Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Ukikitana na Mtanzania anaipinga CCM na serikali yake basi ujue huyo tayari yupo kwenye list ya mashoga watarajiwa.
Maana wameona hiyo ndiyo namna ya kuwatisha na kuwazima watu
Sijui kwanini wanafanya hivyo, ukishatekwa na wasiojulikana ujue kuna namna inafanyika na hakuna anaesema.
 
Mkuu si rahisi kama unavyofikiria Roma mkatoliki ilikuwaje huyo NAE alikuwa na matatizo binafsi? Ukipelekwa huko huachiwi hivi hivi bila kupewa mwongozo
yaani mtu hata akwa na matatizo yake binafsi mnasema mkosoaji katekwa sasa dawa ya hii kitu ajitokeze hazarani aseme alikuwa wapi na aliambiwa nini huko ili tujuwe kama kweli alitekwa sababu ya ukosoaji bila hivyo huyo ni mharifu tu kama wahalifu wengine
 
Edgar anaishi Mbezi kwa Msuguli na amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.
Bantu Lady usiseme sikukwambia unaona mwenzio hatimae alikua anapelekwa kwenda kusalimiana na Chatu na Wewe fanya fyoko Hawa hapa mlangoni kwako wapite na Wewe utafutwe ukutwe Mbugani huko unapambana na Uhai wako peke yako
 
Wakuu Salama,

Sativa amekuwa akitafutwa toka weekend (Jumapili - 23/6/2024), baada ya ndugu zake kumtafuta bila mafanikio.

Watetezi wa haki za binadamu wamepiga kelele kuhusu hili hata mmojawapo wa viongozi wa ACT Wazalendo Rahma Mwita alizungumza suala hili kwenye kwenye XSpaces jana 26/6/2024 kuwa yupo tayari kujitolea muda wake kuambatana na ndugu wa kijana huyo kwenda kwenye vyombo vya habari na asasi mbalimbali za kiraia kupaza sauti kuhusu kupotea kwa kijana huyu.

Edgar anaishi Mbezi kwa Msuguli na amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.


Kama kelele zisingepigwa huyu ndio ilikuwa ntolee, halafu kuna chawa wanaotetea ujinga kila siku.

Kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera kuhusu kuwapoteza watu soma hapa: Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

Aisee, wakati wa kubadilika ni sasa, mtu akipotea wote tupige kelele, serikali ikienda kushoto wote tupige kelele. Isiwe kazi ya wanaharakati wachache au watetezi wa haki za binadamu, peke yao hawawezi. Tukiungana wote tunakuwa na nguvu.

Tuendeleze hashtag Wakuu, #KataaMachawa #KataaUozo2025, amsha kila utakayeweza kumuasha, tushikamane na kuteteana wakati wote kuleta uwajibikaji nchini.
Msiba huanza na wafiwa,Mimi ndio kwanza namsikia baada ya hizi.kelele zenu sijui hata huko Twitter alikuwa anakosoje.

Alikuwa chama gani?
 
Msiba huanza na wafiwa,Mimi ndio kwanza namsikia baada ya hizi.kelele zenu sijui hata huko Twitter alikuwa anakosoje.

Alikuwa chama gani?
Huyu hapa anatema Cheche zake huko X
Screenshot_20240627-221949.png
 
Unatukana alafu unaonyesha Sura?
Alikuwa anatukana Viongozi tena matusi ya nguoni eti anamuiga Mdude,anatukana Kila mtu mwenye maoni tofauti na anasambaza taarifa za mgomo.

Siku nyingine hatorudia amejifunza kufunzwa na ulimwengu.

Binafsi Huwa Siwa follow watu wa hivyo japo mara Moja nikukuta post naweza wajibu ila wanaotukana hapana.
 
Back
Top Bottom