Ukiangalia hapo Marekani ni #3 yeye pekee amenunua na kuuziana miizigo mingi
Na ukiangalia kwa karibu utaona hizo takwimu zinaongea kwa sauti kwamba Uchina inaitegemea zaidi Marekani kwa soko kuliko Marekani inavyoitegemea Uchina.
Kwa mfano unaposema ASEAN yaani The Associatioi of Southeast Asian Nations unamaanisha ni nchi kumi kwa Pamoja na hizo nchi zina uchumi mkubwa kuliko nchi nyingi za Afrika. ASEAN ina nchi kama Brunei, Cambodia, Indonesia, Laos, Malaysia, Myanmar, Philippines, Singapore, Thailand, na Vietnam. Yaani hizi nchi kwa ujumla wake ndiyo zimempiku Marekani kwa kufanya biashara na China.
Kundi la pili ni Umoja wa ulaya, ambalo lina nchi zifuatazo; Austria, Ubeligiji, Bulgaria, Croatia, Jamhuri ya Cyprus, Jamhuri ya Czech, Denmark, Estonia, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Hungary, Ireland, Italia, Latvia, Lithuania, Luxembourg, Malta, Uhalanzi, Poland, Ureno, Romania, Slovakia, Slovenia, HIspania na Sweden.
Ukiziangalia nchi hizo za ulaya na ukubwa wa chumi zake, lakini zote kwa umoja wao ndiyo zimeifanya Marekani iwe ya Tatu, Sasa kumbe kwa maana nyingine hizo nchi moja moja haziwezi kufikia kiwango cha Biashara ambacho Marekani inafanya na China.