Hapa Petu,
Mkuu nakuelewa sana na mimi nipo nawe ktk jitihada zote zinazoambatana na haki Ardhi kwani wengine hapa tumepoteza mashamba, miji na hata makaburi ya mababu zetu kwa sababu hatua sauti..Hata hivyo karibu JF tupo wengine ndio tumeshafunga ndoa JF ni mke wa Pili huyu..
Kama umenisoma vizuri huko nyuma, nimesema sana na kusisitiza kwamba mtazamo wa hoja hii usi base kwa saudia hata kama wao wako mbioni kupewa ardhi hii. Kufanya hivyo ni kupotosha haki ardhi badala yake kesi yetu inakuwa wananchi against Saudia investers hapo zinatazamwa mifano iliyopita na pengine kuhalalisha Saudia kupewa ardhi.
Nafahamu sana Wadanganyika tunavyofikiria, kumbuka pia swala la Dorwans, limekuja kwa kuizungumzia shirika moja na ndpo wanasiasa na baadhi wataalam wakatumia mashirika mengine yaliyopo nchini kama kigezo cha kununua mitambo ya Dowans - NDIVYO TULIVYO. Ukiuliza kwa nini Kikwete amefanya hivi utaambia mbona Mkapa pia alifanya hivi, Kwa nini Mkandara blaa blaa blaa! jibu litakuja sio kuhusu Mkandara bali Hapa Kwetu pia blaa blaa zipo!..Hii yote ni kutokana na sisi kushindwa kubeba sheria inayofungamana na kosa lililotendeka badala yake tunatazama nani mkosaji..yaani kubebana kupo hata uraiani. Tumeshindwa kuwawajibisha viongozi wetu ktk maswala amabyo yana utata mkubwa na pengine ndio uhai wetu kwa sababu tuna immani na wale tunaofanana nao ktk dini, rangi, makabila au mipaka ya ardhi.
Hivyo, msukumo wa hoja yangu umetokana na pale niliposikia - MBONA TUMECHELEWA!..ile mind set ya kutazama mtu mmoja (Saudia) wakati sheria inatakiwa kusimamiwa na kutekelezwa na watu wote wakati wowote na mahala popote..
Kama sheria ingekuwa wazi huyu Kikwete asingethubutu kuwaambia Waarabu kuhusiana na ukubwa wa ardhi yetu, as a fact maneno haya kayasema hata alipokuja US pale sokoni (Nasdaq) akiuza nchi. Na ukiuliza viongozi wote wa CCM watakwambia kazi yao ni moja tu -Tunauza nchi! sasa ukiuliza wanauza kitu gani bila shaka utasikia sifa za ardhi yetu kuwa na rutuba, madini na rasilimali nyingi ambazo zinaambatana na masharti madogo sana..Hawatafuti mtaji kwa ajili ya wananchi wao, hawatafuti business partner wanaoweza kushirikiana ktk uzalishaji wa mali nchini mwetu bali wanauza Nchi!
Huu sio Ubepari hata kidogo ila ni Utumwa wa fikra..Huwezi kumyima haki hiyo mwananchi wako ukampa mgeni kisha ukajenga hoja kwamba nchi yako inafuata mfumo wa Ubepari..Ikiwa asilimia 80 ya wananchi wako hawana ardhi yao isipokuwa kwa kukodisha, kisha wananchi hawa hawa hawawezi kupewa mikopo au njia zozote za kukuza mitaji yao ktk uwekezaji huwezi ku apply Ubepari kama mfumo wa ujenzi wa maendeleo ya nchi yako kwa kutegemea wageni ndio wenye fursa na nafasi ya urithi huo....Hizi ndizo alama kubwa za Ukoloni mamboleo!..