Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Wakuu Salama,

Sativa amekuwa akitafutwa toka weekend (Jumapili - 23/6/2024), baada ya ndugu zake kumtafuta bila mafanikio.

Watetezi wa haki za binadamu wamepiga kelele kuhusu hili hata mmojawapo wa viongozi wa ACT Wazalendo Rahma Mwita alizungumza suala hili kwenye kwenye XSpaces jana 26/6/2024 kuwa yupo tayari kujiyolea muda wake kuambatana na ndugu wa kijana huyo kwenda kwenye vyombo vya habari na asasi mbalimbali za kiraia kupaza sauti kuhusu kupotea kwa kijana huyu.

Edgar anaishi Kimara kwa Msuguli na amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.


Kama kelele zisingepigwa huyu ndio ilikuwa ntolee, halafu kuna chawa wanaotetea ujinga kila siku.

Aisee, wakati wa kubadilika ni sasa, mtu akipotea wote tupige kelele, serikali ikienda kushoto wote tupige kelele. Isiwe kazi ya wanaharakati wachache au watetezi wa haki za binadamu, peke yao hawawezi. Tukiungana wote tunakuwa na nguvu.

Tuendeleze hashtag Wakuu, #KataaMachawa #KataaUozo2025, amsha kila utakayeweza kumuasha, tushikamane na kuteteana wakati wote kuleta uwajibikaji nchini.
Pole nyingi kwake!!!
Btw usibishane na serikali!!!
 
Erythrocyte usimfanananishe na huyo mbubujikwa machozi Mwamala unaposoma.
Kwangu ukishakuwa chawa wa mtu yeyote nakuweka kundi moja na wapuuzi wengne ndio mana wao wote nawafananisha mana wote ni walamba mataco kwa watu wao
 
Karibuni tena chai Ikulu...
Wakitoka hapo na vibahasha vilivotumwa kwenye akaunti zao wanakuwa wapole wanasubiri mpaka ladha ya chai iishe mdomoni na pesa kuisha ndio waanze kupiga kelele tena.
 
Hospitali zetu unaweza kumfikisha wakakataa kumtibu mpaka awe na PF3


Kuna jamaa yetu alishavamiwa akachomwabna visu tumekimbia police haraka kupitia pf3 hapo tumepanic balaa akatoka askari ile tunamwambia tuandike haraka jamaa linajibu "huyo mbona bado mpya, hata hajapigwa sana, Kuna watu wanaletwa hapa wamechakaa" 😃
Maisha ya mbongo kweli yana thamani ndogo sana
 
Wakitoka hapo na vibahasha vilivotumwa kwenye akaunti zao wanakuwa wapole wanasubiri mpaka ladha ya chai iishe mdomoni na pesa kuisha ndio waanze kupiga kelele tena.
Wahuni tu kama wahuni wengine🚶‍♂️🚶‍♂️hii inji akili kumkichwa
 
Back
Top Bottom