"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....

"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....

Kilikuwa na uzi huu:

Lissu rudini ubaoni, Majukwaani hakutamng'oa CCM

Katika mapendekezo ilikuwa issue ya habari na propaganda.

Kwamba hadi sasa hawajaukana hadharani uzi huu wa ndugu Uzima Tele, ni jambo la kushangaza sana.

Haya sidhani kuwa ni mawazo ya Chadema bali ya chawa tena wasiojitambua.

Kwa hakika ukombozi si Kwa njia hii Chadema wanaonekana kuchukua.

Bila kutambua kuwa hakuna adui wala rafiki wa kudumu bali agenda, hakuna mafanikio hapo.

Ninakubaliana na list hii:

TEC, Mbarikiwa, Lissu, Dr Slaa, Mwabukusi, Madeleka, Mdude, Dr Nshalla , Mwamakula, nk nk ndo wanabeba agenda za wananchi Kwa vitendo.

Nikurekebishe hapa: Kina Bashiru na Ndugai na wa namma hiyo inabidi wajitokeze wazi wazi huku tujiridhishe zaidi.

Ni kweli kuwa hata wao si haba.
Ndugu brazaj unataka CHADEMA waje kukana au ku - clarify nini kwenye hiki nilichokipost mimi?

Haya ni mawazo na mtazamo wangu binafsi msingi wake ukiwa ni mjadala unaoendelea katika jamii juu ya kikundi hiki kinachoitwa Sauti ya Watanzania kilichoibuka ghafla na kuivamia CHADEMA..

Mimi si mwanachama wa CHADEMA. Mimi ni mwananchi tu niliyeko huku kwetu Shinganga na ni mpenzi sana na huwa nakiunga mkono CHADEMA ktk harakati zake za kisiasa..

Hawanijui wala Mimi simjui kiongozi yeyote wa CHADEMA, hata wa tawi tu achilia mbali wa kitaifa au mkoa..
 
CDM ndio inasaliti watz ktk HOJA ya Bandari Kwa kuipeleka kwenye mikutano ya hadhara Badala ya kuongoza maandamano yasiyo na kikomo wakiungana na watz, sauti ya watz,Hadi Bandari zetu na maliasili zetu ziheshimiwe na Watawala.
Wewe huwezi kuandamana? Unasubr uongozwe na CHADEMA?
 
Ndugu brazaj unataka CHADEMA waje kukana au ku - clarify nini kwenye hiki nilichokipost mimi?

Haya ni mawazo na mtazamo wangu binafsi msingi wake ukiwa ni mjadala unaoendelea katika jamii juu ya kikundi hiki kinachoitwa Sauti ya Watanzania kilichoibuka ghafla na kuivamia CHADEMA..

Mimi si mwanachama wa CHADEMA. Mimi ni mwananchi tu niliyeko huku kwetu Shinganga na ni mpenzi sana na huwa nakiunga mkono CHADEMA ktk harakati zake za kisiasa..

Hawanijui wala Mimi simjui kiongozi yeyote wa CHADEMA, hata wa tawi tu achilia mbali wa kitaifa au mkoa..

Kumbe wala si mwanachama halafu kwa kujua au kutojua umeandika ugolo huo?

Ushauri wangu Chadema kwa watu kama wewe ni huu hapa:

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

Nitawashangaa mno wasipokutolea uvivu na bila kuchelewa.

Ninyi ni ma CCM au vibaraka wao kwa kujua au kutokujua.

Si mbaya kujua, hatudanganyiki!
 
Kumbe wala si mwanachama halafu kwa kujua au kutojua umeandika ugolo huo?

Ushauri wangu kwa watu kama wewe ni huu hapa:

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

Nitawashangaa mno wasipokutolea uvivu na bila kuchelewa.

Ninyi ni ma CCM au vibaraka wao kwa kujua au kutokumjua.

Si mbaya kujua, hatudanganyiki!
Yes, you are right...

Mimi siyo mwanachama wa CHADEMA. Lakini ni shabiki na mpenzi wa chama hiki. Ndicho ninachokiamini kuliko vingine vyote..

Kama nilichokiandika ni ugolo kwako, it's ok. Ni hiari yako uone ugolo au buskuti. Ila nafurahi umeusoma ugolo na hulali Kila siku inachangiwa..

By the way, kwani ili kuandika kuihusu CHADEMA ni lazima uwe mwanachama? Wewe brazaj ndiyo unajua hivi siyo??
 
Ni kweli ugolo wote nimeusoma na ndiyo maana wote nimeujibu.

Kwamba wewe si mwanachama ninakuona zaidi hapa:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Tunawajua nyie kuwa mnaandika ugolo tena sana. Tena hata mambo ya kijinga tu, kutafuta mifarakano kama itapatikana.

"Tunajua mko tayari hata kujaribu kutega kunguru hata kwa maharage makavu kama itawasaidia."

Habari mbaya mno kwenu ni kuwa:

Hatudanganyiki!
 
