Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Ukikitana na Mtanzania anaipinga CCM na serikali yake basi ujue huyo tayari yupo kwenye list ya mashoga watarajiwa.
Maana wameona hiyo ndiyo namna ya kuwatisha na kuwazima watu
Sijui kwanini wanafanya hivyo, ukishatekwa na wasiojulikana ujue kuna namna inafanyika na hakuna anaesema.
 
Yule mtu mkubwa huwenda alipigwa vibao tu, ila vijana machachali kama hawa ni sekunde kuwafanyia mchezo mchafu...
Inasikitisha sana, ndio maana ni ngumu sana kufanya mabadiliko hapa kwetu.
 
Mkuu si rahisi kama unavyofikiria Roma mkatoliki ilikuwaje huyo NAE alikuwa na matatizo binafsi? Ukipelekwa huko huachiwi hivi hivi bila kupewa mwongozo
 
Edgar anaishi Mbezi kwa Msuguli na amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.
Bantu Lady usiseme sikukwambia unaona mwenzio hatimae alikua anapelekwa kwenda kusalimiana na Chatu na Wewe fanya fyoko Hawa hapa mlangoni kwako wapite na Wewe utafutwe ukutwe Mbugani huko unapambana na Uhai wako peke yako
 
Msiba huanza na wafiwa,Mimi ndio kwanza namsikia baada ya hizi.kelele zenu sijui hata huko Twitter alikuwa anakosoje.

Alikuwa chama gani?
 
Unatukana alafu unaonyesha Sura?
Alikuwa anatukana Viongozi tena matusi ya nguoni eti anamuiga Mdude,anatukana Kila mtu mwenye maoni tofauti na anasambaza taarifa za mgomo.

Siku nyingine hatorudia amejifunza kufunzwa na ulimwengu.

Binafsi Huwa Siwa follow watu wa hivyo japo mara Moja nikukuta post naweza wajibu ila wanaotukana hapana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…