Saudi investors eye Tanzanian farmland

Saudi investors eye Tanzanian farmland

kunamahala hapa kunamtu aliongelea swala la kuandika barua ya wazi kwa raisi kumpa maoni yetu juu ya swala la ardhi na sisi ambao hatufurahishwi na utoaji wa ardhi yetu kama paremende tusaini. Tafadhali wale ambao mnauzoefu wa ardhi na uelewa wa jinsi ardhi yetu inavyogawiwa bila mpango, andikeni kawalaka halafu mtume tuandike majina yetu kusopoti.

Nadhani nimuhimu kumuandikia raisi, tumepata taarifa kwamba serikali imekuwa ikigawa ardhi kwa wageni kwa muda mrefu sasa. Tuorozesha hizo zilizogawiwa na hasara zake, halafu tumwambie pia kunataarifa za saudi kwamba watapewa ardhi na sisi tunapinga uamuzi huu kwa sababu... , na tunapendekeza kama ardhi zikitolewa zifuate masharti fulani...

wako watiifu watanzania,

1.
2
 
Petu Hapa,
Nahisi we may be a bit late. Kumbuka wafanyi biashara wa Saudi walikuja Tz na kuomba ardhi. Mheshimiwa na delegation yake wakafunga safari hadi Saudia na kututangazia mpango huo. Kuna uwezekano sahihi zimeshaanguka wakati wa ziara hii ya Saudia.
 
Jasusi,
Mkuu bado mimi napenda sana kuelewa.. Hili swala la ardhi linawakuna vichwa na roho zenu kwa sababu ya Saudia?..
Iweje kuna mataifa kibao ambao tayari wana ardhi tena kwa lease ya miaka 99 isiwe issue ya kumwandikia barua rais isipokuwa hili la Saudia na maswala ya kuchelewa!. Mtaonekana wajinga na wenye fikra za Udini..ndicho nachokiona mimi hapa JF mtanisamehe lakini.
Mtakuwa hamna tofauti na yule waziri Masha alipopeleka malalamishi kuhusiana na vitambulisho..Kwa nini tulifikiria ana mkono ndani yake ni kwa sababu alitetea shirika moja tu.. Na kwa upande huu wa hoja hii itaonyesha mnapinga sio sheria za ardhi isipokuwa wawekezaji wa Saudia kupewa ardhi..
Let me be open on this, Inachusha sana kuona nchi yetu inauzwa wakati raia yaani wananchi wenyewe hawana madaraka na ardhi hiyo..
Tunapewa kibali cha milki ya ardhi lakini wanapokuja wageni tunanyang'anywa ardhi kwa madai kwamba hawa ni wawekezaji pia ardhi ni mali ya serikali..at the same time kuna kimtego cvha kisheria kinachodai kuwa serikali ni watu (wananchi).. hii inanipa taabu sana kuelewa urithi huu wa Uhuru wetu.
Sasa kabla nchi yetu haijafikia mahala pabaya, kabla hatujapoteza kabisa maana ya uhuru wetu ambao ulitokana na kupigania umiliki ya ardhi,. bila shaka ni wakati Muafaka wananchi wakapewa ardhi yao. Ni wakati kila Mtanzania apewe kipande chake na mwenyewe ataamua kukiuza ama kupangisha.. kwa sababu ikiwa leo tunashindwa kuelewana na nchi majirani Kenya na Uganda kwa sababu ya Ardhi..basi ni muhimu kwetu kuelewa sisi tumechelewa wapi?..Kwa nini Kenya na Uganda wako radhi ku share vitu vingi ambavyo sisi tunaogopa hadi leo kuweka mguu wetu!.. Ni kwa sababu sheria zetu za miliki ya ardhi bado ni ule wa Kikomunist.. Mwananchi hana milki ya ardhi isipokuwa amekodishiwa na serikali ambayo kimaandishi unaambiwa ni wananchi hao hao..Na mwananchi, ardhi yake inayotambulika ni kaburini (Mwitunga) ndipo anaweza kujenga himaya yake ya kudumu.
Hii haijakaa sawa kabisa!
 
Petu Hapa,
Nahisi we may be a bit late. Kumbuka wafanyi biashara wa Saudi walikuja Tz na kuomba ardhi. Mheshimiwa na delegation yake wakafunga safari hadi Saudia na kututangazia mpango huo. Kuna uwezekano sahihi zimeshaanguka wakati wa ziara hii ya Saudia.

Tufanye uchunguzi tuelewe kinachoendelea, hataka kama tumechelewa bado tunaeza kuinfluence. Always there is a loophole for change!
 
