Sasa unaweza kumpa mnyama jina lako kwa Tsh Milioni 5

Sasa unaweza kumpa mnyama jina lako kwa Tsh Milioni 5

Wakiweza kudhibiti ujangiri ama uwindaji haramu...Hilo litaleta manufaa sana...ila kinyume chake nadhani mpaka kufikia 2033 mbuga itakayokuwa na wanyama ni kitanda TU chenye kunguni🤣🤣🤣🤣
 
Hivi faru fausta yuko wapi siku hizi? Kuna member humu anajiita bujibuji simba nyanaume ahawi ofa akampe simba jina lake. Kina diamond wanajii simba nao wawahi.

Wapo wanaojiita chui, mamba ndege na nyumbu, tangazo ndio hilo wakatoe majina yao kwa wanyama wanaowapenda
 
Hili suala binafsi sijalielewa limekaa vipi
Yaani ulipe pesa alafu urudi nyumbani sasa itakuwa ndio nini
Btw kuna yule faru mtoto wa malkia alimpa jina lake nasikia wahuni walilamba kichwa sijui ni kweli
Hapo Ni kipengere labda wangesema ukilipa hicho kiasi Cha M 5 unakuwa unapewa gawio kila mwaka na idara huska Kama hisa
 
Kwanini wasituuzie tule nyama?tuanze ujinga wa kuwapa majina ili iweje?
Marketing and Branding, mbona mashule au taasisi yanapewa majina ya MaRais au watu mashuhuri wa eneo husika. Ukilitumia kiuchumi linakubeba mfano mtu akisikia Emirates Stadium wa Arsenal tayari ni branding ya Fly Emirates.
 
Nina Majibwa 5 na yote nimeyapa majina ya watu.
La kwanza

MAGUFULI.. . 5MILION
SADAM HUSEIN . 5MILION
PUTIN.. .5MILION
GADAF.... 5MILION
FIDEL CASRTRO... 5MILION

TOTAL 25MILION...Nitumien control mamba nilipie chap
 
#HABARI Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)limeanzisha programu maalum ya mtu anayetaka kuasili ama kumpa mnyama jina lake anaweza kufanya hivyo lakini kwa kulipia fedha za kitanzania milioni 5 ambayo itatolewa na mwenye jina na kupewa kibali.

Hilo limekuja baada yakuonekana baadhi ya majina ya binadamu wanayopewa wanyama kuvutia watu wengi hali ambayo imewasukuma mamlaka hiyo kuanzisha utaratibu huo na fedha zitakazopatikana zinakwenda kuendesha shughuli za utunzaji wanyamapori na uhifadhi mali asili ya nchi.


Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom