SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Hilo baraza la seneti limejaa wakoloni watupu kwahiyo kama hao madaktari walishaajiriwa makazini ndio wanakuwa sio madaktari tena kwa ajili ya karatasi moja tu ya matokeo?
Huyo ndio muafrika ni zaidi ya shetani halafu ni chuo Cha mtakatifu fransi,nyie mnojiita watakatifu kumbe ni pe......p.....o
 
Hilo baraza la seneti limejaa wakoloni watupu kwahiyo kama hao madaktari walishaajiriwa makazini ndio wanakuwa sio madaktari tena kwa ajili ya karatasi moja tu ya matokeo?
Kwani hizo transcripts waliziiba? Na kama hawakuziiba; nani aliwapa? Yaani kuna watu wana bahati sana nchi sina mamlaka nao!

Yaani watu wanaaanza tena kuwachezea madakatari wetu wakati wao wapo serious kazini wanafanya kazi?
 
Hili suala wale waliopata ajira rasmi serikalini ndo watauonaa motoo vizurii yanii KESHO MBALII MABOSS WATAANZA KUWASUMBUA wasipoenda mahakamani kupindua haya maamuzi kibarua ndo kimeota nyasii yani huu mwezi ndo mshahara wa mwisho watakula. Chuo kimezingua snaaa haya maamuzi ya kukurupuka mnoo
Kabisa, dunia haiko fair kabisa Ndugu daaaah [emoji25]

Lakini nani ajuaye isijekuwa ile kanuni ya "just make the problem then solve it" imetumika?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la kutoa cheti kwa makosa/kimakosa linarekebishika (ni curable) Utaratibu wa kuzingatia katika kufanya Marekebisho ni pamoja na kuretrieve hizo Transcripts. Na hilo SAUT wamelifanya kwa muda mrefu sana lakini bila mafanikio - Madokta wakekaza shingo. Hatua ya mwisho ndo hiyo ya kuzifuta juu kwa juu ww unabaki na karatasi lisilo na thamani i.e. halitambuliwi kisheria. Endapo Hawatafikia Muafaka, bado ni hatari kubwa zaidi kwani Waajiri (Serikali au Private Sector) watafuatiliwa kuhusu Ajira kwa Mujibu wa Qualifications. Wewe Utakuwa ni mmojawapo wa waathirka - Huna qualifications za Udaktari. Hapo utakuwa mgeni wa nani???
Lakini kwa nini kote huko?? Si urudishe karatasi la watu halafu mengine mtayajenga? Hakuna lisilowezekana chini ya hili jua. Nyie ni watu wazima -fanyeni mambo yenu ki-Utu uzima. Umeshafanya kazi kwa zaidi ya 6yrs na nina amini unao uzoefu wa kutosha kazini. Hili la karatasi linakushindaje?
Unaogopa nini?
Kwa watu wanaopenda ku practice sheria wataanza kuwafuatilia popote pale walipoaj8riwa na kuwawekea mapingamizi ya kuendelea na ajira zao kwa kuwa hawana vyeti
 
Zuio huwekwa ili hukumu isitimilizwe

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app

Ndugu Hakuna injunction kwenye rulling and judgment. Injunction ni kuomba kuweka zuio kwa Jambo lililoamuriwa na chombo ambacho sio Cha mahakama, ili mahakama isikilize shauri Hilo. Refer kesi ya akina mdee.
 
Kwa watu wanaopenda ku practice sheria wataanza kuwafuatilia popote pale walipoaj8riwa na kuwawekea mapingamizi ya kuendelea na ajira zao kwa kuwa hawana vyeti
Yeah. Hiki ndo alifanyaga Magu kipindi kile.
 
Kaendeshe barabarani bila leseni uone
elewa kwamba leseni haikuondolei ujuzi wa kuendesha gari. Huo ni utaratibu usio na maana. Ukute kuna shida barabarani dereva mwenye leseni kapata shida mi nisio na leseni niache kuendesha gari kuwahisha abiria ili kutatua tatiza kwa dharura? Ujuzi kwanza
 
Tuanze na yeye kumfutia vyeti vyake vyote hadi uprofessor na wengi kwenye bodi.
Maana wanivuruga mpango wote wamaisha....
 

Chuo kikuu cha St. Augustine kimebatilisha shahada ilizotoa kwa madaktari 162 waliohitimu chuo cha udaktari cha St. Franscis kuanzia mwaka 2015-2019.

St. Augustine imechapisha tangazo kwenye gazeti la Daily news ikitoa notisi kubatilisha shahada za wanafunzi hao 162 ambao inadai wamegoma kurejesha nyaraka ya matokeo(Transcripts) ambazo walipewa bila baraza la senete la chuo kuwa na taarifa na kuziidhinisha.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa seneti ya chuo hicho, balozi Prof Costa Mahalu imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mkutano wa senet ilioketi mwezi wa pili.

===

Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kimewafutia shahada Madaktari 162 waliohitimu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha St Francis (SFUCHAS) kuanzia mwaka 2015-2019.

Notisi kwa Umma iliyochapishwa katika Gazeti la Daily mnamo Jumatatu (27 Machi, 2023), ilisema wahitimu 162 walikataa kimakusudi kurudisha nakala za masomo, 'Transcript' walizopewa bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti ya chuo kikuu licha ya kukumbushwa kwa muda mrefu.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa seneti ya SAUT Balozi Prof. Costa Mahalu inaeleza uamuzi wa kuondoa shahada hiyo umekuja baada ya kikao cha Seneti cha Chuo Kikuu kilichofanyika Februari mwaka huu.

"SAUT kupitia Seneti ya Chuo Kikuu katika Seneti yake ya 54 isiyo ya kawaida, mkutano uliofanyika tarehe 25 Februari 2023 katika chuo kikuu cha SAUT na kwa mujibu wa Kifungu cha 47(1) & (2) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sheria Na. 7 ya 2005 ikisomwa pamoja na Vifungu. 6(3)(ii), 7,8 na Kanuni ya 29 (1) ya Mkataba wa SAUT GN. HAPANA. 580 ya 2020 ilifuta shahada walizopewa wahitimu 162 wa Madaktari wa Udaktari wa SFUCHAS kuanzia 2015 -2019,” inasomeka taarifa hiyo.

Source: Daily News
Hatari
 
Back
Top Bottom