"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....

Hatuwezi kuelewana kama tatizo la msingi kwa CHADEMA tunalitazama tofauti; hii ndiyo shida kati yetu, wewe na mimi.
Ni lipi hili specific?
Nimekwishaeleza sana, hofu yangu juu ya CHADEMA inayopelekwa kwa Samia na Mwenyekiti Mbowe; wewe hili si tatizo kwa upande wako.
CHADEMA inapelewakwaje Kwa Samia. Fafanua..

Utamkwepaje huyu maana kwa sasa ndiye Rais na mkuu wa nchi?

Kama kuna mambo tunahitaji, huwezi kumkwepa. Ni lazima ukutane na kuzungumza naye tu!
Sasa unataka nikubaliane tu na wewe kwamba sioni tatizo lolote?
Categorically, ni lipi hilo? CHADEMA kuzungumza na CCM? Ni kwa vipi ni tatizo?
Wewe umeona tatizo la akina Mwambukusi kuwa vibaraka wa CCM, sijui CCM ipi hiyo;
Ndiyo nilitahadharisha japo wewe unaiona tahadhari kwa jicho la "kuponda". Hata hivyo, it's ok, sikuhukumu...

Tatizo lao na CHADEMA linaweza kuwa corrected. Nimesema hili several times. Kwamba ishu kati Yao ni ZERO TRUST, yaani kutoaminiana...

Solution ni kujenga mazingira ya kuaminiana tu. Kuna ubaya kuwa na mtazamo huu?
lakini uaamini kwa vile baadhi yao walishaonyesha kuwa watu wasioaminika, hiyo inatosha kabisa kuwasuta na kuwakataa
Temporarily, unawasuta na kuwakemea. ZERO TRUST ikishakuwa settled, maisha yanaendelea, tunapiga kazi pamoja...
hata katika yale yanayoonekana wazi ni ya kuwapinga CCM hao hao.
Hapa ndipo ilipo shida yako!

Siyo kila anayeimba wimbo unaofanana na unaoimba wewe ni mwenzio...!
Hii ni tofauti kati yako na mimi. Mimi nitawaamini hawa kwa haya wanayoyafanya sasa, na nitawaunga mkono.
It's ok. No crime at all...
 
Tufike mahali tuseme "IMETOSHA", maanake sasa tunazungushana mlle mle tulimoanzia. Hatupiga hatua yoyote na wala hatuongezi jipya.

Nitaendelea kuwaunga mkono CHADEMA, kwa dhumuni moja tu kwa sasa; kama watasimama kidete na kuwa na lengo la dhati la kuwaondoa CCM madarakani, nje ya lengo hilo sioni tofauti yao na CCM ya Samia. Na kama bado hunielewi juu ya hili, huko ndiko roho ya Mwenyekiti Mbowe ilikolalia zaidi, na kutufanya wengine tuwe na mashaka juu yake na hizi chenga chenga nyingi za wakati huu ndani ya chama hicho.

Huwezi kuwa na "ZERO TRUST" kwa mtu au kundi, halafu useme utafanya kazi na kundi hilo. Hii ndiyo hukumu ya kifo uliyokwishatoa wewe juu ya watu hao.
Ikiwa umekwisha wanyonga, utawapata wapi tena ili ushirikiane nao?

Ngoja nijaribu tena kukufahamisha kwa kifupi juu ya CCM, ambayo sote tunaiimba humu kuwa ndiye shetani mkubwa kabisa ndani ya nchi yetu kwa sasa hivi.

CCM inazo sura nyingi inazozitumia kila mara, kutokana na nani kashika kiti cha hapo juu, cha Mwenyekiti wa chama.

CCM hii iliyopo sasa chini ya Samia, siyo CCM iliyokuwa ikiwasurubu akina Mbowe chini ya Magufuli. Kisichobadilika ndani ya chama hicho ni kuwa na nia ya kuachia madaraka, kwa kutumia mbinu zote hadi zile haramu kubaki madarakani. Tatizo hili, sisi wengine ndilo la msingi kabisa linalotufanya kukataa aina zote za CCM zinazojitokeza, bila uwepo wa mabadiliko ya msingi.
CCM ya Samia inayo mambo mengi sana inayoweza kushirikiana na CHADEMA ya Mbowe; na hapa ndipo panapoanzia Mbowe aone ni bora kufanya kazi na CCM hii, na kusahau tatizo la msingi, la kuiondoa moja kwa moja CCM madarakani.

