Sasa tuhamasike, kuwa na akaunti za Benki ni rahisi. Miamala ya simu gharama hazivumiliki

Sasa tuhamasike, kuwa na akaunti za Benki ni rahisi. Miamala ya simu gharama hazivumiliki

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Sasa ni wakati wa benki kujitanua zaidi na kila mmoja ajitahidi kuwa na akaunti ya benki, japo na wao wana makato Ila haya ya simu ni makubwa mno, yaani kusafirisha milioni wanakata 31,000 kutuma na kutoa.

Sasa nitahamia Benki, au nitasafirisha pesa kwa Gari yaani basi, pia tujitahidi kujiunga internet banking ambayo ukienda cafe nusu saa 500 unafanya muhamala kwa Bei rahisi.

Gari pia nauza siwezi kununua mafuta.
 
The struggle is real

Sijui nani atasikiliza kilio hiki Ndugulile wizara haimfai 99.9%%
Unamlaumu Ndungulile, umesoma Finance act ya mwaka huu?

Hebu jiridhishe hapa utapata anayestahili hizo lawama
 
Attachments

Yeye kama waziri wa technojia ni lazima apitie mambo yote ya mawasiliano kwa ivo hii inamhusu kwa kiasi kikubwa!! Au lawama ziende kwa nani mkuu?
Narudia tena soma hiyo Finace act, kisha jikumbushe mchakato wa mabadiliko ya sheria unavyopaswa kua, mpaka kusainiwa kwake.
Usijibu for the sake yakutetea point. Jibu kwakua umeelewa.

Haya mabadiliko sio service providers waliojiamulia. Sheria imeintroduce Levy mpya kwenye mobile money transfer inayorange kwenye sh. 10/= mpaka 10,000/= kwa kila muamala.

So ukituma hiyo milioni moja Levy ni 10 to 10000.
Na unayemtumia akitoa, Levy ni 10 to 10000
Ukijumlisha na makato kama yalivyokuwepo ndo unapata hiyo 31+
 
Hela itabanwa kila sehemu, serikali si wajinga hivyo
Ndomaana Umasikini hapa itakua wa kudumu, saving ni ngumu huwezi kubakiza pesa ya development kabisa. Uchumi wa nchi unahitaji overhauling kupata mchumi nje ya CCM to fix it back.
 
Sasa ni wakati wa benki kujitanua zaidi na kila mmoja ajitahidi kuwa na akaunti ya benki, japo na wao wana makato Ila haya ya simu ni makubwa mno, yaani kusafirisha milioni wanakata 31,000 kutuma na kutoa...
Awamu ya TOZO hii. Hivyo tuendelee tu kuvumilia maumivu.
 
20210709_114339.jpg

Tozo hizi hakika ni kubwa Sana na hazibebeki. Zitafanya watu wengi sana sasa waache kufanya miamala kwa njia za simu. Tutapanga foleni benki na tutapeana fedha mkononi.

Hata kama mpokeaji yupo mkoa jirani ni bora kupanda basi ukampelekea hiyo milioni moja kuliko kuituma.

Mfano nauli ya kwenda na kurudi
Moro-Dar, Mwanza-Shinyanga, Mwanza-Geita, Mwanza - Mara, Mbeya- Iringa, Mtwara-Lindi, Dar- Tanga, Tabora -Kigoma, Dodoma-Singida, n.k haizidi Shs 20,000/= wakati kutuma kwa simu hata mtaa wa pili tu ni Shs 31,000/=

Kama chaguzi zingekuwa zinafanyika kihalali ccm wangekuwa wanawaogopa wananchi na hivyo wangekuwa wanapanga mipano isiyowaumiza wananchi kama hivi.

Anyway, tunahitaji katiba mpya
 
View attachment 1846638

Mkuu mara Mia upande basi tu
31800 kwa mil moja nauli ya Dar ni 7000 kwenda na kurudi 14000 dah wacha turudi kwenye ujima
 
Back
Top Bottom