Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi hiyo wizara kazi zao za kila siku nini?? Je wana idara huko mikoani? Nawaza kwa kina sipat jibu,Daktari wa binadamu na tahama wapi na wapi! Utawala pekee anaojua ni kusimamia wagonjwa, na mgonjwa hana kauli. Akiambiwa vua nguo, hana swali.
Sasa ni wakati wa benki kujitanua zaidi na kila mmoja ajitahidi kuwa na akaunti ya benki, japo na wao wana makato Ila haya ya simu ni makubwa mno, yaani kusafirisha milioni wanakata 31,000 kutuma na kutoa.
Sasa nitahamia Benki, au nitasafirisha pesa kwa Gari yaani basi, pia tujitahidi kujiunga internet banking ambayo ukienda cafe nusu saa 500 unafanya muhamala kwa Bei rahisi.
Gari pia nauza siwezi kununua mafuta.
Sahizi kama mtu yuko jirani apande pikipiki tu afate hela!Inaumiza sana.tutakuwa tunapeana pesa mkono kwa mkono maana haya ni maumivu makubwa sana.pesa hakuna mtaani alafu iingie hyo mkate pakubwa hvyo.hapana kabisa.
duhh,Internet bank ni nafuu kweli ila kwa benki kama CRDB hawataki kabisaa watu wajiunge na hiyo huduma kwakuwa inawakosesha mapato, niliomba hiyo huduma kwa mara ya kwanza, nilijibiwa baada ya miezi 6 kupita. Mfumo wao ukazingua, nikaenda wa-reset password tu, nikakalishwa kwenye foleni siku nzima, ikapita miezi 6 tena, kwenda kuulizia tena, wakanipa fomu nijaze upya, kimbembe kikawa kwenye sahihi, wanasema haifanani na niliyosaini miaka 10 nyuma, kuwa kuna tofauti kidogo hivyo hawawezi kunipa hiyo huduma mpaka nipige sahihi kama ile.
Nikaona sio kesi, nitakapofikia maamuzi, i will kiss them good bye
Bank gani account maintenance ni 10,000?Benki pia ni gharama na ina usumbufu fulani, account mantainace fee kila mwezi 10000 to 20000, atm muamala 1000 to 1500, kupada boda utafute Atm kwanza ziko mbali sana, bora kupunguza miamala esio ya lazima tu.
Hili halikupangwa kweli na wizara ya fedha katika kutafuta vyanzo vya mapato ya serikali?Yeye kama waziri wa technojia ni lazima apitie mambo yote ya mawasiliano kwa ivo hii inamhusu kwa kiasi kikubwa!! Au lawama ziende kwa nani mkuu?
Hii ndio impact ya kuondoa wabunge makini bungeni kama akina zito kabwe,john mnyika ,nk !!!!Wabunge wapumbavu sana..yapo yapo tuu