Sauli ni mfano wa wamiliki wa mabasi waliofilisiwa na madereva fake

Sauli ni mfano wa wamiliki wa mabasi waliofilisiwa na madereva fake

Uongo uongooo sauli biashara ya mabasi ilimshinda mwenyewe kwa hesabu zake gari la mkopo gari zilikuwa zinajaa kila siku unasema vipi alikuwa hapati hela?? Gari inapiga iende irudi mwezi mzima iko full utasema vipi alikuwa hapati hela??

Kilichomuangusha sauli ni kwamba alikuwa anasevu pesa kuliko kulipia madeni ya gari pia alikuwa anasevu pesa kuliko kuhudumia gari ndio maana akapokonywa gari akabakiwa na gari 4 kile kibenzi kilikuwa kibovu kishenzi kilihitaji mategenezo makubwa ila kilikuwa kinafungwa spea za bei chee akaja muachia gari dada yake elika nae alikuwa hana ujuzi wowote wa mambo ya ufundi zaidi ya pesa tuu mafundi wakampiga sana pesa za spea mafundi walikuwa wanafungua spea nzima wanafunga mbovu gari ikienda inaaribika

Fundi akipewa hela ya spea mpya anaenda chukua tabata dampo anafunga gari zikawa mchezo ndo huo kufakufa hadi walipokuja kushtuka washapigwa sana huwezi simamia gari ukiwa mbali nalo bwana ndio sauli akazikamatia mwenyewe enzi za mwisho mwisho kabla ya ajali ya basi lake moja kuungua baada ya kubaki mbili akaamua kupaki hivi karibuni ndio alitaka zirudisha zikishapigwa sevis kubwa hadi rangi walikuwa wanamalizia tu siti cover ndio hivyo mwamba akafariki. Na sauli aliagiza G7 kenya yeye na katarama kwa pamoja iyo ishu kuwa aliagiza yutong ni uongo mtupu. Wale wachina walipoga tu picha.
 
Biashara ya mabasi ya abiria kwa Dunia ya leo si ya kushadadia ma mbio yasiyo na tija bali ni akili yenye wingi wa ubunifu ndaniye kwa mambo yatakayomvutia abiria taraji.

Mfano Sauli ni wazi alifilisiwa na madereva wake kwa kushadadia sifa za kijinga za mwendo kasi hali iliyosababisha mabasi mengi kuharibika na kwayo kutumia gharama kubwa kwenye matengenezo na mwisho kushindwa kujiendesha na wadai wakafilisi vyao.

Mwisho wa siku Sauli imebaki simulizi.

NB: Kisbo ana bahati ya kung'amua mapema kurejea kwenye ustaarabu vinginevyo naye ingeshabaki simulizi.
Shabiby anaongoza kwa biashara ya mabasi. Kwaanzia customer care, wafanyakazi wake wote.
 
Mtanzania gani utampa investment ya mamilioni akakutafutie pesa kama wanavyoita wao?

Ukweli mchungu hakuna mwenye bus au Lori atatoboa.

Hata latra hilo wanajua.

Wote unaowaona ni just a matter of time.
Naona akili yako haina akili kuna watu walianza n'a gari moja leo hii wana gari 300 n'a kila baada ya Miez kadhaa anaongeza fleet sasa hiyo hawawez kutoboa unataka atoboe tundu lako?
 
Kiswahili unaelewa lakini ndugu? Hebu rejea kusoma kama nimeandika au hata kumaanisha unachosena hapa.

Wazi wazi nimesema nunua bus la mamilioni, mpe dereva na konda uone kama watakuletea lolote!
Na hawa walioko kwenye game mwaka wa 20 km shabiby kilimanjaro wao wanaletewa nn? Tatzo watu mnajifanya wajuaji na ktk ukoo wenu hakuna hta mwenye biashara ya maandazi mnaropoka tu
 
Mtanzania gani utampa investment ya mamilioni akakutafutie pesa kama wanavyoita wao?

Ukweli mchungu hakuna mwenye bus au Lori atatoboa.

Hata latra hilo wanajua.

Wote unaowaona ni just a matter of time.
Ni sahihi. Kuna ndugu yangu alikuwa na lori 7 zinazochukua mizigo Bandarini Dar na kupeleka nje ya nchi, sasa anatumia watu na kulaumu kila mtu.

Biashara ya usafirishaji inahitaji umefika na kutokuelewa na nyani. Ukiendelea Madereva sijui Matingo, utafilisika vibaya.
 
Unaweza kuwa sahihi mkuu, ila tu kwa taarifa yako Marehemu Sauli alikuwa kishaagiza unit 6 za yutong. Sema mipango ya Mungu si ya mwanadamu. Aendelee kupumzika alipojiandalia.
Unit za yiutong bado asingetoboa, for the record sauli kama alivyo katarama mwanza wanakua tofauti na wapinzani wao kwa sababu wanatumia unit za scania,
Yuotong haiwezi pambana na zhongtong ambazo tayari wapinzani wake wakuu, newforce na Achimwene wanatumia. Angefeli mapema kweupe.
 
Na hawa walioko kwenye game mwaka wa 20 km shabiby kilimanjaro wao wanaletewa nn? Tatzo watu mnajifanya wajuaji na ktk ukoo wenu hakuna hta mwenye biashara ya maandazi mnaropoka tu
Acha ujuaji na matusi dogo. Tunaeleweshana tu. Hata hao ni mida tu mkuu japo hatuwaombei Mabaya. Biashara ya usafirishaji ni ngumu sana ndugu yangu.

Leo kampuni nyingi za mabasi mazuri zimefilisika. Hata hao unaosema wengi wanaishi kwa mikopo toka Mabenki. Muulize Sumry, kaamua kwenda kulima huko kwao Sumbawanga.
 
Mtanzania gani utampa investment ya mamilioni akakutafutie pesa kama wanavyoita wao?

Ukweli mchungu hakuna mwenye bus au Lori atatoboa.

Hata latra hilo wanajua.

Wote unaowaona ni just a matter of time.

Word. Hakuna biashara pasua kichwa kama ya mabasi.

Scandinavia iliyokuwa gold standard na iliyoleta mapinduzi kwenye hii sekta ilikufa kifo cha mende the rest don't stand a chance.

Hood, sumry wote chali.
 
Unit za yiutong bado asingetoboa, for the record sauli kama alivyo katarama mwanza wanakua tofauti na wapinzani wao kwa sababu wanatumia unit za scania,
Yuotong haiwezi pambana na zhongtong ambazo tayari wapinzani wake wakuu, newforce na Achimwene wanatumia. Angefeli mapema kweupe.
Kwanza unajua yutong ni nn na zhongtong ni nn ila waswahili bana ujuaji mwingi elimu hakuna
 
Kingine kilichomfilisi Saul ni kuwa aliktapeli mzungu kwa ishu ya dhahabu fake yule mzungu akamfuata JPM kulalamika Sauli akaingia kwenye madeni ili alipe
 
Acha ujuaji na matusi dogo. Tunaeleweshana tu. Hata hao ni mida tu mkuu japo hatuwaombei Mabaya. Biashara ya usafirishaji ni ngumu sana ndugu yangu.

Leo kampuni nyingi za mabasi mazuri zimefilisika. Hata hao unaosema wengi wanaishi kwa mikopo toka Mabenki. Muulize Sumry, kaamua kwenda kulima huko kwao Sumbawanga.
Hakuna biashara rahisi zote ni ngumu inategemea biashara unaindeshaje
 
Back
Top Bottom