SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Oysterbay kabla ya kusafirishwa sehemu nyingine na nimepigwa risasi ya kichwa

SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Oysterbay kabla ya kusafirishwa sehemu nyingine na nimepigwa risasi ya kichwa

Sio justification ya kutekwa na kufanyiwa huo unyama ,ni ushenzi wa serikali ya ccm na vibaka wao ,wanaojiita vyombo vya usalama kufanya vitendo vya kijambazi kama hivi na kuleta justification za kipuuzi kama hizi
Na Wewe nenda katukane basi upate hio justification within few day's ungependa tukuokote msitu gani?
 
Nimesikia watangazaji fulani wakisoma magazeti kwa mbwembwe yani machawa wale wanaonekana kupingana na huyo jamaa.
Waandishi wanaoshabikia mambo hata yasiyona ulazima wa kushabikia wanatia aibu na wanaaibisha media zao
 
Shulee tatizoo ndo maana lazima ushangae
Ni kweli Mkuu nimeishia la tatu C, lakini uzoefu nilionao katika kuangalia sinema za Rambo, Anorld na Van Dame umenifanya nione kabisa jamaa anatulisha matango pori.
Yaani kitu cha Norinco au TT-30, kipite kichwani halafu kwa kupata huduma ya kwanza tu kwenye kituo cha afya uanze kunyooka kuelezea tukio vizuri kabisa.
Shame on you na elimu yako ya makaratasi.
 
Sure maana Pori la katavi lina simba wala watu na pia wasiojilikana wamemiss-target ya kupiga kwenye ubongo wakapiga kwenye TAYA ,jamaa bado kazi aliyotumwa hajaikamilisha.

Kumbuka Alipelekwa Arusha kisha KATAVI.

->Kama lengo lilikua kumpeleka Katavi, njia rahisi ingekua kupita Mbeya au Tabora. Kwanini wazungukie Arusha? Walienda kumfuata nani Arusha?

->Je aliyeorganize unyama huo yupo Arusha? Ni nani anaishi Arusha mwenye uzoefu wa kuteka, kutesa na kuua?

Lissu alivyopigwa risasi ,kuna mtu alionekana Dodoma siku ya Tukio na hakuwepo kabisa kwenye sherehe za ikulu ambapo si kawaida yake ,kutekwa kwa Sativa na kupelekwa Arusha ,KUNANI?
Sawa, haya tuambie sasa kwann Katavi na sio sehemu nyngn mana inaonyesha una details nyingi
 
wamemfilimbaa huyo hatakaa atukane serikali kamweer

View attachment 3027767
Edger Mwakalebela maarufu kama Sativa ambae anadaiwa kutekwa Dar es Salaam siku chache zilizopita amesema baada ya kutekwa alipelekwa kituo cha OysterBay.

Sativa ameyasema hayo wakati akiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe alipokuwa akipatiwa matibabu kabla ya kupelekwa hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi huku Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Martin Lohay akithibitisha kumpokea akiwa na majeraha.

Pia soma
Kutoka Kwa Martin
KUTEKWA, KUPOTEA, KUTESWA, KUPATIKANA KWA SATIVA. 💔


Maelezo yote yametoka katika kinywa cha Edgar Edson Mwakabela, @Sativa255 ambaye alitekwa jumapili 23.06.2024 Darces Salaam na kupatikana 27.06.2024 Katavi.


Shughuli inaanza siku ya Jumapili, 23.06.2024, maeneo ya Ubungo. Edgar Edson Mwakabela aliagana na kaka yake Patrick, na akaanza safari ya kurudi Kimara.


Walitoka wote Coco Beach. Baada ya muda, Patrick alimuuliza kama amefika salama, hakujibiwa ujumbe wake, na simu za SATIVA baada ya hapo hazikupatikana tena.


SATIVA alikuwa anatafuta chumba, wakakubaliana na dalali kwamba hiyo sehemu ambayo anataka kuhamia, mpangaji katika nyumba hiyo anatoka mwezi wa (10) Oktoba.


Baada ya muda mfupi, dalali akarudi kumpigia simu SATIVA akimueleza kwamba jamaa katika nyumba ile ametoka hivyo anaweza kufanya malipo yake muda huo.


Wakati huo, SATIVA alikuwa amewaaga rafiki zake aliokuwa nao, akawa amechukua usafiri wa bodaboda, alipopigiwa simu na dalali, akabadilisha bodaboda yule.


Wakati akishuka na kutafuta bodaboda nyingine kueleka alipo huyo dalali, akawekwa mtu kati na watu watatu. Wakamfunga pingu na kumtupa katika gari waliyokuja nayo.


Watekaji hao walimpokonya simu zake zote tatu. Simu mbili walizima. Simu moja ikabaki hewani kwa muda mfupi, baadae simu zote za SATIVA zikawa hazipatikani.


