Sauli ni kijana mdogo ambaye anapenda sana maujiko, nakumbuka alikua anapenda sana kucheza pool table.
Sa ikitokea anacheza pool table halafu ukawa mpambe wake kumpa sifa basi pesa atayopata hapo kama akimfunga mpinzani yote anakupa wewe.
Wahuni walipogundua huo udhaifu wakawa kila kona wako naye, hua anapenda kutembea na katoto kake basi hapo wahuni wakawa wamepata tiketi.
Sauli akianza kucheza wahuni wanambeba mtoto wanajidai wanacheza naye, na ukimbeba mtoto utakuta anakupa 20k anasema kamnunulie juice mtoto halafu chenchi inayosalia yako.
Ikafika hatua wahuni wakawa wanagombea kumchukua mtoto, yani kila mtu anataka aonekane na sauli kamshika mtoto wake. Na jamaa alikua hana kwere haijalishi mmeshika wangapi alikua anahakikisha kila mmoja anamtembezea michuzi
Hata mpinzani wake kwenye pool alikua akikufunga na kukumaliza pesa zako hua anakurudishia na wale wadau waliokua pembeni yake wanamshangilia nao anawatembezea michuzi
Alikua anapenda sana mashindano ya piki piki sijui kwa saizi, kipindi kile nakumbuka alikua analipia kibali polisi kwa ajili ya kufanya battle ya pikipiki na jamaa mmoja alikua anaitwa konga
Analipiki piki lake hilo moja hatari yani umbali wa kilomita 75 ye alitumia dakika 6
Ana mengi ya kustaajabisha na mengi katika hayo ni ukijana sana halafu yuko social