lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Mimi naamini kua Kwa Sasa Urusi Iko vitani na NATO.
Nae USA ni Mkuu wa NATO.
Lkn wapo pro NATO wanakuambia hapana Urusi Iko vitani na Ukraine peke yake,NATO haimo,wanaenda mbele Wana sema nchi ndogo TU ya Ukraine Urusi imechukua miaka miwili kuishinda je hii Urusi ndio ya kupigana na NATO?.
Haya tuache hapa kwanza .
Wapo Pro USA,NATO na west humu,sijui hua wanafikiri kwa kutumia viungo Gani zaidi ya ubongo.
Wengi au wote kwa pamoja Kila siku wamekua wakisema kua Urusi hakua na haki ya kuivamia Ukraine Kwa sababu inataka kujiunga na NATO,wanasema Urusi Haina haki kwa sababu suala la kujiunga na NATO ni halali ya Ukraine Kwa kua Ukraine ni taifa huru na Lina maamuzi yake,na uhuru wake wa kujichagulia rafiki au kujichagulia upande wa kushirikiana nayo.
Hawa watu tuliwaelewesha sana kua Ukraine anakosea kumkaribisha adui namba moja wa Urusi hapa duniani ambae ni USA kwa sababu za usalama wa Urusi,lkn watu humu walikataa kuiona sababu hiyo.
Sasa wala hatujafika mbali Leo hii majibu tumeanza kuyapata live kabisa wala bila chenga mara baada ya Urusi kupeleka melivita na NYAMBIZI huko Cuba.
Majibu yenyewe ni kwamba mara TU baada ya Urusi kufikisha hizo silaha zake Kali kabisa huko Havana Cuba,nchi ya Marekani ilipaniki vibaya sana na kuanza kutoa kauli zinazopingana.
Lakini kubwa na baya kuliko yote ni kua nayo Marekani ilipeleka silaha za aina mbalimbali katika eneo hilo la maji kati ya Cuba na mji wa pwani wa Marekani wa Miami.
Marekani imepeleka makumi ya helkopta,ndegevita,ndege za upelelezi,melivita,NYAMBIZI na boti maalumu za kutafuta NYAMBIZI,pamoja na silaha nyingi nyinginezo ambazo Mimi bado sijapata kuzifahamu.
Sasa hapa ndio kwenye majibu ya ubishi wetu wa mda mrefu humu kati ya sisi Pro haki na wenzetu Pro USA NATO na west.
Majibu yenyewe ni kwamba:
kama Ukraine ni nchi huru na Ina haki ya kujichagulia marafiki na ina haki ya kujiunga na NATO je Cuba sio nchi huru kukaribisha rafiki yake wa jadi Urusi kupeleka meli na NYAMBIZI zake Havana kwa ajili ya kufanya mazoezi?
Si tuna amini kua Urusi haiko vitani na Marekani,je ni Kwa Nini na kwa sababu Gani Marekani imepeleka silaha zake pwani ya Miami eneo jirani kabisa na Cuba mara baada TU ya Urusi kupeleka meli zake Cuba?
Kwa Nini ifanye hivyo wakati hakuna ugomvi baina Yao?
Je Marekani inapopelekaga meli zake black sea mbona Urusi hua Haina hofu na vurugu kama ambazo Marekani imezionesha mara baada ya Urusi kutia nanga Cuba?
Kwa kifupi Marekani imeingiwa na hofu kubwa ,je hofu hiyo yanini?
Maana alivyofanya Urusi ndivyo Marekani hufanya katika maeneo jirani na Urusi.
Kwa msiofatilia tukio hilo ni kwamba marekani imelalamika sana,wameongea Kila maneno na mengine kupigana,lkn neno moja kubwa ambalo Mimi nimelikumbuka ni kusema hii ni "Provocation" na kuiomba Urusi iondoe meli zake.
Urusi wala hawakua na hofu Bali walisema toka mwanzo kua meli hizo zitakaa siku 6 TU na zitaelekea Venezuela.
Hofu iliyopo huko Washington ni kwamba huenda meli hizo zimeshusha mzigo wa Nyukilia hapa Cuba na mzigo mwingine utapelekwa Venezuela.
Hofu imetawala sana huko Marekani.
Majibu mengine ni nje ya mada. Kwa miaka mingi tuliambiwa Marekani na west ni mababa wa Demokrasia na uhuru wa habari,uhuru wa kujieleza na uhuru wa kusafiri.je tulidanganywa au muda wa ku prove ulikua hatujafika?
Iko hivi:
Mmarekani mmoja kati ya wamarekani wengi ambae amekua akizikosoa sera za mambo ya nje za Marekani za uchokozi na undumilakuwili wa taifa lake,amekua akizikosoa vita ya Ukraine na Israel kua chanzo ni taifa lake.bwana huyo amekua akilaani vikali matumizi mabaya ya Hela za walipa Kodi wa USA. Na Kupelekea Vifo visivyo na sababu vya vijana na watu wa Ukraine Kwa sababu TU ya uchokonozi wa Marekani dhidi ya Urusi.
Huyu bwana sio mtu mdogo,bali ni mwanqjeshi wa zamani wa Marekani,Jasusi na mkaguzi wa silaha za Iraq anaitwa Scott Ritter.
Huyu bwana amekua akisafiri sehemu mbalimbali ulaya na Asia kwa mambo yake binafsi na amekua akihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kutoa maoni yake kuhusu vita ya Ukraine na vita vya Palestine,lakini kwa kweli amekua akipinga vita zote na kusema chanzo ni nchi yake.
Sasa juzi kati hapa alialikwa kwenye kongamano la kimataifa nchini Urusi katika mji wa St Petersburg.
Kichekesho ni kwamba Mwamba huyu akiwa tayari ndani ya ndege alishushwa na maafisa usalama wa Marekani na mizigo yake na kunyang'anywa Pasi yake ya kusafiria,alipouliza sababu akajibiwa kua wao wamepewa maagizo kutoka juu
Je Demokrasia na uhuru wa kujieleza umekwisha Marekani?
TUMEPATA MAJIBU hapa
Angekua ni raia wa Urusi ndio ambae angetaka kuondoka Urusi kwenda ulaya ama Marekani kafanyiwa hivyo na serikali ya urusi,naamini vyombo vyote vya habari vya west vingelitangaza tukio hilo na hata channel 10 ya Tanzania ingeamrishwa kutangaaza tuko hilo.
Mbali na hiyo, kuna kiongozi mmoja wa nchi za ulaya alikusudiwa kuuwawa lkn akajeruhuiwa vibaya sana na Sasa Yuko hospitali mahututi, huyu nae ni mpinga vita vya ukraine. Wapenda vita wakaona ni kikwazo Cha ajenda zao wakapanga kumla kichwa lkn Mungu hakuridhia.
Huyu angekua ni kiongozi wa Urusi,nadhani Kila siku kwa mwaka mzima vyombo vya west vingelitangaza tukio hilo.
Haya yote ni majibu tumeyqpata katika mgogoro huu wa Ukraine na Urusi.
Ma Pro USANATO tunaomba mtuambie je Cuba sio nchi huru?
Haina haki ya kuchagua upande?
Kosa la Cuba nini au Cuba alimkosea ni USA hata kumuwekea vikwazo vikali na vya maisha?
Je, Ukraine ndio mwenye haki ya kujiunga na NATO lkn Cuba Hana haki hiyo.
Je, Urusi Haina haki ya kupeleka silaha kwa marafiki zake kwa ajili ya kufanya mazoezi?
Tujadili.