Wakaondoka naye hadi kituo cha Polisi Oysterbay, Mkoa wa Kipolisi - Kinondoni. Hapo wakamfikisha nyuma ya kituo cha Polisi Oysterbay, wanapaita 'karakana"


SATIVA akiwa karakana hapo majira ya saa 2 usiku, waliendelea kumuuliza, kosa lako ni lipi? Umewakosea jambo gani wakubwa hadi kuagiza ukamatwe na kuteswa?


Inavyoonekana, watekaji hao walikuwa na maelekezo ya kumteka SATIVA tu lakini hawakujua kwanini wametumwa kumteka. SATIVA aliwaambia hajui kitu yoyote.


Lakini katika maswali yao ya msingi waliendelea kumuuliza, rafiki zako ni akina Martin Maranja Masese na Boniface Jacob? Mnakutana wapi kupanga mambo yenu?


Akiwa hapo karakana ya magari ya kituo cha polisi Oysterbay, alifika mtu mmoja akiwa ndani ya gari aina ya VX V8 akashuka akiwa amevaa jezi ya timu ya Simba SC.


Mtu huyo chini alivaa pensi ya rangi ya kaki. Kwa muonekano wa nje alikuwa ni mtu wa mazoezi, mrefu wa wastani na siyo mweupe sana. Huo ni wajihi wake wa nje.


Mtu huyo aliposhuka kwenye gari akiwa pekee yake, wale waliokuwa pale walimpigia saluti, akamfuata moja kwa moja SATIVA pahali alipokuwa amefungwa pingu mikononi.


Akamuuliza, unaitwa nani? Katika mitandao ya kijamii unatumia jina gani? SATIVA akampa majibu. Baada ya hapo akawavuta pembeni wale watu waliokuwa na SATIVA pale.


Akatoa maelekezo kuwa kuna watu watakuja kumchukua SATIVA, afungwe katika Karakana ya Oysterbay. Akarudi katika gari aliyokuja nayo, ikawashwa, akasepa.


Usiku huo, SATIVA akafungwa pingu katika moja ya nguzo zilizopo katika hiyo karakana ya Polisi - Oysterbay. Wakiendelea kumuuliza SATIVA amekosa nini kikubwa hicho?


Wao walishangaa kiongozi mkubwa kufika hadi hapo Karakana ya Polisi - Oysterbay na kumuhoji SATIVA, jambo ambalo kwao siyo kawaida. Wakajiuliza, kosa lake nini?


Kwamba kiongozi mkubwa ameacha shughuli zake usiku hadi kumfuata hapo, kosa lake ni nini? SATIVA akawaambia kwa kweli hata mimi sijui gani nimefanya hadi sasa.


Kwa maelezo ya SATIVA anasema watu hao watatu waliomkamata awali, hawamkupiga isipokuwa waliendelea kumuuliza makosa yake hadi kuagizwa kuletwa hapo.


Tangu alipofikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay saa mbili na dakika 25 usiku, akafungwa pingu katika hizo bomba za karakana, amefuatwa alfajiri ya kesho yake.


Ilipofika saa 12 alfajiri ilimfuata gari ambayo haina 'playe number' za Tanzania. SATIVA akachukuliwa na kuwekwa katika gari hiyo, na huko ndani akakutana na sura mpya.


Hapo, wale waliomkamata tangu siku ya 23.06.2024 wakawa wamemaliza wajibu wao, akakutana na watu watu waliopewa kazi maalum ya kumtesa na kumuua.


Kitu cha kushangaza zaidi, ndugu na rafiki zake SATIVA walifika hadi kituo cha polisi Oysterbay, wakaelezwa mtu wa aina hiyo hajawahi kufikishwa kituo hicho cha polisi.


Polisi walipewa taarifa ya kupotea kwa SATIVA, na ikafunguliwa jalada katika kituo cha polisi Gogoni - Kimara, na polisi wakatoa Report Book (RB) Na.


Bado ndugu na rafiki zake waliendelea kumtafuta vituo vya Polisi vyote vikubwa na hospitali hadi mochwari, bado SATIVA hakuonekana na polisi walisema hawajui.


SATIVA anasema wakaanza safari ndefu sana, gari ikiwa mwendo, akiwa amefungwa kitambaa usoni. Lakini katika maongezi yao walisema uelekeo wao ni Arusha.


Tangu amekamatwa jana yake, hiyo ni siku nyingine, SATIVA hakuwa amekula au kunywa kitu chochote. Walipofika Mkoa wa Arusha, SATIVA akaomba apewe maji.


Lakini, wakiwa ndani ya gari kabla ya kumshusha walibadilisha aina ya matamshi yao ili SATIVA asiwasome. Mfano ugali wao waliisema ugaliwa. Wali walisema waliwa.


Wakiwa Arusha, walimshusha, akapelekwa katika moja ya mahabusu katika Mkoa wa Arusha lakini hakufanikiwa kufahamu ni mahabusu ya kituo gani cha Polisi.


SATIVA anasema katika hiyo mahabusu amewekwa kwa siku mbili. Kwa mantiki hiyo ni 25/06/2024 na 26/06/2024. Siku hiyo pili wakamtoa ndani ya mahabusu hiyo.


Wakaondoka naye kama wanampeleka katika moja ya mipaka ya Tanzania na kenya. Wakaendelea kumuhoji huko, saa saba mchana wakarudi naye Arusha Mjini.


Wakaanza safari ndefu, anasema walipofika katika moja ya mapori ambayo hajui ni wapi, gari ile ilisimama, wakatoa panga kubwa na kuanza kumpiga bapa za panga nyingi.


Katika mazungumzo yao yote wakati wakimpiga SATIVA mabapa ya panga, walikuwa wakimuuliza kama anatumwa na Boniface Jacob na Martin Maranja Masese.


SATIVA aliendele kusema hawajui watu hao na hajawahi kukutana nao pahali popote. Wao waliendelea kumtesa wakisisitiza kwamba awataje hao watu wanaomtuma.


Mgongo wa SATIVA umevia damu nyingi sana. Mabapa ya panga pia alipigwa sana kwenye kichwa, mapaja na miguu. Akapata maumivu makali sana kwenye miguu na kichwa.


Walimpiga mabapa ya panga zao mengi kwa muda mrefu wakiendelea kumuhoji SATIVA nani ambaye anamtuma kukosoa serikali ya CCM na kutukana viongozi wa nchi.


Mahojiano yao na SATIVA yalijikita katika kufahamu kama Martin maranja Masese na Boniface Jacob ndiyo wanaomtuma kufanya shughuli za kukosoa serikali yao?


Baada ya mateso makali sana, kiongozi wa msafara akaamuru waende wakamalizane naye haraka muda huo. Hapo imefika majira ya nne usiku wakiwa porini sana.


Wakamfunga kitambaa, wakamrudisha kwenye gari na safari ikaanza. Wakijadiliana kwamba, Katavi kuna wanayama wakali na misitu minene, waelekee huko.


Wakafika Katavi saa 10 kuelekea saa 11 alfajiri. Wakaingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, pembezoni ya mto Ikuu ambao unatajwa kuwa na viboko na mamba wengi.


Wakaegesha gari na kuanza kuingia naye msituni. Kuelekea ulipo huo mto Ikuu. Huko mahojiano yakendelea wakati huo akipigwa mabapa ya panga kila pahali. Noma.


Kwa maelezo yake SATIVA anasema alipigwa pingu na kitambaa usoni. Na wakamueleza kwamba biashara yake itakuwa imeishia katika msitu wa hifadhi ya Taifa ya Katavi.


Kiongozi wa wauaji hao akatoa maelekezo kwa mmoja kati ya wauaji hao kwamba " mpige risasi huyo kibaka tumalizane naye twende zetu". Ikachapwa risasi kutoka kwa nyuma.


Risasi imepita kutoka kwenye upande wa kushoto wa kichwa, ikapita hadi kwenye shavu na kupasua taya mara mbili na kusaga taya. Damu zikamwagika nyingi akiwa chini.


Wakiwa hapo akasikia wakisema hapa kuna fisi wakali sana, ataliwa na fisi au mamba wakali kutoka katika mto huo au viboko wengi waliopo katika mto huo pembeni.0


Baada ya kama dakika mbili wakiwa hapo, akasikia wakiondoka, wakawasha gari. Akapoteza fahamu. Baadae akahisi mwili umepigwa baridi, akaanza kujivuta.


Akajivuta kwenda hadi ilipo barabara, na hapo ndipo akakutana na askari wa doria wa wanayamapori (TANAPA) na wakaanza kumuuliza maswali mengi ya ufahamu.


Sativa alipookotwa na hao watu wakiwepo askari wanyama pori Hifadhi ya Katavi, baada ya kumuhoji kidogo, akapelekwa kituo cha Afya Kibaoni njia ya kwenda Majimoto.


Na kuanzia hapo, hadithi nyingine yote mnaifahamu. Hivyo ndivyo rafiki yetu, Edgar Edson Mwakabela, SATIVA alivyotekwa na maharamia na kuteswa na kunusurika kifo.


NB; Kumbuka, hifadhi ya Taifa ya Katavi katika kundi la wanyama wakali kuna viboko 5,400. Simba 190. Fisi 750. Mbwa mwitu na Mamba sensa haijafanyika. Noma.


Martin Maranja Masese, MMM.
 
Sawa, haya tuambie sasa kwann Katavi na sio sehemu nyngn mana inaonyesha una details nyingi

Waulize watekaji kwanini walienda kumtupa kwenye hifadhi ya pori la KATAVi ,Dr Ulimboka aliokotwa Msitu wa PANDE tar 27-June-2012 na SATIVA aliokotwa PORI la KATAVI 27-June-2024.
 
Una uthibitisho wa Kisayansi mkuu?

Waliosomea masuala ya tiba hawajabisha, labda ni kwamba wanamuogopa au na wenyewe hawajui?
Yaani upigwe Bomba utisini itokee kwenye taya na uweze kuelezea tukio Zima la kutekwa!?
 
Back
Top Bottom