SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Ni sahihi ; ila baadaye utafute uhalali wa ww kuendesha barabarani Vinginevyo utakamatwa na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
 
Ni sahihi ; ila baadaye utafute uhalali wa ww kuendesha barabarani Vinginevyo utakamatwa na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
kwa hiyo walifutiwa wanahesabika ni debe tupu hakuna maarifa waliyonayo?
 
kwa hiyo walifutiwa wanahesabika ni debe tupu hakuna maarifa waliyonayo?
Maarifa, ujuzi na Uzoefu kazini (Kwa waliopata ajira) wanavyo ila Nani atakayemdhamini mtu ambaye hana cheti cha kuthibitisha kuwa yy ni daktari? Kwa mfano Malawi wanataka kumwajiri mmojawapo (au hata zaidi ) wa hao waliofutiwa vyeti. Malawi watahitaji CV ikiambatanishwa na Vyeti. Hao madaktari watavitoa wapi? Je, hapa nchini ikitokea kunafanyika sensa ya madaktari walio kazini, wao siku ya tukio wataonesha vyeti gani? Rejea enzi za Uncle Magu na zoezi la kuhakiki vyeti vya Taaluma makazini. Yani Watumishi tuliwekwa kwenye tension kali.
 
Kwa kuwa jamii imejiwekea utambulisho huo na imezoeleka tutafuata tu utaratibu huo. Mi mwenyewe kuna kozi nilisoma na nina uwezo mkubwa wa kufanya kazi niliyoisomea muda mrefu na uzoefu ninao, kwa kuwa nilikosa cheti cha kunithibitisha kuwa nimesomea kazi hiyo ilibidi mfumo wa ajira uniteme bila kujali uwezo wangu mkubwa wa kumudu kazi hiyo. Kazi hiyo naiweza na naipenda ila mfumo hauwezi kunitambua na imebidi nifute kabisa maarifa hayo kichwani mwangu kwa kuwa hakuna mahali nitatambuliwa zaidi ya kufanywa kibarua tu kwa sababu maarifa yakiingia kichwani hayafutiki daima
 
Unaweza kutoboa hapo kwa kufanya mtihani private candidate kwenye Centre utakayoona kwako itakuwia rahisi kuhudhuria. Ukifaulu mtihani huo cheti utapewa.
 
Mnaoshabikia hili kwamba hao madaktari wako sahihi mnawadanganya, imekula kwao. Kwa nini nao kama kweli wamehitimu kihalali wasirudishe hizo transcripts? Ona sasa kilichowakuta! Niko upande wa Baraza la Seneti!
 
Usiombe yakukute 🤔, ila SERIKALI inabidi ifanye maamuzi sahihi kuhusu ili swala ,
1. Kutengua aya maamuzi ya kukurupuka.
2. Kuiwajibisha hiyo seneti uchwara hususani bwana costa titch.
3. Chuo kiwe na utaratibu mzuri wa kutoa transcript kwa wahitimu.
 
Mnaoshabikia hili kwamba hao madaktari wako sahihi anawadanganya, imekula kwao. Kwa nini nao kama kweli wamehitimu kihalali wasirudishe hizo transcripts? Ona sasa kilichowakuta! Niko upande wa Baraza la Seneti!
Hebu fikiria mtu yuko kikazi Mtwara na SAUT iko Mwanza. Gharama ya kurudisha hiyo transcript imekaaje au wanairudisha kwa mtindo gani?
Kabla ya Tamko la kutengua vyeti vyao madokta hao walikuwa na walihesabika wamehitimu kihalali. i.e. Tangu 2015- 2023 walieleweka wamehitimu kihalali na pengine baadhi yao walisha ajiriwa. Ni baada ya Tamko la SAUT la March 2023 wameanza kuhesabika na kueleweka hawajahitimu kihalali. Kwa mantiki hiyo miaka 8 walikuwa madokta halali lakini as from March 2023 hao sio madaktari tena waliohitimu kihalali. Sababu inayotolewa haina mashiko. Eti kwa sababu wameshindwa kurejesha Transcripts. Ina maana hakuna njia nyingine ya kuweza kuzipata hizo Karatasi? OK, tuseme ikatokea wakazirudisha. SAUT watafanyaje kuhusu Tamko lao na yatokanayo (Impact) yake kwa hao madaktari? Kuna kitu hapo hakijakaa vizuri. Pande zote zina mapungufu. Ni kitu gani kimewasukuma hao SAUT kutoa Tamko lakini kwa kuchelewa hivyo 2015 -2019 walikaa kimya, lakini Tamko linatoka March 2023. Uvumilivu waliokuwa nao umeisha? Kwa nini hawakutoa Ultimatum na Kuweka bayana Hatua za Kinidhamu zitakazochukuliwa kwa daktari atakayekaidi agizo hilo ikiwa ni pamoja na kufutiwa cheti?
 
Yeah. Senet ya chuo inapaswa ioneshe kutenda na kufanya maamuzi kwa kuzingatia weledi mkubwa lakini pia kujiepusha na maamuzi yanayovuruga na kuathiri mustakabali mzima wa maisha ya Wahitimu wa chuo hicho. Inafaa Senet ione kwamba bila kuwepo kwa wanafunzi wanaosoma hapo chuoni, Senet hiyo haina sababu ya kuwepo hapo chuoni ni useless.
Na wanafunzi watambue kwamba bila Senet hapo hapatakuwa ni chuoni bali ni kama mkusanyiko tu wa vijana bila malengo - ni kusanyiko la wahuni fulani hv.
Ka mantiki hiyo, Point 1-3 ulizotaja hapo juu 👆 👆 ni ushauri mubashara sana.
 
Hii ishu ina mengineyo,Sisi wa nje tusijaji SANA ,labda chuo kimebaini wahitimu walifaulu kwa mchongo
 
Kuna Mwanangu ni Graduate wa 2019 na jina lake nimeliona hapo
 
Tuna tatizo la uhaba wa madaktari nchini ukilinganisha Na mahitaji na idadi ya watu hivyo uamuzi ulofanywa wananchi hatuwezi kukubaliana nao mpaka tupewe ufafanuzi wa kina.

Iwapo kuna tatizo la msingi na kiufundi matharani uhitimu wao kuwa na makosa basi wananchi tujulishwe.
 
Huo ni mwanzo tu, kuna PhD za kufutwa haraka iwesekanavyo.
1. Dr Abood
2. Dr musukuma
3. Dr Biteko
4. Dr. Gwajima Bishop
5. Dr Samia
6. Dr Hans M
6. Dr Jafo
Ongezeeni wengine
Kuwa na heshima na shule za watu huyo Dr gwajima na Biteko wamekaa darasani heshima vyuo walivyosoma .
 
Uspanic Mkuu Thread Iko wazi ni St Francis ni kampasi nafikiri hii itakuwa ya Ifakara kama Niko sawa.Ila Sauti Wana vyuo vingi Vya Udaktari kikiwemo Bugando.Niko tayari kurekebishwa.
BUGANDO wameshajitenga na SAUT muda sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…