KWELI Sauti ya Keefe D yasikika akikiri namna alivyoahidwa dola milion 1 na P. Diddy amuue Tupac

KWELI Sauti ya Keefe D yasikika akikiri namna alivyoahidwa dola milion 1 na P. Diddy amuue Tupac

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Salaam ndugu zangu,

Leo katika pita zangu mitandaoni nimeona baadhi ya kurasa zinazoweka masula ya burudani na habari za Wasanii zikieleza kuwa kuna sauti ya Keefe D imevunja ikikiri kuhusika na kifo cha 2 Pac.

Upi ukweli kuhusu sauti na sakati hilo?

1697258643246.png
 
Tunachokijua
Duane Keith Davis 60 ni mzaliwa huko Compton, California nchini Marekani. Anajulikana zaidi katika tasnia ya burudani kwa jina la "Keffe D,". Anaelezwa kuwa alikuwa Mwanachama wa genge la California, South Side Compton Crips.

Davis amepata umaarufu ulimwenguni sababu ya kuwa ndiye shahidi pekee aliyebaki hai kati ya wote wanaohusishwa na kifo cha Rapa 2 Pac.

Tangu Julai mwaka 2023 kumekuwapo taarifa kutoka vyombo mbalimbali duniani vikielezea suala la Polisi nchini Marekani kumshikiia Keffe D kwa ajili ya kuendeleza uchunguzi juu ya mtu aliyehusika na kifoo cha Rapa 2 Pac.

Zipo pia taarifa katika mitandao ya kijaamii zikidai kwamba hivi karibuni imesikika Sauti ya Keefe D ikikiri kumuua Rapa Tupac kwa kuahidiwa Dola milioni moja na Rapa P. Diddy.

Upi ukweli wa sakata hili kwa sasa?
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali vya uhakika vya kitaifa na Kimataifa vilivyoelezea tukio hili ili kupata uhalisia wa tukio hili kama ifuatavyo:

Mnamo September 29, 2023 Ukurasa maarufu wa Marekani wa New York Post ulieleza sakata la sauti hiyo ya Keffe D pamoja na namna alivyotoa utetezi wake juu ya mauaji ya Tupac.

Ufafanuzi wao pia unaendana na na ufafanuzi uliotolewa na Ukurasa wa The Sun U.S ambao wanabainisha kuwa sauti hiyo ilitokana na mahojiano kati ya Keffe D na polisi akieleza kwa kina tukio hili andiko hili kama ifuatavyo:

Ikiwa ni wiki chache zimepita tangu mwanachama wa kundi la South Side Compton Crips akamatwe kwa kuhusika na mauaji ya Rapa Tupac Shakur, kuna Video na Sauti zimeanza kusambaa mitandaoni zikimwonesha Davis akikiri wazi kufahamu kila kitu kuhusu mauaji hayo.
Katika mahojiano mbalimbali aliyofanya, Davis maarufu kama Keefe D anasimulia juu ya uwepo wake kwenye gari jeupe aina ya Cadillac ambalo lilipita karibu na BMW ya Tupac kwenye makutano barabara na kufyatua risasi zilizochukua uhai wa Nyota huyo wa Hip Hop.
Mwaka 2018 wakati akizungumza katika makala ya Netflix, "Death Row Chronicles", Davis aliweka wazi kuwa ni mgonjwa na anataka kufichua kilichotokea katika usiku wa mauaji ya Tupac.
"Nilikuwa mfalme wa Compton, mfanyabiashara wa dawa za kulevya, ni mimi pekee niliye hai ninayeweza kukueleza hadithi kuhusu mauaji ya Tupac," Davis alisema.
"Watu wamekuwa wakinifuatilia kwa miaka 20, natoka hadharani sasa kwa sababu nina Saratani. Na sina kitu kingine cha kupoteza. Ninachojali sasa ni ukweli."
Aidha, kwa maneno yake mwenyewe katika kitabu chake kilichochapishwa mwaka 2019 "Compton Street Legend" Davis, 60, anaeleza jinsi alivyokuwa Las Vegas siku ya tukio, Septemba 7, 1996, wakati akitoka kutazama pambano la Ndondi la Mike Tyson lililofanyika kwenye hoteli ya MGM.
Baada ya mechi, Tupac na Bosi wa 'Lebo' ya muziki ya Death Row records, Marion 'Suge' Knight na wanaodaiwa kuwa genge lao, Mob Piru Bloods, walimvamia mpwa wa Anderson kwenye hoteli hiyo, ugomvi ambao ulinaswa kwenye Kamera.
Anaeleza zaidi kuwa yeye (Davis) na wafanyakazi wake walikuwa sehemu tofauti hadi wakati kundi lingine la "118 East Coast Crips" walipokuja kuwafahamisha kuwa "baadhi ya watu kutoka Death Row, wamemshambulia Mpwa wao.
Pia katika Kitabu hicho, Davis anasema tayari alikuwa amekubali kufanya kazi ya kulishambulia kundi la Tupac kutokana na ugomvi uliokuwepo baina ya Tupac na hayati Notirious BIG.
Kazi hiyo alipewa na wapinzani wa Tupac akiwemo Sean Combs maarufu kama Puff Daddy, lakini anasema hakwenda Vegas kwa nia ya kuingia kwenye matatizo na Tupac ingawa anakiri baada ya mpwa wao kushambuliwa, alilichukulia jambo hilo kuwa binafsi kwake.
Wakiwa wanajiandaa kuelekea Club 662 ambapo Tupac alipangwa kutumbuiza, Davis anasema mwanaume anayeitwa Eric Von Zip alimvuta ndani ya gari lake aina ya Mercedes Benz na kumuonesha Bunduki, na inasemekana alimwambia muuaji huyo huku akimwonesha Tupac na kusema: “Ni wakati wa kupata pesa.”
Davis, Anderson na wanaume wengine wawili walisubiri kwenye maegesho katika Club ya usiku ili Tupac na wasaidizi wake watoke nje. Davis ananukuliwa tena akisema “Hakukuwa na haja ya maneno; sote tulielewa kwa nini tulikuwa hapo,” aliandika.
Baada ya Tupac kutofika kwa muda wa saa moja na nusu, Davis aliamuru watu wake waondoke na kwenda kwenye duka la kuuza vileo. Wakati huo walikutana na gari la Tupac na Suge, ambalo walilitambua mara moja kwa sababu Tupac alikuwa upande wa dirisha la abiria huku mashabiki wakimwita jina lake.
Gari ya Davis iligeuza na kujisogeza kando. Davis anadai kuwa alimwona Tupac akiinama chini, ndani ya gari (kwa kawaida wahalifu huchukulia kuinama huko kama kitendo cha kuchukua Silaha), na "hapo ndipo Risasi zilipoanza."
Anakiri zaidi "Mmoja wa vijana wangu kutoka Siti ya yuma alichukua Bunduki na kuanza kushambulia," Davis aliandika katika kitabu chake. "Wakati risasi zikiendelea kuruka, nilijitupa chini ili nisije nikapigwa."
Katika mahojiano mengine Davis alidai Anderson, ambaye alipigwa risasi na kufariki mwaka 1998, ndiye aliyempiga risasi Tupac mara 4 kifuani ingawa Anderson alikana kuhusika na mauaji hayo na hakuwahi kushtakiwa.
Baada ya risasi kunyamaza, Davis alisema Cadillac yao iliondoka na hakuna aliyewafuata na kuongeza “Sijui ni kwa nini Polisi wa Vegas hawakuangalia mikono ya Tupac kuona kama alishika Bunduki kujibu mashambulizi kwasababu Gari letu pia lilipigwa risasi. Sielewi kwa nini watu wanafanya kama Tupac alikuwa malaika,” Davis aliandika.
Kuhusu Rapa P. Diddy kuhusika?
Ukurasa wa The Sun U.S unafafanua kwa kina namna Keffe D ambaye alifikishwa katika mahakama ya Las Vegas mara kadhaa amekuwa akielezea na kumhusisha P. Diddy kuwahi kutuma kummaliza Pac na bosi wa lebo ya rekodi Suge Knight, ingawa P.Diddy amekuwa akipinga shutuma hizo mara zote na kuziita ni za kipuuzi.

The U.S. Sun wanaeleza kuwa madai ya P. Didy kuhusika na kifo cha Tupac yalitolewa na Keffe D katika kupitia kitabu chake na kwenye mahojiano aliyofanyiwa mitandao ya kijamii - na hata katika mahojiano ya siri na polisi wa LAPD. Sehemu ya andiko hili linaeleza

Mshukiwa wa mauaji ya Tupac Keffe D akitoa ushahidi mbele ya jeshi la Polisi ameeleza kuwa kweli amehusika na tukio na hakufanya hivyo tu bali alitumwa na Rapper mkongwe P Diddy kuwa Endapo akifanikisha mauaji hayo atapewa kiasi cha Dollar za kimarekani $1 Millioni.

Pamoja na shutuma hizi kuibuka tena hivi karibuni lakini Wawakilishi wa Diddy hawakutoa maoni walipoulizwa kuhusu madai hayo na bado hakuna uthibitisho wowote kuhusu ukweli wa shutuma hizo zinazoteolewa na Keffe D dhidi ya P Diddy.

Aidha, pamoja na kuvuja kwa sauti hizi, JamiiForums imebaini kuwa sio za Alhamisi, Oktoba 12, 2023 kama inavyodaiwa, bali zimekuwepo mtandaoni kwa muda sasa kama ambavyo gazeti la New York Post liliripoti Septemba 29, 2023.
Back
Top Bottom