Kleptomaniacs
Member
- Apr 23, 2008
- 86
- 2
Mh! Watanzania tulivyokuwa mbumbu! eti tunafikria kila ardhi inayoonekana inafaa ama matumizi yake ni kilimo tu! yaani wewe ukipanda ndege unachokiona ni ardhi tupu! ebu acheni wendawazimu wenu! ardhi Tanzania ipo katika makundi makubwa matatu, ya vijiji, hifadhi na jumla. Ardhi pekee ambayo mwekezaji anaweza pata bila kuleta athari kubwa sana ni ardhi ya Jumla ambayo ni asilimia 2 ya ardhi iliyopo iliyobaki yote ni ama ardhi ya kijiji ama ya hifadhi. Ardhi ya kijiji jumla yake ni karibia asilimia 70 na kitu, ilyobakia yote ni hifadhi. Sasa sio kila pori ni ardhi ya kilimo! halafu wengine mnaongea as if hii nchi ni ya wakulima tu! mnasahau kuwa Tanzania tuna wafugaji nao wana mchango wao mkubwa katika uchumi pamoja na mateso na manyanyaso wanayopewa!
Haihitaji mtu kusoma shahada ya uchumi kuelewa kwamba kwa vyovyote vile ujio wa hawa Wasaudia hauwezi kuleta tija kwa nchi katika msitakabali tuliokuwa nao, kama wanataka kuwakomboa kweli wananchi wakulima masikini, wakiwezeshwa na serikali wanaweza kuzalisha kwa makubaliano na kwa kuwa soko litakuwepo hiyo ni motisha tosha kwa mkulima kufanya kazi na hata ikibidi kuzitafuta fedha za kuzalishia! acheni bla blah zenu ni midhaha itakayotufikisha pabaya! mnatuletea mambo ya akina Mangungo haki ya nani hapatakalika hapa. Mambo mangapi tumewaaminia hawakuweza kuyafanya?
Jambo la pili la kuangalia ni kuwa macho na huyu mkwere!simwamini kabisa huyu anaweza kutwaa na kuwapa wasaudia ardhi ya wanavijiji eti tu kwasababu sheria zenyewe zimekaa vibaya hasa pale linapokuja suala la kulinda haki za ardhi, hatuna security of tenure hata Waziri alisema tuna haki ya matumizi tu!maana yake nini? HATUNA HAKI YA UMILKI! kwahiyo Rais kupitia uwezo wake wa milki ya hatima(Radical title) anaweza kutwaa na kufanya lolote alitakalo! sasa wengi wetu kwa kuwa hata hatujui juu ya hilo huwa tunajikuta tunatupwa nje ya maeneo yetu na kuambulia fidia.
Haya KIGAMBONI si yamewakuta! kama kungekuwa na nia ya kweli kumkomboa mwananchi kungefanyika partnership nikiwa na eneo langu waje tukubaliane na mie nakuwa na share na mtaji wangu ni ardhi, hapo tungeelewana kuhusu hizo faida sio huu ujanja ujanja wa kufanywa manamba na mijitu inashangilia hili!