Jasusi,
Mkuu bado mimi napenda sana kuelewa.. Hili swala la ardhi linawakuna vichwa na roho zenu kwa sababu ya Saudia?..
Iweje kuna mataifa kibao ambao tayari wana ardhi tena kwa lease ya miaka 99 isiwe issue ya kumwandikia barua rais isipokuwa hili la Saudia na maswala ya kuchelewa!. Mtaonekana wajinga na wenye fikra za Udini..ndicho nachokiona mimi hapa JF mtanisamehe lakini.
Mtakuwa hamna tofauti na yule waziri Masha alipopeleka malalamishi kuhusiana na vitambulisho..Kwa nini tulifikiria ana mkono ndani yake ni kwa sababu alitetea shirika moja tu.. Na kwa upande huu wa hoja hii itaonyesha mnapinga sio sheria za ardhi isipokuwa wawekezaji wa Saudia kupewa ardhi..
Let me be open on this, Inachusha sana kuona nchi yetu inauzwa wakati raia yaani wananchi wenyewe hawana madaraka na ardhi hiyo..
Tunapewa kibali cha milki ya ardhi lakini wanapokuja wageni tunanyang'anywa ardhi kwa madai kwamba hawa ni wawekezaji pia ardhi ni mali ya serikali..at the same time kuna kimtego cvha kisheria kinachodai kuwa serikali ni watu (wananchi).. hii inanipa taabu sana kuelewa urithi huu wa Uhuru wetu.
Sasa kabla nchi yetu haijafikia mahala pabaya, kabla hatujapoteza kabisa maana ya uhuru wetu ambao ulitokana na kupigania umiliki ya ardhi,. bila shaka ni wakati Muafaka wananchi wakapewa ardhi yao. Ni wakati kila Mtanzania apewe kipande chake na mwenyewe ataamua kukiuza ama kupangisha.. kwa sababu ikiwa leo tunashindwa kuelewana na nchi majirani Kenya na Uganda kwa sababu ya Ardhi..basi ni muhimu kwetu kuelewa sisi tumechelewa wapi?..Kwa nini Kenya na Uganda wako radhi ku share vitu vingi ambavyo sisi tunaogopa hadi leo kuweka mguu wetu!.. Ni kwa sababu sheria zetu za Umiliki wa ardhi bado ni ule wa Kikomunist.. Mwananchi hana milki ya ardhi isipokuwa amekodishiwa, mwananchi ardhi yake inayotambulika ni kaburini (Mwitunga) ndipo anaweza kujenga himaya yake ya kudumu.
Hii haijakaa sawa kabisa!

Concern yako ni ya msingi sana lakini unanitia woga kaka! Ni kweli kwamba ardhi imekuwa ikitolewa kama peremende nchi kwetu. HakiArdhi kwa uelewa wangu imekuwa iko mbele sana kuonyesha matatizo yaliyopo kwenye ardhi lakini wananchi walikuwa hawaoni kama wanayagusa. Mimi mwenyewe nimeshapiga kelele nyingi tu katika wizi wa ardhi! Lakini mtu aliyekuwa anasikia ila waibaji ndio waliokuja na vishindo! Pia kunabaadhi wananchi waliamka na kukataa kuwapa wawekezaji ardhi yao.

Sasa, tunapotoa wazo la watu kuandika wakala sio kwamba tunasema swala la ardhi limeanza leo, ama tunaubaguzi wa kidini au rangi. Si kwamba hatuelewi ardhi yetu ya arusha, ukanda wa ziwa, hifadhi zipo mikononi mwa wageni ambao wengi wao ni wazungu, tunalitambua hilo, na juhudi nyingi zimefanyika kuhamasisha mijadala hiyo bila mafanikio.

Leo hii swala la saudi, limewashitusha watu, watu wanaonekana kuguswa, ni hapo tunaposema tutumie nafasi hii kumweleza Raisi kwamba, nguvu zake za kugawa ardhi kihistoria zimezidi mipaka. Nimetoa rai kwa watu wanaojua migogoro ya ardhi watuandikie hiyo barua, kwani kunamengi yanayotia uchungu katika umiliki wa ardhi.

Sasa, kama nuru imekuja utasema tuache giza tu kwa sababu tumezoea? Mabadiliko yanakuja pale jamii inapopatwa na mguso, na hili la wasaudi limewakuna watu kwanini hilo ni swala jingine, lakini mkuno huo unatoa nafasi kwa wapambanaji wa ardhi kuweka kifua mbele na kuanza mapambano juu ya ardhi!
 
Saudis request for 500,000 hectares

By The Citizen Reporters and Agencies

Saudi Arabian investors want to lease 500,000 hectares of farmland in Tanzania to grow rice and wheat.

The Saudis made the request during President Jakaya Kikwete?s visit to the Kingdom that ended yesterday. Senior officials from the Saudi capital's chamber of commerce came up with the request on the sidelines of a meeting with the Head of State.

President Kikwete is reported to have told the Saudis that Tanzania could lease them plots that covered up to 10,000 hectares each for 99 years.
"Tanzania is ready to do business with you ... There is 100 million acres (40.5 million hectares) of good arable land," Reuters quoted Mr Kikwete as telling the Saudi businessmen.

The Citizen yesterday spoke to several prominent individuals, who welcomed the development but called for a systematic approach, saying the country?s interests should come first.

Senior economist Ibrahim Lipumba said promoting agriculture was important, but added that such investments required concrete policy direction. Mr Lipumba is also chairman of the opposition Civic United Front.

The president of the Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA), Mr Aloys Mwamanga, called it "good business", provided collateral benefits for the country were taken into account.

Tanzania Investment Centre (TIC) executive director Emmanuel ole Naiko said such an investment would create many jobs for locals, adding that he expected the Head of State to refer the Saudi investors to TIC.

"We already have policies on contract farming and outgrowing. We have the Land Act of 1999. All these will be adhered to. It's a fact that we have abundant land and there are already institutions renting land to local investors to farm for a specified period of time," Mr ole Naiko noted in a telephone interview from abroad.
Reuters reported yesterday that Saudi businessmen and officials would visit Tanzania in the next few weeks to follow up the matter. The Saudis are interested in leasing the equivalent of about 0.5 per cent of Tanzania's land surface because of the country's geographic proximity, political stability and availability of water resources and farmland.

"He (President Kikwete) told us that Tanzanian authorities can lease us plots each of which covers up to 10,000 hectares for a 99-year period," Mr Samir Ali Kabbani, head of the chamber's agriculture committee, told Reuters.

"They can lease the land from the Government," Mr January Makamba, an aide to President Kikwete, also told Reuters.

The Saudis are not alone in this since in the face of food shortages and with demand for biofuels growing, an increasing number of wealthy nations are buying up land in developing countries, particularly in Africa, to ensure a steady supply of crops.

High-ranking officials from many of these nations have been on the road since March 2008 in a diplomatic treasure hunt for fertile farmland in places like Uganda, Brazil, Cambodia, Sudan and Pakistan.

The idea, which has been called a "new scramble for Africa", is not without its critics, who question why Africa should lose valuable farmland when it is chronically short of its own food.

Kenya, Sudan, Ethiopia and now Madagascar have all recently offered vast tracts of farmland for lease, hoping to cash in on a growing trend whereby developing countries from Ukraine to Cambodia offer fertile land to the highest bidder.

Qatar plans to lease 40,000 hectares along Kenya's coast to grow fruit and vegetables for its own citizens in return for building a ?2.4 billion (Sh3 trillion) port close to the Indian Ocean tourist island of Lamu. The plan has, however, met with stiff opposition from activists.

Prof Lipumba said there was nothing wrong with leasing land to foreigners in a country where less than 10 per cent of arable land is under cultivation, but added that such investments should come through TIC, and not private requests to the President. He said he expected the Saudis to create jobs for locals and bring into the country modern farming methods.

"The issue of promoting agriculture is primary. What we currently need is a transparent policy on foreign direct investment in the sector. The policy should lay down conditions that protect national interests," Prof Lipumba added.

Mr ole Naiko said the Saudis had already shown interest in farming in Tanzania, but the latest development could lead to the biggest land-leasing agreement with foreign investors. He said such a project would be beneficial, but cautioned that the sensitivity of land matters in the country needed to be keenly considered.

"A contingent of large-scale farmers from Saudi Arabia visited us about two months ago, and made a request to lease land, but we told them to wait for results of the feasibility study of the project. We are still trying to find out whether there are people willing to lease out land or not," he noted.

Two contradicting statements from the executives and the legislaters. Hivi vitu vinafanywa kwa makusudi au kwakutoelewa? Kama contract farming ipo then why leasing? Am I confused or dont understand the concepts of contract farming, leasing and renting? Then after the agreement they would say mkataba mbovu. Lets not play over the resources of our country if we are ignorant then let us first get knowledge of how to go about things.

Naona kuna ka mtego hapo that contract farming between the state and the provided through leasing. Sasa angalia sheria inasemaje kwenye payment per ha through lease uone kama si kugawa hiyo ardhi bure.
 
Last edited:
Filister,
Safi sana mkuu wangu kusema kweli hii inatisha sana.. Mimi naomba sana wanasiasa wanambie nini maana UHURU! kwa nini tulitafuta Uhuru wetu ikiwa wakati tunatawaliwa na Mkoloni tulikuwa na ajira vile vile..Tena basi mkoloni aliweza kuwasaidia wananchi wakulima madogo wadogo kupata mbegu na dawa za mimea bila kushukua ardhi zao.
Iweje leo nchi yetu iwe leased ktk hali ambayo haitofautiani kabisa na milki ya ardhi ambayo tulitawaliwa. Muingereza hakuwa mtawala wa Kudumu, ilijulikana wazi tulikuwa ktk Protectorate, lakini bado tulitafuta UHURU wetu kwa siasa za wananchi wote kuwa HURU..
Ikiwa swala lilikuwa Kushika IKULU kubadilisha kichwa toka mzungu na kuwa mwafrika mbona wananchi wengi tungependa mzungu kuongoza nchi..Na sababu kubwa ingekuwa uwezo wetu mdogo ktk Utawala!..
 
Mada hii inanifanya nijiuliza swali moja: Kwanini Watz wanapenda sana "kubanana" katika maeneo finyu na kuacha mapori ya ekari na ekari yakiwa matupu hayajakaliwa na mtu? Hii siyo kwa watu binafsi tu bali hata Serikali utaona inapofanya mipango inayohitaji ardhi bado wataendelea kubananisha maeneo ambayo tayari ni congested.Badala ya kuona mapori hayo ni muafaka kuwapatia wageni kama hao waarabu wa Saudia basi wangehakikisha maeneo yenye ardhi nzuri ya kutosha yanawekewa angalau barabara na basic infrastructure ili wananchi waweze kuishi na kufanya shughuli zao kwa nafasi.Nadhani ni kwa vile maeneo yamekaa kama mapori bila watu ndiyo maana huo mwanya wa kuwapa/kuwakodishia wageni unajitokeza, na tukiendelea kukatalia ardhi yetu inakuwa kama " a dog in a manger" - kitu hukitumii na hutaki mwenye kuweza kukitumia akitumie.
 
..binafsi nadhani tuwe na juhudi za makusudi kabisa za kuhakikisha wakulima wetu wanaongeza uzalishaji per unit area.

..juhudi hizohizo zielekezwe kuwawezesha wafugaji na wavuvi kuongeza thamani ya mazao yao.

..binafsi sioni umakini na juhudi za serikali ktk kushughulikia masuala hayo mawili niliyoeleza.

..vilevile vipi kuhusu wawekezaji wa ndani? kwanini hawa hawasaidiwi kuweza kulikamata soko la ndani?

..Tanzania kumejaa waagizaji na wachuuzi tu. kina TATA,DAEWOO,..wa Tanzania ni kina nani? we need our own indigenous industrial captains.

Jokakuu:

Kuna points mbili nataka kueleza. Kwanza ni kuhusu perspective ya wawekezaji wazawa. Mkandara ni mwalimu wangu mkuu hapa hivyo nitatumia mifano yake. Wakati tupo BCstimes forum alisema kuwa, watanzania wengi wazawa wana asili ya uvuvi, ukulima au ufugaji wa kujikimu. Huu ndio mwanzo wetu. Na kwenye hii thread amesema kuwa mara nyingi tukijua kuendesha baiskeli basi tunafikiri tunaweza kuendesha gari tena la abiria.

Now kuhusu TATA na DAEWOO, watanzania wanaweza kufanya lakini groundworks ni lazima ziwepo. Biashara ni shrewd activity, kuna watanzania wanaoweza kuwa exceptional na kufanya biashara bila kuwa na exposure yoyote hile. Lakini hao ni wachache sana. Wengi wetu ni lazima tuwe na exposure au urithi wa biashara unaotokana na juhudi ya vizazi vilivyopita. TATA wana zaidi ya miaka 200 katika biashara. Familia ya TATA asili yao ni Iran na walikuwa wajenzi wa meli za kivita zaidi ya miaka 200 iliyopita na walipewa tender ya kujenga meli za kivita za jeshi la uingereza. Na biashara wanazofanya sasa ni diversification ya miaka 200.

Point ya pili ni sisi kuwa Wachuuzi na waagizaji. Nakubaliana kwa 100% ya mtazamo wako. Hili linatokana na mind-set zetu. Wachuuzi na waagizaji mara nyingi wana mind ya short term investments. Kwa mfano ukiwa mkulima wa mahindi ni lazima ufanye kazi ya miezi sita bila kupata return yoyote. Sidhani kama kuna vijana wengi wanaoweza kujaribu biashara ya kulima mahindi.

Kubadilisha mind-set ya watu sio kazi ndogo lakini inaweza kufanyika.
 
Mada hii inanifanya nijiuliza swali moja: Kwanini Watz wanapenda sana "kubanana" katika maeneo finyu na kuacha mapori ya ekari na ekari yakiwa matupu hayajakaliwa na mtu? Hii siyo kwa watu binafsi tu bali hata Serikali utaona inapofanya mipango inayohitaji ardhi bado wataendelea kubananisha maeneo ambayo tayari ni congested.Badala ya kuona mapori hayo ni muafaka kuwapatia wageni kama hao waarabu wa Saudia basi wangehakikisha maeneo yenye ardhi nzuri ya kutosha yanawekewa angalau barabara na basic infrastructure ili wananchi waweze kuishi na kufanya shughuli zao kwa nafasi.Nadhani ni kwa vile maeneo yamekaa kama mapori bila watu ndiyo maana huo mwanya wa kuwapa/kuwakodishia wageni unajitokeza, na tukiendelea kukatalia ardhi yetu inakuwa kama " a dog in a manger" - kitu hukitumii na hutaki mwenye kuweza kukitumia akitumie.

WoS:

Hiyo avatar yako inatuogopesa maana imekaa queenly. Anyway, ngoja nirudi kwenye mada.😀.

Siku zote sisi tuliopata bahati ya kusoma au kuwa na kazi hatuelewi kwanini watu wasirudi vijijini au kwenye mapori na kulima. Na mara nyingine tunatoa lawama kwa serikali zetu.

Uchambuzi wangu wa kwanza ni kuwa kilimo cha mkono ni kilimo cha kujikimu tu. Kwa miaka mingi theme ya maendeleo ya vijijini imekuwa around matumizi ya jembe la mkono. Hata kwa simple mathematics model, bado output ya jembe la mkono ni ndogo.

Vilevile kilimo tunachozungumzia hapa kina risks nyingi sana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Instintively waTanzania wengi wenye vijisenti hawataki ku-invest kwenye kilimo kwa sababu ya risks za ukame au mafuriko. Na hakuna sera za risks management. Kuna mzee ninamfahamu baada kustaafu alitumia mafao yake yote kufungua mashamba, lakini ukame ulipopita hakupata hata gunia moja la mahindi. Angekuwa ni mkulima wa Marekani basi angetegemea ruzuku ya serikali ambayo ingeweza kumsaidia katika msimu unaofuatia. Sisi hivi yupo mjini anaganga njaa.

Kwa maoni yangu maisha ya kubanana yanasaidia ku-mitigate risks nyingi katika uchumi wetu wa kijikimu.
 
Hapa Petu,
Sasa, kama nuru imekuja utasema tuache giza tu kwa sababu tumezoea? Mabadiliko yanakuja pale jamii inapopatwa na mguso, na hili la wasaudi limewakuna watu kwanini hilo ni swala jingine, lakini mkuno huo unatoa nafasi kwa wapambanaji wa ardhi kuweka kifua mbele na kuanza mapambano juu ya ardhi
Mkuu nuru ilitokea toka miaka 10 iliyopita, toka utawala wa Mkapa swala hili la kuuza nchi lilizungumziwa sana na hata kumfikia Mkapa mwenyewe na majibu yake yalikuwa wananchi maskini hamna fedha!..
Matatizo ya Makaburu na Mugabe hayakuanza jana yameanza toka mwaka 2001 na hata hayo mashamba ya wazungu (wageni) nchini hayakuanza jana..Yapo hivi tunavyozungumza na vibali wanavyo mkononi.

Tatizo langu kubwa ni kwamba wananchi walikubali uwekezaji wa hawa wazungu na wakamilikishwa ardhi kwa miaka 99.. Na sheria yetu ktk milki ya ardhi inatoa miaka hiyo kwetu sote raia na wageni hivyo nashindwa sana kuelewa mnaposema nuru hii imekuja tu baada ya saudia kupewa Offer ya ardhi wakati wapo wageni tayari wanamiliki ardhi hizo na hamsemi kitu..
Ukiniuelewa hapo ndipo napokuja na hoja kwamba tunapotaka kuzungumzia swala la Ardhi tusitaje nchi (Saudia).. ni swala la wageni wote, sheria zirekebishwe kulingana na uzito wa swala la milkli ya ardhi in general na sio Saudia kuwa kiamsho!..Mwenzako nilisha amka long time na niliuona mwanga siku nyingi nikapigwa vita sana humu JF nikaitwa mjamaa, mbaguzi na sipendi maendeleo mfano wa Mugabe mwenyewe, wengine wakasema namchukia Mkapa kwa sababu ni Mkristu, sasa naposoma hoja hizi hapa na kupima yale yaliyonikuta nyuma naona huu sii mwanga tena isipokuwa in coming headlights zinazo niumiza macho..
Mkuu sasa hivi kuna maeneo ambayo mwananchi hutakiwi kukanyaga - Private Property wenyewe wanasema!..kumbuka Coco beach ilikuwa imekwenda hiyo!..Kuna Beaches huko Zanzibar huruhusiwi kukanyaga ni maeneo yaliyokuwa leased kwa wazungu..sasa inakuwaje kichwa cha habari hii iwe wawekezaji wa Saudia ambao hata hiyo ardhi hawajakabidhiwa?
 
Leo hii swala la saudi, limewashitusha watu, watu wanaonekana kuguswa, ni hapo tunaposema tutumie nafasi hii kumweleza Raisi kwamba, nguvu zake za kugawa ardhi kihistoria zimezidi mipaka. Nimetoa rai kwa watu wanaojua migogoro ya ardhi watuandikie hiyo barua, kwani kunamengi yanayotia uchungu katika umiliki wa ardhi.

Tukumbuke the Presidential Commission of Inquiry into Land Matters whose chairman was Prof Issa Shivji, huyu mzee anajua vizuri sheria na historia ya matatizo ya Ardhi Tanzania.

Shivji who is a founder of Haki Ardhi Institute Haki Ardhi - Home ameandika kitabu kuhusu land reform

Title: Not yet democracy: reforming land tenure in Tanzania.
Personal Authors: Shivji, I. G.
Author Affiliation: Faculty of Law, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania.
Editors: No editors
Document Title: Not yet democracy: reforming land tenure in Tanzania.

Abstract:

The problems of land tenure reform in Tanzania are addressed. It is noted that in 1991, the Tanzanian government formed a Commission of Inquiry into Land Matters (CILM) and published a report in 1992. The work of the Commission is placed within its broader context, setting its findings within the current democracy debate that is occurring all over Africa, including treatment of the proposed new Tanzania Land act. Ten chapters are divided into three parts. Problems of land tenure examines: the conceptual framework; problems of land tenure in the post-Arusha period I: nationalization and villagization; problems of land tenure in the post-Arusha period II: urbanization and liberalization; and towards a new land policy: preview of social forces. Democratisation of land tenure: recommendations of the Land Commission examines: land tenure policy and structure; and institutional and legal framework. Debating land: the making of the policy and the law examines: critiques of the report I: the radical title; critiques of the report II: gender and land; law, land and justice; and contradictory perspectives on reform through law.

Publisher: International Institute for Environment and Development (IIED)
 
Filister,
Safi sana mkuu wangu kusema kweli hii inatisha sana.. Mimi naomba sana wanasiasa wanambie nini maana UHURU! kwa nini tulitafuta Uhuru wetu ikiwa wakati tunatawaliwa na Mkoloni tulikuwa na ajira vile vile..Tena basi mkoloni aliweza kuwasaidia wananchi wakulima madogo wadogo kupata mbegu na dawa za mimea bila kushukua ardhi zao.
Iweje leo nchi yetu iwe leased ktk hali ambayo haitofautiani kabisa na milki ya ardhi ambayo tulitawaliwa. Muingereza hakuwa mtawala wa Kudumu, ilijulikana wazi tulikuwa ktk Protectorate, lakini bado tulitafuta UHURU wetu kwa siasa za wananchi wote kuwa HURU..
Ikiwa swala lilikuwa Kushika IKULU kubadilisha kichwa toka mzungu na kuwa mwafrika mbona wananchi wengi tungependa mzungu kuongoza nchi..Na sababu kubwa ingekuwa uwezo wetu mdogo ktk Utawala!..

That is a good question!
 
Hapa Petu,

Mkuu nuru ilitokea toka miaka 10 iliyopita, toka utawala wa Mkapa swala hili la kuuza nchi lilizungumziwa sana na hata kumfikia Mkapa mwenyewe na majibu yake yalikuwa wananchi maskini hamna fedha!..
Matatizo ya Makaburu na Mugabe hayakuanza jana yameanza toka mwaka 2001 na hata hayo mashamba ya wazungu (wageni) nchini hayakuanza jana..Yapo hivi tunavyozungumza na vibali wanavyo mkononi.

Tatizo langu kubwa ni kwamba wananchi walikubali uwekezaji wa hawa wazungu na wakamilikishwa ardhi kwa miaka 99.. Na sheria yetu ktk milki ya ardhi inatoa miaka hiyo kwetu sote raia na wageni hivyo nashindwa sana kuelewa mnaposema nuru hii imekuja tu baada ya saudia kupewa Offer ya ardhi wakati wapo wageni tayari wanamiliki ardhi hizo na hamsemi kitu..
Ukiniuelewa hapo ndipo napokuja na hoja kwamba tunapotaka kuzungumzia swala la Ardhi tusitaje nchi (Saudia).. ni swala la wageni wote, sheria zirekebishwe kulingana na uzito wa swala la milkli ya ardhi in general na sio Saudia kuwa kiamsho!..Mwenzako nilisha amka long time na niliuona mwanga siku nyingi nikapigwa vita sana humu JF nikaitwa mjamaa, mbaguzi na sipendi maendeleo mfano wa Mugabe mwenyewe, wengine wakasema namchukia Mkapa kwa sababu ni Mkristu, sasa naposoma hoja hizi hapa na kupima yale yaliyonikuta nyuma naona huu sii mwanga tena isipokuwa in coming headlights zinazo niumiza macho..
Mkuu sasa hivi kuna maeneo ambayo mwananchi hutakiwi kukanyaga - Private Property wenyewe wanasema!..kumbuka Coco beach ilikuwa imekwenda hiyo!..Kuna Beaches huko Zanzibar huruhusiwi kukanyaga ni maeneo yaliyokuwa leased kwa wazungu..sasa inakuwaje kichwa cha habari hii iwe wawekezaji wa Saudia ambao hata hiyo ardhi hawajakabidhiwa?

Wakati wanakupiga vita sikuwepo kaka! Ningekubeba.

Labda niseme naelewa mtizamo wako na kwamba kuchukua swala la saudi ni kuvunja basic principle. Nakubaliana na wewe kwamba swala la ardhi liongelewe kwa ujumla wake. Lakini vile vile, mabadiliko saa zingine kaka yanaanza hatua kwa hatua ambazo zimeshaanza toka siku nyingi sana. Ila pendekezo langu, pale inapotokea nafasi ya kukumbusha wananchi kinachoendelea tuendelee kuwakumbusha. Kama lugha ya sasa wanayoilewa ni saudi arabia tuanze na hiyo, wakati tunaendelea na mambo mengine. Si unajua hata cinema zinaanza na trela! Basi trela yetu ni mamba yaliyopo kwenye pipeline! Tunachohitaji ni wananchi kuanza kuangalia hiyo trela halafu picha kamili itawekwa.

Unajua haya ndio maswala yaliyotokea kwenye land movement baina ya Haki ardhi na Gender Land Task Force. Upande uliokuwa unaongozwa na hakiardhi, ulitaka mabadiliko ya katiba kulinda maslahi ya wanyonge kwa ujumla wake ili kupeleka nguvu za umiliki na maumizi kwa vijiji na kuyapunguza toka kwa raisi, wakati GLTF wao walitaka mwanamke awe na haki ya kumiliki na kutimia ardhi kwa jina lake. mwisho wa movement GLTF wameshinda. Nadhani inakaribia miaka 10 sasa toka ushindi huo umepatikana. HakiArdhi leo wanajiuliza je ule ushindi unawalinda vipi wanawake maskini, maana hata kama haki unayo na nguvu ya kuinunua ama kuilinda hauna haki inakuwa haina msingi. Lakini kwa upande wa GLTF wanasema haki ya kumiliki ni ushindi kwa wanawake na ndio ulikuwa ni mwanzo.

Mitizamo hiyo miwili ni tofauti lakini kwa namna moja ama nyingine ushirikiano wao katika landmovement ulileta mabadiliko katika sheria. Sasa kwa sasa tuendelea kusukuma hilo gurudumu kwa namna yoyote tutakayoweza.
 
Mada hii inanifanya nijiuliza swali moja: Kwanini Watz wanapenda sana "kubanana" katika maeneo finyu na kuacha mapori ya ekari na ekari yakiwa matupu hayajakaliwa na mtu? Hii siyo kwa watu binafsi tu bali hata Serikali utaona inapofanya mipango inayohitaji ardhi bado wataendelea kubananisha maeneo ambayo tayari ni congested.Badala ya kuona mapori hayo ni muafaka kuwapatia wageni kama hao waarabu wa Saudia basi wangehakikisha maeneo yenye ardhi nzuri ya kutosha yanawekewa angalau barabara na basic infrastructure ili wananchi waweze kuishi na kufanya shughuli zao kwa nafasi.Nadhani ni kwa vile maeneo yamekaa kama mapori bila watu ndiyo maana huo mwanya wa kuwapa/kuwakodishia wageni unajitokeza, na tukiendelea kukatalia ardhi yetu inakuwa kama " a dog in a manger" - kitu hukitumii na hutaki mwenye kuweza kukitumia akitumie.

From our national website, the facts of our land! Tanzania National Website

Tanzania has a surface area of 94.3 million ha. of which 22 million ha. (23%) is allocated to reserves ( largest share of land resources allocated by any country in Sub -Saharan Africa), which includes National Parks (4.2 million ha.), Game Reserves (7.7 million ha.), and Forest Reserves (10.1 million ha.). The gross area cultivated/planted annually is about 5.1 million ha., which is only about 5 per cent of surface area of Tanzania. The other arable land, but not cultivated, is 10 million ha. much of it is used as pasture. Within the reserves there is additional 4 million ha. suitable for cultivation.

However, in 2008, i remember listening to Executive director of HakiArdhi on "Uchumi Wetu" speaking about the misconception of availability of arable land. If we can get his fact here it could inform our discussion if we indeed have a lot of land in relation to our population growth and basic needs of our people.
 
Hapa Petu,
Mkuu nakuelewa sana na mimi nipo nawe ktk jitihada zote zinazoambatana na haki Ardhi kwani wengine hapa tumepoteza mashamba, miji na hata makaburi ya mababu zetu kwa sababu hatua sauti..Hata hivyo karibu JF tupo wengine ndio tumeshafunga ndoa JF ni mke wa Pili huyu..

Kama umenisoma vizuri huko nyuma, nimesema sana na kusisitiza kwamba mtazamo wa hoja hii usi base kwa saudia hata kama wao wako mbioni kupewa ardhi hii. Kufanya hivyo ni kupotosha haki ardhi badala yake kesi yetu inakuwa wananchi against Saudia investers hapo zinatazamwa mifano iliyopita na pengine kuhalalisha Saudia kupewa ardhi.

Nafahamu sana Wadanganyika tunavyofikiria, kumbuka pia swala la Dorwans, limekuja kwa kuizungumzia shirika moja na ndpo wanasiasa na baadhi wataalam wakatumia mashirika mengine yaliyopo nchini kama kigezo cha kununua mitambo ya Dowans - NDIVYO TULIVYO. Ukiuliza kwa nini Kikwete amefanya hivi utaambia mbona Mkapa pia alifanya hivi, Kwa nini Mkandara blaa blaa blaa! jibu litakuja sio kuhusu Mkandara bali hata Hapa Petu pia blaa blaa upo!..

Hii yote ni kutokana na sisi kushindwa kubeba sheria inayofungamana na kosa lililotendeka badala yake tunatazama nani mkosaji..yaani kubebana kupo hata uraiani. Tumeshindwa kuwawajibisha viongozi wetu ktk maswala amabyo yana utata mkubwa na pengine ndio uhai wetu kwa sababu tuna immani na wale tunaofanana nao ktk dini, rangi, makabila au mipaka ya ardhi.
Hivyo, msukumo wa hoja yangu umetokana na pale niliposikia - MBONA TUMECHELEWA!..ile mind set ya kutazama mtu mmoja (Saudia) wakati sheria inatakiwa kusimamiwa na kutekelezwa na watu wote wakati wowote na mahala popote..

Kama sheria ingekuwa wazi huyu Kikwete asingethubutu kuwaambia Waarabu kuhusiana na ukubwa wa ardhi yetu, as a fact maneno haya kayasema hata alipokuja US pale sokoni (Nasdaq) akiuza nchi. Na ukiuliza viongozi wote wa CCM watakwambia kazi yao ni moja tu -Tunauza nchi! sasa ukiuliza wanauza kitu gani bila shaka utasikia sifa za ardhi yetu kuwa na rutuba, madini na rasilimali nyingi ambazo zinaambatana na masharti madogo sana..Hawatafuti mtaji kwa ajili ya wananchi wao, hawatafuti business partner wanaoweza kushirikiana ktk uzalishaji wa mali nchini mwetu bali wanauza Nchi!

Huu sio Ubepari hata kidogo ila ni Utumwa wa fikra..Huwezi kumyima haki hiyo mwananchi wako ukampa mgeni kisha ukajenga hoja kwamba nchi yako inafuata mfumo wa Ubepari..Ikiwa asilimia 80 ya wananchi wako hawana ardhi yao isipokuwa kwa kukodisha, kisha wananchi hawa hawa hawawezi kupewa mikopo au njia zozote za kukuza mitaji yao ktk uwekezaji huwezi ku apply Ubepari kama mfumo wa ujenzi wa maendeleo ya nchi yako kwa kutegemea wageni ndio wenye fursa na nafasi ya urithi huo....Hizi ndizo alama kubwa za Ukoloni mamboleo!..
 
I can never be different from you. However, i am calling for multiple strategies. As other stake holders are demanding for land rights focusing on changing laws and educating citizens on land rights, other's should focus on mobilizing citizens to engage on public debate on land question.

The question is can we still write a public letter to the president! We could make sure the context provide holistic picture and demand for general change of power relations over land? Since you are engaged with people or HakiArdhi could you ask them to draft it with right context and send it here to the forum. We could read to make sure the context is right, and then send a letter to the responsible authorities. i think it is very important to write and re-write out position, even if that is required to do it everyday! Even if there are other initiative going on, but a simple statement can easily be red by majority.
 
Hapa Petu,
Mkuu nakuelewa sana na mimi nipo nawe ktk jitihada zote zinazoambatana na haki Ardhi kwani wengine hapa tumepoteza mashamba, miji na hata makaburi ya mababu zetu kwa sababu hatua sauti..Hata hivyo karibu JF tupo wengine ndio tumeshafunga ndoa JF ni mke wa Pili huyu..

Kama umenisoma vizuri huko nyuma, nimesema sana na kusisitiza kwamba mtazamo wa hoja hii usi base kwa saudia hata kama wao wako mbioni kupewa ardhi hii. Kufanya hivyo ni kupotosha haki ardhi badala yake kesi yetu inakuwa wananchi against Saudia investers hapo zinatazamwa mifano iliyopita na pengine kuhalalisha Saudia kupewa ardhi.

