Bt yaezakuwa ni mitizamo wao binafsi.Chadema kutowakana ndugu hawa hadharani haiwasaidii ..
Ndugu brazaj unataka CHADEMA waje kukana au ku - clarify nini kwenye hiki nilichokipost mimi?Kilikuwa na uzi huu:
Lissu rudini ubaoni, Majukwaani hakutamng'oa CCM
Katika mapendekezo ilikuwa issue ya habari na propaganda.
Kwamba hadi sasa hawajaukana hadharani uzi huu wa ndugu Uzima Tele, ni jambo la kushangaza sana.
Haya sidhani kuwa ni mawazo ya Chadema bali ya chawa tena wasiojitambua.
Kwa hakika ukombozi si Kwa njia hii Chadema wanaonekana kuchukua.
Bila kutambua kuwa hakuna adui wala rafiki wa kudumu bali agenda, hakuna mafanikio hapo.
Ninakubaliana na list hii:
TEC, Mbarikiwa, Lissu, Dr Slaa, Mwabukusi, Madeleka, Mdude, Dr Nshalla , Mwamakula, nk nk ndo wanabeba agenda za wananchi Kwa vitendo.
Nikurekebishe hapa: Kina Bashiru na Ndugai na wa namma hiyo inabidi wajitokeze wazi wazi huku tujiridhishe zaidi.
Ni kweli kuwa hata wao si haba.
Wewe huwezi kuandamana? Unasubr uongozwe na CHADEMA?CDM ndio inasaliti watz ktk HOJA ya Bandari Kwa kuipeleka kwenye mikutano ya hadhara Badala ya kuongoza maandamano yasiyo na kikomo wakiungana na watz, sauti ya watz,Hadi Bandari zetu na maliasili zetu ziheshimiwe na Watawala.
Ndugu brazaj unataka CHADEMA waje kukana au ku - clarify nini kwenye hiki nilichokipost mimi?
Haya ni mawazo na mtazamo wangu binafsi msingi wake ukiwa ni mjadala unaoendelea katika jamii juu ya kikundi hiki kinachoitwa Sauti ya Watanzania kilichoibuka ghafla na kuivamia CHADEMA..
Mimi si mwanachama wa CHADEMA. Mimi ni mwananchi tu niliyeko huku kwetu Shinganga na ni mpenzi sana na huwa nakiunga mkono CHADEMA ktk harakati zake za kisiasa..
Hawanijui wala Mimi simjui kiongozi yeyote wa CHADEMA, hata wa tawi tu achilia mbali wa kitaifa au mkoa..
Unajua maana ya maandamano?Wewe huwezi kuandamana? Unasubr uongozwe na CHADEMA?
Wewe huwezi kuandamana? Unasubr uongozwe na CHADEMA?
Unajua maana ya maandamano?
Yes, you are right...Kumbe wala si mwanachama halafu kwa kujua au kutojua umeandika ugolo huo?
Ushauri wangu kwa watu kama wewe ni huu hapa:
CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni
Nitawashangaa mno wasipokutolea uvivu na bila kuchelewa.
Ninyi ni ma CCM au vibaraka wao kwa kujua au kutokumjua.
Si mbaya kujua, hatudanganyiki!
Yes, you are right...
Mimi siyo mwanachama wa CHADEMA. Lakini ni shabiki na mpenzi wa chama hiki. Ndicho ninachokiamini kuliko vingine vyote..
Kama nilichokiandika ni ugolo kwako, it's ok. Ni hiari yako uone ugolo au buskuti. Ila nafurahi umeusoma ugolo na hulali Kila siku inachangiwa..
By the way, kwani ili kuandika kuihusu CHADEMA ni lazima uwe mwanachama? Wewe brazaj ndiyo unajua hivi siyo??
Kama CDM ingekuwa na msimamo isingemchukua LowasaHivi unajua credibility
Mkuu kwenye siasa kama ukiwa malaya huna msimamo hakuna atakayekuamini haijalishi una point nzuri kiasi gani
Hizi makala zako ndefu zinasisitiza tu kuwa wewe tayari uko kazini kuponda kundi moja na kukingia kifua kundi jingine.Unajuaje kuwa Sauti ya Watanzania si huyu shetani aliyejigeuza kuwa malaika wa nuru? Ni kwa kuwa tu wanazungumza lugha kama yenu?........ Oooh, utaliwa mchana kweupe!!!
Hizi makala zako ndefu zinasisitiza tu kuwa wewe tayari uko kazini kuponda kundi moja na kukingia kifua kundi jingine.
Huna 'objectivity' tena katika maandishi yako.
Ndiyo maana nikasema toka kule mwanzo kwenye ile mada nyingine, kwamba huenda tayari uko ndani ya kibarua kinachotokana na fedha za waarabu zinazotumika kwenye kampeni ya kutuwekea serikali wanayoitaka wao.
Narudia tena, hayo ni maoni na mtazamo wangu binafsi kwa kinachoendelea ktk jamii na kuzua mjadala nami nashiriki mjadala huu kama tu wewe unavyoshiriki..Hizi makala zako ndefu zinasisitiza tu kuwa wewe tayari uko kazini kuponda kundi moja na kukingia kifua kundi jingine.
Huna 'objectivity' tena katika maandishi yako.
You're absolutely wrong. Fikra zako hizi ni batili..Ndiyo maana nikasema toka kule mwanzo kwenye ile mada nyingine, kwamba huenda tayari uko ndani ya kibarua kinachotokana na fedha za waarabu zinazotumika kwenye kampeni ya kutuwekea serikali wanayoitaka wao.
Wewe ni chawa wa wapi na wa nani?Kama huyo nimelazimika kuandika uzi huu:
CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni
Pana haja ya kuwa nao makini.
EEEeeenHeeeee!Sijalazimisha mtu (ukiwemo wewe) kukubaliana nami au kuona sawa na nionavyo mimi. Kila mtu ana mawazo na mtazamo wake juu ya jambo lolote likiwemo hili. Huu ndio unaoitwa "uhuru wa mawazo" kama ulikuwa hujui..
Unapigania hao hao unaowaita "wakoloni weusi, CCM", na hiyo kama ulivyosema mwenyewe, ni haki yako.Na hongo yao kwangu ni hii....ππππ Nawaamini, nawajua na kuelewa misimamo yao na wanachokipigania katika nchi yangu...
Kwa hiyo, kila hatari ya hujuma inayoweza kuwa mbele yao, ni lazima kupiga kelele kama tulivyofanya miaka yote kukilinda chama hiki tegemeo la wanamapinduzi wengi.!
Hoja yako ni nini hasa?Wewe ni sehemu ya mkanganyiko mkubwa unaoendelea ndani ya chama hicho cha CHADEMA.
Ndivyo unavyodhani siyo?Hili kundi lenu likifanikiwa kukisalimisha kwa CCM ya Samia, Mwenyekiti Mbowe atakuwa kamaliza kazi yake muhimu.
Dah!Hoja yako ni nini hasa?
Ndivyo unavyodhani siyo?
Yaani ni kuwa;
β Una macho, lakini huoni...
β Una masikio, lakini husikii...
β Kikubwa zaidi ni kuwa, kwa kuwa hujajaliwa yote hayo basi hata kuelewa huwezi kuelewa..!!
##Kwani hii story ya CHADEMA itakufa au imeuzwa, umezianzisha wewe leo kuisema? Ni zaidi ya miaka 30 lakini jamaa wapo..!!
##Unajisumbua bure. Ni kwamba, waambie Sauti ya Watanzania warudi mezani wapange mambo yao vyema, na kama wanataka kutumia jukwaa la CHADEMA kama mshirika wao, basi wana kazi ya ziada kujenga trust kwao na kwa wananchi. Kanuni kuu ya ushirika wowote ni TRUST..
Chadema na Mbowe wanapambana vipi na hiyo Sauti ya Watanzania? Hivi hao wakina Slaa walishirikiana na Chadema kupanga hayo maandamano? Aidha, hivi kwa nini wanaamini kuwa bila Chadema kuungana nao hawatafika mbali? Mbowe amesema kuwa wao wana ratiba yao na wataendelea nazo. Na kuwa hana shida na wanachadema kushirikiana na Sauti ya Watanzania ila kichama wataendelea na ratiba yao. Kwa nini hiyo Sauti ya Watanzania wasijipange ku complement hiyo mipango ya Chadema? Kweli wanataka waache kila kitu wawafuate wao? Kweli stupid as stupid does.Mbowe na genge lake hawawezi kuungana na watu wenye nia ya kweli ya kuitoa CCM madarakani. Chadema hawahawa walikua busy kupambana na kundi la Hayati Magufuli. Hili ni kundi muhimu sana kwao na ni mtaji wa kisiasa kuitoa CCM madarakani ila wao walikua busy kulipiga vita. Sio bahati mbaya, Huu ni mkakati wa CCM kuhakikisha wanatugawa ili waendelee kututawala na moja ya masharti waliyopewa Chadema ni kuwa mbali na sukuma gang na aina yoyote ya watu wenye kutishia kuitoa CCM madarakani. Now wako busy kupambana na sauti ya watanzania, sio bahati mbaya. Hii ni mikakati ya CCM wakiwatumia akina Mbowe na genge lake. Hizi operation wanazofanya akina Mbowe hazina madhara yoyote kwa CCM na ndio maana hawapigwi pin. Kila linapotokea jambo Zito kwa CCM basi Mbowe hutumika kuzima moto kwa akili nyingi sana. Mbowe ndiye aliyetumika kuzima operation UKUTA na ni Mbowe ametumika kuzima Vuguvugu la bandari kwa kuja na operation zake Uchwara. Niulize tu toka wameanza hizo operation mmesikia utawala ukitikisika hata nywele?
Jamaa anajichanganya,Mbowe ni mnafiki na anapiga Hela ya serikali vizuri sana kupitia kujipendekeza kwa Samia na viongozi wa CHADEMA top brass ukimuondoa Lissu wote wanawaza Ubunge 2025 na wanaona wakimuuzi Samia watakosa kitumbua.
CCM ikibanwa kwenye Kona Mbowe utamuona anarudi nyuma badala ya kuchochea zaidi mapambano.Wale wakina Heche,Msigwa,Mnyika et al wanaogopa kupingana na Mbowe simply wanajua watakosa mkate.Lissu peke yake ndiyo mara nyingine anapingana na misimamo ya Mbowe hasa kwenye Maridhiano na CCM!
Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app