Unajuaje kuwa Sauti ya Watanzania si huyu shetani aliyejigeuza kuwa malaika wa nuru? Ni kwa kuwa tu wanazungumza lugha kama yenu?........ Oooh, utaliwa mchana kweupe!!!
Hizi makala zako ndefu zinasisitiza tu kuwa wewe tayari uko kazini kuponda kundi moja na kukingia kifua kundi jingine.
Huna 'objectivity' tena katika maandishi yako.

Ndiyo maana nikasema toka kule mwanzo kwenye ile mada nyingine, kwamba huenda tayari uko ndani ya kibarua kinachotokana na fedha za waarabu zinazotumika kwenye kampeni ya kutuwekea serikali wanayoitaka wao.
 
Kama huyo nimelazimika kuandika uzi huu:

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

Pana haja ya kuwa nao makini.
 
Hizi makala zako ndefu zinasisitiza tu kuwa wewe tayari uko kazini kuponda kundi moja na kukingia kifua kundi jingine.
Huna 'objectivity' tena katika maandishi yako.
Narudia tena, hayo ni maoni na mtazamo wangu binafsi kwa kinachoendelea ktk jamii na kuzua mjadala nami nashiriki mjadala huu kama tu wewe unavyoshiriki..

Sijalazimisha mtu (ukiwemo wewe) kukubaliana nami au kuona sawa na nionavyo mimi. Kila mtu ana mawazo na mtazamo wake juu ya jambo lolote likiwemo hili. Huu ndio unaoitwa "uhuru wa mawazo" kama ulikuwa hujui..
Ndiyo maana nikasema toka kule mwanzo kwenye ile mada nyingine, kwamba huenda tayari uko ndani ya kibarua kinachotokana na fedha za waarabu zinazotumika kwenye kampeni ya kutuwekea serikali wanayoitaka wao.
You're absolutely wrong. Fikra zako hizi ni batili..

Je, ni kwa sababu tu nimetillia shaka kikundi kinachoitwa "Sauti ya Watanzania?" kwenye harakati za kulikomboa taifa toka kwenye makucha ya wakoloni weuzi, CCM..?

Kama wewe unawaamini, basi jenga hoja kutushawishi na sisi wengine tusiowaamini tuwaamini. Lakini ni utoto na pengine ujinga kudhani kila mtu anayewatilia shaka, basi kahongwa...

Na kama ni ishu ya kuhongwa, basi mimi nikiri mbele yako sasa kuwa nimehongwa na CHADEMA kwa kuwa nawatetea..

Na hongo yao kwangu ni hii....👉👉👉👉 Nawaamini, nawajua na kuelewa misimamo yao na wanachokipigania katika nchi yangu...

Kwa hiyo, kila hatari ya hujuma inayoweza kuwa mbele yao, ni lazima kupiga kelele kama tulivyofanya miaka yote kukilinda chama hiki tegemeo la wanamapinduzi wengi.!
 
Sijalazimisha mtu (ukiwemo wewe) kukubaliana nami au kuona sawa na nionavyo mimi. Kila mtu ana mawazo na mtazamo wake juu ya jambo lolote likiwemo hili. Huu ndio unaoitwa "uhuru wa mawazo" kama ulikuwa hujui..
EEEeeenHeeeee!
Nilikuwa sijui mkuu 'Uzima', asante kwa kunistua kuhusu hili.

Kwa hiyo umeona popote nikizuia uhuru wako wa maoni; au kwa vile nami nimekataa maoni yako, basi sina ruhusa ya kufanya hivyo.
 
Na hongo yao kwangu ni hii....👉👉👉👉 Nawaamini, nawajua na kuelewa misimamo yao na wanachokipigania katika nchi yangu...

Kwa hiyo, kila hatari ya hujuma inayoweza kuwa mbele yao, ni lazima kupiga kelele kama tulivyofanya miaka yote kukilinda chama hiki tegemeo la wanamapinduzi wengi.!
Unapigania hao hao unaowaita "wakoloni weusi, CCM", na hiyo kama ulivyosema mwenyewe, ni haki yako.
Wewe ni sehemu ya mkanganyiko mkubwa unaoendelea ndani ya chama hicho cha CHADEMA.
Hili kundi lenu likifanikiwa kukisalimisha kwa CCM ya Samia, Mwenyekiti Mbowe atakuwa kamaliza kazi yake muhimu.
 
Wewe ni sehemu ya mkanganyiko mkubwa unaoendelea ndani ya chama hicho cha CHADEMA.
Hoja yako ni nini hasa?
Hili kundi lenu likifanikiwa kukisalimisha kwa CCM ya Samia, Mwenyekiti Mbowe atakuwa kamaliza kazi yake muhimu.
Ndivyo unavyodhani siyo?

Yaani ni kuwa;

✓ Una macho, lakini huoni...

✓ Una masikio, lakini husikii...

✓ Kikubwa zaidi ni kuwa, kwa kuwa hujajaliwa yote hayo basi hata kuelewa huwezi kuelewa..!!

##Kwani hii story ya CHADEMA itakufa au imeuzwa, umezianzisha wewe leo kuisema? Ni zaidi ya miaka 30 lakini jamaa wapo..!!

##Unajisumbua bure. Ni kwamba, waambie Sauti ya Watanzania warudi mezani wapange mambo yao vyema, na kama wanataka kutumia jukwaa la CHADEMA kama mshirika wao, basi wana kazi ya ziada kujenga trust kwao na kwa wananchi. Kanuni kuu ya ushirika wowote ni TRUST..
 
Dah!

Mkuu 'Uzima'', utahangaika sana na mada hii lakini najua hutafika popote.
Mbowe kishakengeuka na wakati wa kuimaliza CHADEMA ndio huu sasa kama ataendelea kukaza shingo.

Wewe hukuanza kunifundisha habari za CHADEMA, ninazifahamu barabara, na hapa inakoelekea tena ghafla tu baada ya Samia na Mbowe kula yamini, sioni hicho chama kikienda popote zaidi ya hapo kitakapokuwa kimefikia.
Nilikwisjha sema zamani humu maneno "Mbowe Kwisha" baada ya kumsikiliza kwenye hotuba yake iliyosemwa kwamba aliitoa kwa Diaspora huko ughaibuni. Sibadili chochote juu ya hilo, kama sasa atakuwa amefanikiwa kuwalaghai wale waliokuwa hawaoni aliyoyaona yeye na Samia.

Kwa hiyo wewe hapo huna lolote jipya la kunifundisha juu ya hicho chama chini ya Mbowe.
Alichofanikiwa kufanya Mbowe, ni kukisalimisha chama wakati mgumu wa Maghufuli; lakini sasa kayeyuka kama barafu mbele ya Samia.
 
Mbowe na genge lake hawawezi kuungana na watu wenye nia ya kweli ya kuitoa CCM madarakani. Chadema hawahawa walikua busy kupambana na kundi la Hayati Magufuli. Hili ni kundi muhimu sana kwao na ni mtaji wa kisiasa kuitoa CCM madarakani ila wao walikua busy kulipiga vita. Sio bahati mbaya, Huu ni mkakati wa CCM kuhakikisha wanatugawa ili waendelee kututawala na moja ya masharti waliyopewa Chadema ni kuwa mbali na sukuma gang na aina yoyote ya watu wenye kutishia kuitoa CCM madarakani. Now wako busy kupambana na sauti ya watanzania, sio bahati mbaya. Hii ni mikakati ya CCM wakiwatumia akina Mbowe na genge lake. Hizi operation wanazofanya akina Mbowe hazina madhara yoyote kwa CCM na ndio maana hawapigwi pin. Kila linapotokea jambo Zito kwa CCM basi Mbowe hutumika kuzima moto kwa akili nyingi sana. Mbowe ndiye aliyetumika kuzima operation UKUTA na ni Mbowe ametumika kuzima Vuguvugu la bandari kwa kuja na operation zake Uchwara. Niulize tu toka wameanza hizo operation mmesikia utawala ukitikisika hata nywele?
Chadema na Mbowe wanapambana vipi na hiyo Sauti ya Watanzania? Hivi hao wakina Slaa walishirikiana na Chadema kupanga hayo maandamano? Aidha, hivi kwa nini wanaamini kuwa bila Chadema kuungana nao hawatafika mbali? Mbowe amesema kuwa wao wana ratiba yao na wataendelea nazo. Na kuwa hana shida na wanachadema kushirikiana na Sauti ya Watanzania ila kichama wataendelea na ratiba yao. Kwa nini hiyo Sauti ya Watanzania wasijipange ku complement hiyo mipango ya Chadema? Kweli wanataka waache kila kitu wawafuate wao? Kweli stupid as stupid does.

Amandla...
 
Mnajitahidi sana kuwachonganisha Lissu na Mbowe na hamtafanikiwa. Lissu atapingaje maridhiano yaliyopelekea mikutano ya hadhara kuruhusiwa na kupewa ulinzi wa polisi? Acheni hayo.

Amandla....
Jamaa anajichanganya,Mbowe ni mnafiki na anapiga Hela ya serikali vizuri sana kupitia kujipendekeza kwa Samia na viongozi wa CHADEMA top brass ukimuondoa Lissu wote wanawaza Ubunge 2025 na wanaona wakimuuzi Samia watakosa kitumbua.
CCM ikibanwa kwenye Kona Mbowe utamuona anarudi nyuma badala ya kuchochea zaidi mapambano.Wale wakina Heche,Msigwa,Mnyika et al wanaogopa kupingana na Mbowe simply wanajua watakosa mkate.Lissu peke yake ndiyo mara nyingine anapingana na misimamo ya Mbowe hasa kwenye Maridhiano na CCM!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom