Sasa tumemuelewa Rais Samia Suluhu. Kazi iendelee!

Sasa tumemuelewa Rais Samia Suluhu. Kazi iendelee!

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
373
Reaction score
467
SASA TUMEMUELEWA RAIS SAMIA SULUHU KAZI IENDELEE

Kwa heshima na taadhima kwa niaba ya wapenda maendeleo napenda kutoa shukurani za dhati kwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kwa jitahada zake za dhati za kulirejesha taifa katika umoja wake na mshikamano kuanza kuzaa matumaini.

Hakika Tanzania Kama taifa tumepitia kipindi kigumu Sana baada ya kumpoteza mpendwa wetu aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John pombe Magufuli, kwani ni Mara ya Kwanza kwa Tanzania kupata pigo la kuondokewa na Rais akiwa madarakani.

Kutokana na takwa la kisheria na kwa Mujibu wa katiba yetu pendwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempasa aliyekuwa makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kupokea kijiti na kuendeleza hatamu ya uongozi na kwasasa yeye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya sita.

Macho na masikio ya Watanzania yalikuwa na shauku ya kuona na kujua vipi serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia itaweza kuendeleza maendeleo yaliyofikiwa na serikali iliyoongozwa na Hayati Magufuli.

Waswahili husema dalili ya mvua ni mawingu na mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,tukiweka pembeni itikadi zetu kisiasa ukweli wa Mambo unaonekana kwani mwenye macho haambiwi ona, Rais Samia Suluhu Hassan anakila dalili za kutuvusha tukiwa salama na hilo linadhihirika katika vitendo vyake na kauli zake zilizojaa hekima na busara ya hali ya juu.

Rais Samia Suluhu akiwa Kama kiongozi mkuu wa serikali amejipambanua kwa Mambo mengi mazuri na yenye kutia faraja.
Rais Samia Suluhu anasisitiza upendo na umoja wa kitaifa ilikujenga nchi yenye mshikamano.

Rais Samia Suluhu anaonesha kwa vitendo kuwa anachukia rushwa na ufisadi ikiwa ni miongoni mwa changamoto kubwa zilizo fanikiwa kudhibitiwa kwa hali ya juu na mtangulizi wake.

Rais Samia ameahidi kuendeleza miradi ya kimkakati iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano na pia anamatarajio ya kuanzisha miradi mipya yenye tija na maslahi makubwa kwa taifa.

Rais SAMIA ameonesha kwa vitendo kuwa yeye ni muumini wa demokrasia na Uhuru wa vyombo vya habari na katika hili tunatarajia kuona muswada wa mabadiliko ya baadhi ya vipengele kandamizi ili vifanyiwe maboresho katika Sheria ya habari.

Rasi Samia ni mchapakazi na mzalendo wa kweli hatunashaka na hilo kwakuwa tunajionea wenyewe kwa macho yetu namna anavyojituma na kujitoa kwa aajili ya maslahi Watanzania.

Rais Samia amesheheni hekima na busara za hali ya juu pamoja na karama ya uongozi silka ambazo ni nadra Sana kupatikana kwa baadhi ya viongozi.

Tunashukuru Mungu kwa kutupa tunu ya kutunukiwa Rais Bora Kama huyu, Sasa tutembee kifua mbele kwa kuwa Tanzania tunayoitaka inakuja.

Japo ni mapema Sana lakini kwakweli tumepata tumaini kwa Mama, tuondoe Shaka juu yake,tumpe muda atujengee nchi yetu,tumpe ushirikiano wa dhati ilikufikia Tanzania ya maendeleo tuitakayo.

Ni dhahiri kuwa Sasa watanzania kiu yetu imepoa na hofu yetu imeondoka na Imani yetu imerejea,kwa kuwa Rais Samia anatufanya tuamini tupo salama chini ya uongozi wake.

Rais Samia ameonesha kuwa yeye ni CCM na atatekeleza ilani ya CCM Kama mtangulizi wake na ametuhakikishia kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja.

Tuweke tofauti zetu kando tuungane kwa pamoja ilituweze kuwashinda maadui zetu wasiolitakia mema taifa letu. Mwisho kwakuwa Mama tumemuelewa Sasa tuache kazi iendelee ili tusonge mbele.
 
Akitaka kuanguka afate foot step za jiwe! Ataanguka mbaya mbovu! But she is intelligent enough hawezi kufuata utoto kama ule ana washauri wazuri sana yani alivyoanza tuu ni wazi hatafata upuuzi.
 
Get to work. Kelele Zipungue.
 
Back
Top Bottom