Nafahamu sana Wadanganyika tunavyofikiria, kumbuka pia swala la Dorwans, limekuja kwa kuizungumzia shirika moja na ndpo wanasiasa na baadhi wataalam wakatumia mashirika mengine yaliyopo nchini kama kigezo cha kununua mitambo ya Dowans - NDIVYO TULIVYO. Ukiuliza kwa nini Kikwete amefanya hivi utaambia mbona Mkapa pia alifanya hivi, Kwa nini Mkandara blaa blaa blaa! jibu litakuja sio kuhusu Mkandara bali Hapa Kwetu pia blaa blaa zipo!..Hii yote ni kutokana na sisi kushindwa kubeba sheria inayofungamana na kosa lililotendeka badala yake tunatazama nani mkosaji..yaani kubebana kupo hata uraiani. Tumeshindwa kuwawajibisha viongozi wetu ktk maswala amabyo yana utata mkubwa na pengine ndio uhai wetu kwa sababu tuna immani na wale tunaofanana nao ktk dini, rangi, makabila au mipaka ya ardhi.
Hivyo, msukumo wa hoja yangu umetokana na pale niliposikia - MBONA TUMECHELEWA!..ile mind set ya kutazama mtu mmoja (Saudia) wakati sheria inatakiwa kusimamiwa na kutekelezwa na watu wote wakati wowote na mahala popote..
Kama sheria ingekuwa wazi huyu Kikwete asingethubutu kuwaambia Waarabu kuhusiana na ukubwa wa ardhi yetu, as a fact maneno haya kayasema hata alipokuja US pale sokoni (Nasdaq) akiuza nchi. Na ukiuliza viongozi wote wa CCM watakwambia kazi yao ni moja tu -Tunauza nchi! sasa ukiuliza wanauza kitu gani bila shaka utasikia sifa za ardhi yetu kuwa na rutuba, madini na rasilimali nyingi ambazo zinaambatana na masharti madogo sana..Hawatafuti mtaji kwa ajili ya wananchi wao, hawatafuti business partner wanaoweza kushirikiana ktk uzalishaji wa mali nchini mwetu bali wanauza Nchi!
Huu sio Ubepari hata kidogo ila ni Utumwa wa fikra..Huwezi kumyima haki hiyo mwananchi wako ukampa mgeni kisha ukajenga hoja kwamba nchi yako inafuata mfumo wa Ubepari..Ikiwa asilimia 80 ya wananchi wako hawana ardhi yao isipokuwa kwa kukodisha, kisha wananchi hawa hawa hawawezi kupewa mikopo au njia zozote za kukuza mitaji yao ktk uwekezaji huwezi ku apply Ubepari kama mfumo wa ujenzi wa maendeleo ya nchi yako kwa kutegemea wageni ndio wenye fursa na nafasi ya urithi huo....Hizi ndizo alama kubwa za Ukoloni mamboleo!..

Mkandara:

Nilikuwa nasoma maandishi fulani ya wajerumani na sera zao kuja kutawala Tanganyika.

Wanasema kuwa Ardhi ni kubwa kiasi cha settlers waKijerumani kuweza kufungua mashamba bila kunyang'anya wazawa ardhi zao.

Concept ya sisi kuwa na ardhi kubwa imeanza zamani. Lakini population yetu imeongezeka sana na ardhi imebaki palepale.

Kitu kingine kinacholeta migogoro ni kuwa kwa kisiasa matumizi ya ardhi yametumika Tanzania kama unemployment Benefit.

katika nchi zingine, ukiwa huna ajira utalalamika serikalini. Lakini Tanzania ukiwa huna kazi, utaambia katafuta shamba au bustani ulime.

Labda tukubali tu kuwa kilimo sio profession ya kila mtu kufanya. Tuwaachie wachache ambao wanaweza large scale farming na sisi wengine tutafute kazi zingine za kufanya.
 
I can never be different from you. However, i am calling for multiple strategies. As other stake holders are demanding for land rights focusing on changing laws and educating citizens on land rights, other's should focus on mobilizing citizens to engage on public debate on land question.

The question is can we still write a public letter to the president! We could make sure the context provide holistic picture and demand for general change of power relations over land? Since you are engaged with people or HakiArdhi could you ask them to draft it with right context and send it here to the forum. We could read to make sure the context is right, and then send a letter to the responsible authorities. i think it is very important to write and re-write out position, even if that is required to do it everyday! Even if there are other initiative going on, but a simple statement can easily be red by majority.
Swahiba zangu bado tu mnajadili hii kitu. Acheni Bwana. Twendeni katika EPA. This is not an issue. LAND Inakuumeni sana. Sasa na sisi ndio maana tunasema mafuta yakitoka katika Land ya Watu wale - ni yao. Msiwadahil.
 
Kitu cha kwanza kabisa kumwambia January Makamba ni kwamba aache kuropoka. yeye kama mtu aliyesoma "Conflict Resolution" anajua sana kuhusu the egos of nations na kauli yake kuhusu "tusije kuwa kama Nigeria wenye mafuta lakini misururu ya mafuta haiishi" ilikuwa at best unfortunate, kwa sababu kwanza ina imply kwamba hatuko hivyo, which is not the case (ignorant and or uninformed) pili it is unnecessarily explosive.

Huwezi kufanya kitu cha maana na watu wa caliber hii ya January Makamba na muungwana wakituwakilisha.

Kwa Tanzania, hilo swala la possible diplomatic tension hapo ni non-issue. Hicho cha mtoto. Nakwambia Bernard Membe alisema hadharani kwamba Tanzania tusikatae misaada ya "shetani," ya Iran. Wakauchuna Wairan, maskini, walijua hawa watu ni vilaza wakutupwa, wasiojua walisemalo. Hillary Clinton angethubutu kutamka kitu kama hicho Wairan wasingemuacha.

January Makamba, presidential aid wa Tanzania anaenda Saudi Arabia kupiga madongo economic decision making za Nigeria, wakati sisi tumechoka kuliko Nigeria. Kuna watu loose canons humu duniani sijapata ona.
 
Back
Top Bottom