mikono,jasho na damu zao lakini haikufa...
Kwanza napenda kukujulisha kuwa uanasisa ni kazi ya kutafuta ajira. Chama kinapopata wabunge wengi na kura nyingi kinatengeza ajira kwa wanachama na viongozi. Wingi wa wabunge na kura unaongeza ruzuku kwa chama.

Chama kinaposhindwa kupata kura au wabunge mwisho wake ni kufa, kwa sababu uhai wa chama hasa katika nchi maskinbi kama TZ unategemea hasa ruzuku na labda uwekezaji wa chama. CHADEMA kama chama kichnga hakina mali au uwekezaji wowote. Kwa hiyo mategemeo yake ni ruzuku ya serkali pamoja na michango waliyokuwa wakipata toka wabunge wake.

Kurubuniwa wanachama wenye nguvu kunatokana au na siasa mbaya za kufkuzana (Zitto,Slaa) bila kujuwa na bhili hupunguza saana nguvu za chama. mCHADEMA imekuwa na msukosuko wa kuondokewa na wanasiasa wenye nguvu, aidha kwa sababu kuna watu wanakumbatiwa na wanadhani bila wao CHADEMA haitakuwepo. Kukisha kuwa na mawazo ya namna hii hukatisha tamaa viongozi wengine ambao huonekana kama wasaliti wanapojitokeza kugombea nafasi. Dr. Slaa aliondoka CHADEMA kwa sababu walimuengua kugombea na kumpa nafasi Lowasa mtu aliyejiunga na CHADEMA baada kupata matatizo kwenye chama chake. Zitto ambaye aliijenga sana CHADEMA aliwekewa mizengwa tu eti kwa sababu alitaka kugombea.

Cha ajabu CHADEMA ni haki kuwawekea wanachma wao mizengwe na kuwafukuza, lakini CCM ikiwaziodi kete maneno. Kwa nini mbowe huwa hata hataki kuwa na mpinzani? Yeye anaogopa nini watu kusimama kugombea uwenyekiti. Hivi anategemea kuwa Museveni wa CHADEMA?
 
Hapo ndiyo ujue kuwa Mungu yupo upande wa cdm chama pekee cha kuwapigania watanzania wa aina zote.
Kasma mnawapigania Watanzania kwa nini hawawachagui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…