Umekwishasema mwenyewe kwamba, upo tayari kushirikiana na mtu/kundi ambalo tayari ulikwishatangaza "ZERO TRUST", juu yake. Sasa sioni ajabu utakapogeuka na kuja hapa kutetea Mbowe kuisalimisha CHADEMA kwa CCM ya Samia, ambayo ilikwishajiapiza yenyewe, kuwa itakuwa madarakani milele!

Imetosha. Tugange mengine.
 
Huwezi kuwa na "ZERO TRUST" kwa mtu au kundi, halafu useme utafanya kazi na kundi hilo. Hii ndiyo hukumu ya kifo uliyokwishatoa wewe juu ya watu hao.
Ikiwa umekwisha wanyonga, utawapata wapi tena ili ushirikiane nao?
Ndugu Kalamu "Zero Trust" ni kama kipimamwendo ktk gari (Speed Meter). Gari kama haiko ktk mwendo, obvious Speed Meter itasoma "zero". Ikianza kitembea itaanza kusoma ikipandisha alama kulingana na kanimwendo inayotumika kuifanya gari itembee..

Ndivyo ilivyo kwetu sisi binadamu. Naweza nisikuamini leo kwa kiwango cha "zero" kabisa kwa sababu fulani fulani. Lakini kumbuka kuwa binadamu ni kiumbe kinachobadilika kila wakati kitabia na mwenendo hadi kufikia kwenye "normal".

By the way, kama watu wana mashaka nawe ndani ya ushirika au kukukaribisha ktk ushirika wao, then, it's your responsibility to show them that they don't need to doubt you..

Kwa hiyo basi, Zero Trust inaweza kupandishwa au inaweza kubaki hivyo kama anayehusika hatafanya juhudi kufanya aaminike Kwa wengine...

Waambie Sauti ya Watanzania waseme ni kwanini wanadhani wanaweza kuaminiwa na wenzao. That's all; nothing more, nothing less..

Na mashaka ya mwenzako dhidi ya kitu fulani au mtu fulani hakuna mwenye haki ya kuanza kuyahoji au kuanza kulazimisha watu wakuamini tu.

Hii haipo kwa sababu, this is absolutely natural human instinct..
Imetosha. Tugange mengine.
Haijatosha na haitatosha.

Ukijaribu kuganga la kesho, utashangaa kulikuta hilihili la leo huko mbele. Kwa hiyo maliza biashara sasa, kesho siyo yako na inaweza isiwepo kabisa..!!

Wakomavu ktk mijadala hutumia kutumia kiswahili hiki kupumzika ktk mjadala: TUKUBALIANE KATIKA KUTOKUKUBALIANA
 
Wakomavu ktk mijadala hutumia kutumia kiswahili hiki kupumzika ktk mjadala: TUKUBALIANE KATIKA KUTOKUKUBALIANA
Huko ndiko ninakokuita "Imetosha". Wewe lipe hilo jina unalotaka kuliita; haibadili kitu.
 
Mimi naamini kuwa Chadema wanawahitaji zaidi akina Mwabukuzi kuliko akina Mwabukuzi wanavyowahitaji Chadema.Kwa hiyo,Chadema hawakuwa sahihi kukataa ushirikiano na akina Mwabukuzi.
Kibri kile kile cha hicho chama kujion wao ni mAlaika na hawakosei
 
Nawe sauti yako ni ya kufanya nini wadanganyika
 
Mpaka sasa Sauti ya Watanzania ndiyo watetezi wa kweli wa madhila yanayowapata Watanganyika, hao wengine wako busy na kusuguana kuhusu Uchaguzi wa 2024 na 2025 maana nikiangalia mwenendo wa harakati hizi Tayari Sauti ya Watanzania imeisha weka point moja kubwa Mkononi ya ya kuzuia umilikishwaji wa rasilimali za nchi, uhuni uliotaka kupitishwa Bungeni, Tatizo sisi Watanganyika bado hatujajitambua na hatujui tunataka nini Issue ya Bandari chadema wanaisemea midomoni tu lakini Mioyoni wapo na CCM. Huo wimbo wa Katiba mpya sasahivi umeisha chuja Ulianza toka vyama vingi vilipoanzishwa, zikifika nyakati karibu na uchaguzi ndiyo wanashtua ili kuwavuruga Watanganyika wawe busy na malumbano ya Katiba Ili wao wafanye mambo yao kiulaini kwa kisingizio cha maridhianao.
 
Nimesoma
Nitaendelea kusoma kwa kutulia zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…