Sauli: Bilionea ambaye Wazungu/Wageni wanamtambua Waswahili hatujamfahamu kabisa

Hivi Dar coach ile unakuta basi imeandikwa body by dar coach ni kampuni ya bongo?, inamilikiwa na dar express?, nao si wanatumia scania?
Dar Coach wao ni body builders tu....na wanatumia chassis yoyote utakayoenda nayo mteja. Ukienda na Scania sawa, ukiwa na Isuzu sawa, iwe Faw poa tu, iwe Nissan fresh tu.

Wao wanachojali ni bei ya body aitakayo mteja. Ukiimudu wanakujengea body.

Dar Coach ni kampuni ya Bongo...inamilikiwa na Wahindi si Dar express. Walikuwepo kina Manji pia wakitengeneza body...Quality Group engineering(QG) siku hizi ni kama wame cease operations.
 
Hizi promo nasubiri mshindo,kuanzia kwenye Mabasi na sasa PR
 
Unapinga ulikuwepo?
 
Acha uongo na wewe, ameongeza gari moja DTF mwaka huu, alianza na DPC na DPN akongeza DRH then DTF kati ya hizo moja ni Mercedes Benz na tatu ni scania gemilang, hizo gari hazitengezwi Kenya mkuu, zinatoka Ng'ambo. Kwa route za southern highland scania gemilang anazo yeye na Rungwe express. Nyongeza tu Sauli ndio mabasi yanayokuwa yakwanza kuingia Mbeya Karibu kila siku.
 
Mbona kama umeumia sana? Hupaswi kuumia hivyo haya mambo madogo tu.🤣😁😁


 
Shukran nimeelewa mkuu umeeleza vizuri.
 
Unafahamu gemilang wanatengeneza body kwa chassis za Mercedes Benz, man vovlo na scania ? Unafahmu kuwa hizi unazoziita gemilang za Ava Ni mabati tupu na kuwa huo mfumo haupo kwenye body za nje? , Umeshaziona hizo gemilang za Ava zikichoka zinakuwaje , Tashrif anayo moja uone jinsi zikichoka inavyokuwa mbaya ,

F95 ilipotoka kwa Mara ya kwanza , huko Malaysia ilijengwa body na gemilang body builder, ilipopata umaarufu huko ikajulikana Kama scania gemilang,
Gemilang Ni trade mark ya kampuni inayojenga body , sio ya scania



Sent
 
I know all that mkuu...si mgeni kwenye tasnia hii. Gemilang anatengeneza body Scania anatengeneza Chassis. Ni sawa na Marcopolo anayetengeneza buses kwenye chassis za kampuni tofauti tofauti.
 
I know all that mkuu...si mgeni kwenye tasnia hii. Gemilang anatengeneza body Scania anatengeneza Chassis. Ni sawa na Marcopolo anayetengeneza buses kwenye chassis za kampuni tofauti tofauti.
Asante sana, umafahamu gemilang anatengeneza bodies kwa vovlo na man pia?

Sent
 
Unamsemea Sauli Hendry Amon ninaemfahamu mimi au mwingine!! Mbona wa kawaida sana huyu chaah labda kwako anakushtua
Siyo huyu mnyakyusa wa Tukuyu aliyeibukia madawa ya kulevya na sasa ana landmark hotel. Huyu ni mwingine
 
Hao wakishapata pesa za kula ukurupukia kwenye mabus then mfereji ukitaka chali. Kumiliki mabus ambayo ushuka thamani unajiitaje bilionea, we we ni level ya machinga tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…