Sativa aeleza kwa kina tukio la Kutekwa Dar: Kasi, vitisho na safari hadi Arusha

Sativa aeleza kwa kina tukio la Kutekwa Dar: Kasi, vitisho na safari hadi Arusha

JamiiForums

Battle ya Sativa vs ZCO Faustine Mafwele bado mbichi​

First Prev2 of 3Next Last
Subscribe
•••
[IMG alt="Stuxnet"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/37/37228.jpg?1571598149[/IMG]

Stuxnet

JF-Expert Member​

12. Yuko tayari kwa lolote katika battle hii

View: https://x.com/Sativa255/status/1834160655663772095?t=i7DBdZVnB5Bmb7O9mO37WQ&s=19

Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="Lucha"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/502/502767.jpg?1708874513[/IMG]

Lucha

JF-Expert Member​

Naamini huyo Mafwele atamtafuta Sativa wakiwa wawili tu wamalize tofauti zao

Thanks Quote Reply
Report
Reactions:Stuxnet and Seth saint
[IMG alt="Stuxnet"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/37/37228.jpg?1571598149[/IMG]

Stuxnet

JF-Expert Member​

13. Anasema Polisi wakimuua yeye yuko mwenzie Tavina, na wakiwaua wote ipo Gen Z

View: https://x.com/Sativa255/status/1834164149535793497?t=ppoJS1kU4O09SdilG4Chsw&s=19

Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="Bubu Msemaovyo"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/2/2872.jpg?1205240816[/IMG]

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member​

Nitaweka mfulizo wa posts za Sativa kutoka kwenye ukurasa wake wa Twitter akimshutumu ZCO Faustine Mafwele kuwa ndiye kinara wa utekaji na uuaji unaotekelezwa na taasisi za Serikali dhidi ya wakosoaji/ wanaharakati wa siasa.

1. Namna alivyomtambua ZCO MAFWELE

View: https://x.com/Sativa255/status/1833929192569790685?t=BVXlaYncA5lCPAmQwUV_tg&s=19
Click to expand...
Mara nyingi nikiangalia picha ya huyu mtu, kwa jicho la tatu, huyu ameanza kutafunwa na nafsi yake. Damu alizomwaga ni nyingi sana. Hana raha ya kipato anachopata, watoto wake wanalipiwa kwa fedha ya damu za watu masomo yao hayana baraka ya Mungu. Mkewe akivaa akadhani kapendeza ni mavazi ya damu za watu.
Muuaji wa kwanza tangu ulimwengu kuumbwa alikuwa Kaini.
Baada ya Kaini kumuua Abel, Kaini alichimba shimo akamfukia, damu ya Abel ikamlilia Mungu, Mungu akasikia kilio cha Abel. Mungu akamuita Kaini, naye akaitika Mungu akamuuliza yu wapi Abel ndugu yako? Kaini akamjibu ovyo sana Mungu eti kwani mimi ni mlinzi wake?

Majibu ya ovyo ya Kaini kwa Mungu ni dailies ya kufadhaika kwa nafsi ya Kaini. Ndivyo wauaji wanavyofadhaika. Mwisho wataanza kuelezea kwa watu kuhusu maovu waliyotenda na kamwe haitasaidia.
 
JamiiForums

Battle ya Sativa vs ZCO Faustine Mafwele bado mbichi​

First Prev2 of 3Next Last
Subscribe
•••
[IMG alt="Stuxnet"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/37/37228.jpg?1571598149[/IMG]

Stuxnet

JF-Expert Member​

12. Yuko tayari kwa lolote katika battle hii

View: https://x.com/Sativa255/status/1834160655663772095?t=i7DBdZVnB5Bmb7O9mO37WQ&s=19

Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="Lucha"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/502/502767.jpg?1708874513[/IMG]

Lucha

JF-Expert Member​

Naamini huyo Mafwele atamtafuta Sativa wakiwa wawili tu wamalize tofauti zao

Thanks Quote Reply
Report
Reactions:Stuxnet and Seth saint
[IMG alt="Stuxnet"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/37/37228.jpg?1571598149[/IMG]

Stuxnet

JF-Expert Member​

13. Anasema Polisi wakimuua yeye yuko mwenzie Tavina, na wakiwaua wote ipo Gen Z

View: https://x.com/Sativa255/status/1834164149535793497?t=ppoJS1kU4O09SdilG4Chsw&s=19

Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="Bubu Msemaovyo"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/2/2872.jpg?1205240816[/IMG]

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member​

Mara nyingi nikiangalia picha ya huyu mtu, kwa jicho la tatu, huyu ameanza kutafunwa na nafsi yake. Damu alizomwaga ni nyingi sana. Hana raha ya kipato anachopata, watoto wake wanalipiwa kwa fedha ya damu za watu masomo yao hayana baraka ya Mungu. Mkewe akivaa akadhani kapendeza ni mavazi ya damu za watu.
Muuaji wa kwanza tangu ulimwengu kuumbwa alikuwa Kaini.
Baada ya Kaini kumuua Abel, Kaini alichimba shimo akamfukia, damu ya Abel ikamlilia Mungu, Mungu akasikia kilio cha Abel. Mungu akamuita Kaini, naye akaitika Mungu akamuuliza yu wapi Abel ndugu yako? Kaini akamjibu ovyo sana Mungu eti kwani mimi ni mlinzi wake?

Majibu ya ovyo ya Kaini kwa Mungu ni dailies ya kufadhaika kwa nafsi ya Kaini. Ndivyo wauaji wanavyofadhaika. Mwisho wataanza kuelezea kwa watu kuhusu maovu waliyotenda na kamwe haitasaidia.
Kusema ukweli ningekuwa mimi ndiyo Sativa, sasa hivi ningekuwa nakesha kwenye nyumba za ibada hata ya matambo na bifu ningeachana nayo
 
Kusema ukweli ningekuwa mimi ndiyo Sativa, sasa hivi ningekuwa nakesha kwenye nyumba za ibada hata ya matambo na bifu ningeachana nayo
Ndo maana wewe si Sativa, kuna watu wameumbwa hivo huwezi wabadilisha. Kuna mwingine akiingia tu rumande ya polisi hatamani kurudia kosa. Lakini wengine anaiba anafungwa akiwa gerezani anaendelea kuiba na akitoka anaiba na kurudishwa tena jela
 
Hili ndio gari walilolitumia kunisafirisha kutokea DAR (kituo cha polisi OSTABAY siku ya 24/6 "jumatatu" majira ya saa 0520- 0525).

Nilifunikwa na mzura (zile mask zenye matobo ya macho na mdomo) ila hayo matundu waliyageuzia kwa nyuma kwenye kisogo.

Hii gari ilitembea speed kubwa sana kwenye 120 - 140. Nilijua hii speed baada ya wao kwa wo kuanza kuzozana baada ya kuwa wamevuta BANGI SANA NA POMBE NYINGI.

Mmoja akaanza kuingia mashaka na dereva kuwa "kuwa makini saizi ni usiku afu umevaa miwani ya tinted utatuletea shida"

Ndipo dereva akajibu kwa kupanic "yani mchana wote nilikuwa natembea na speed ya 120-140-160 saizi natembelea 100 unaniletea mawenge yako" akaanza kutukana matusi.

Hili gari nililijuaje kama ni "HILUX 4X4 DOUBLE KAB".

Kuna muda baada ya kuulizwa maswali na kuna tuhuma walitaka kunipa ambayo mimi niliona kabisa natenda kuteswa kwa kosa la kuonewa TUMBO LILIVHAFUKWA nikaomba nijisaidie haja kubwa.

Tumbo lilianza kuunguruma wakaona wanishushe PORINI na kunitoa mask na pingu na kuniambia nisimame pale nijisaidie.

Wakati huo nimeshushwa ndio nikawaona wao body structure zao wakiwa na miili mikubwa sana (WANATISHA SANA).

Wakaniambia "unaiona hii?" Nikajibu ndio naiona. Ilikuwa ni Bastora ndogo. Wakaniambia "fanya usenge tukumwage ubongo". Wakanipa maji ya kujisafisha.

Ikabidi nitoe nguo muda huo waniangalia, kiukweli sikuweza kufanya lolote ikabidi nisimame nivae nguo nigeukie lilipo gari.

Hapo ndio nikalijua gari.

Lilikuwa gari aina ya HILUX DOUBLE KAB.

Rangi ya kijivu.

Plate number haikuwa yenye usajilu wa TANZANIA zilikuwa namba nyingi nyingi kama zile gari za usajili kutokea "South Africa"

Nikapigwa Pingu na mask na kurudishwa kwenye gari na safari kuendelea.

Saizi nilipelekwa kituo cha polisi ARUSHA ambacho sikukijua jina ila niliweza kukijua kuwa ni kituo cha polisi kwa rangi nilizoziona zimepakwa ukutani pale mapokezi (blue & white).

Lakini pia kuna muda nililetewa chakula na Mapolisi waliovalia sare za jeshi la Tanzania kabisa.

MAFWELE HAWA WATU NDIO ALIOWAAMBIA WALE MAPOLISI WA OSTABAY KUWA WANIFUNGE PINGU KUNA WATU WATAKUJA KUNICHUKUA.

HAWA WATU MAFWELE ANAWAJUA VIZURI SANA NA NDIO ANAWAFADHIRI HUKO MBELE MTANIELEWA VIZURI SANA.

MAFWELE MUACHIE SOKA NA WOTE ULIOWATEKA MAANA ISHAKUWA NOMA, MIMI KABLA HUJAJA KUNIUA MARA YA PILI DUNIA ITAKUWA ISHAJUA KILA KITU KUHUSU WEWE.

SATIVA17🫡
 
Attachments

  • 31DC5651-3449-4D92-B294-258AC15C4EC1.jpeg
    31DC5651-3449-4D92-B294-258AC15C4EC1.jpeg
    54.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom