"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....

Dah!

Mkuu 'Uzima'', utahangaika sana na mada hii lakini najua hutafika popote.
Kufika popote wapi? Kwani nimekwambia mimi nakwenda wapi hata ujue sitafika huko "popote" ninakokwenda?

After all, hii isingekuwa hoja kweli, badi usingekuwa unahangaika kujibizana nami. Ungeniouuza tu na labda, sasa ungekuwa umelala...
Mbowe kishakengeuka na wakati wa kuimaliza CHADEMA ndio huu sasa kama ataendelea kukaza shingo.
Anaimalizaje maana ipo na mpaka hao Sauti ya Watanzania wanatafuta "collabo" na hawahawa CHADEMA unaosema wanaisha?

NOTE
Honestly, mimi sikuelewi. Na kwani wewe unatetea nini hasa? Kwa mbali naona kama tunatetea kitu kilekile lakini ktk lugha na mitazamo tofauti, au nakosea?

Mtazamo wangu ni huu: Tunawahitaji CHADEMA sana ktk siasa za ushindani za Tanzania...

Muhimu ni kuwa wanapaswa kuwa waangalifu wasijepitia njia iliyopitia CUF au NCCR Mageuzi. Ndiyo mantiki ya maoni na mtazamo wangu ktk thread hii..

Unaweza kuyakosoa au ukayaboresha au ukaya - ignore kabisa.

Lakini kwa hili [msimamo wao kuweka tahadhari ya namna ya kwenda na kikundi hiki cha Sauti ya Watanzania] Freeman Mbowe na wenzake wako kwenye right track na CHADEMA...
 
Kufika popote wapi? Kwani nimekwambia mimi nakwenda wapi hata ujue sitafika huko "popote" ninakokwenda?
Jinsi unavyowasilisha maoni katika mada hii inaonyesha kuna mahali unakwenda, huko ndiko ninakokusema. Unapajua mwenyewe, siyo lazima utaueleze sisi.
 
Chadema na Mbowe wanapambana vipi na hiyo Sauti ya Watanzania? Hivi hao wakina Slaa walishirikiana na Chadema kupanga hayo maandamano? Aidha, hivi kwa nini wanaamini kuwa bila Chadema kuungana nao hawatafika mbali? Mbowe amesema kuwa wao wana ratiba yao na wataendelea nazo. Na kuwa hana shida na wanachadema kushirikiana na Sauti ya Watanzania ila kichama wataendelea na ratiba yao. Kwa nini hiyo Sauti ya Watanzania wasijipange ku complement hiyo mipango ya Chadema? Kweli wanataka waache kila kitu wawafuate wao? Kweli stupid as stupid does.

Amandla...
You never know. Pengine hawa kina MISULI na huyu Kalamu na brazaj ndio hawa Sauti ya Watanzania wenyewe
 
After all, hii isingekuwa hoja kweli, badi usingekuwa unahangaika kujibizana nami. Ungeniouuza tu na labda, sasa ungekuwa umelala...
Mimi unanilazimisha kukujibu, kila mara unapoweka mambo yako katika 'quote' ya niliyoandika mimi. Binafsi sina la ziada la kueleza kuhusu mada yako hii, kwa sababu nilishajieleza toka mwanzo.
 
Jinsi unavyowasilisha maoni katika mada hii inaonyesha kuna mahali unakwenda, huko ndiko ninakokusema. Unapajua mwenyewe, siyo lazima utaueleze sisi.
Ni maoni yangu tu..

Ninakokwenda ni kuiona CHADEMA inadumu ktk siasa za ushindani za Tanzania na ikibidi washinde chaguzi na kuchukua nchi hii ili tuwaone nao wataifanyia nini nchi hii..

Na kingine ni kuhakikisha tunapambana na "distraction agent" yeyote inayoweza kusimama njiani kuzuia harakati hizi Kila mtu Kwa namna na Kwa njia anayoweza na inayofaa..

Wewe kama unamwona Freeman Mbowe na viongozi wenzake wanakwenda uelekeo usio sahihi, basi kemea, onya na toa ushauri... Usiwe mtu wa kulaumu tu ukisahau kuwa kina Freeman Mbowe, Tundu Lissu na viongozi wenzao nao ni binadamu tu ambao wanaweza kukosea pia..
 
Honestly, mimi sikuelewi. Na kwani wewe unatetea nini hasa? Kwa mbali naona kama tunatetea kitu kilekile lakini ktk lugha na mitazamo tofauti, au nakosea?

Mtazamo wangu ni huu: Tunawahitaji CHADEMA sana ktk siasa za ushindani za Tanzania...
Maajabu ndiyo haya sasa.

Yaani imekuchukua muda wote huu kutambua kwamba inawezekana tukawa tunatetea jambo lilelile?

Hukumbuki kabisa nilichokueleza katika bandiko langu la kwanza au la pili kuhusu hili jambo?

Nilisema, heshima ya Dr Slaa aliivuruga yeye mwenyewe katika matamshi yake mbalimbali aliyofanya baada ya kuondoka CHADEMA; nikakueleza pia kwamba, siyo lazima CHADEMA na kundi hilo watofautiane kwa kila jambo, ni lazima kuna mambo wanayoweza kukubaliana kati yao; kwa hiyo hili lisiwe jambo la kung'ang'ania sana kwamba kundi hilo ni mpango wa CCM kama unavyong'ang'ania wewe.
Na hapo hapo nikakutahadharisha kuhusu mbinu anazotumia Samia kumnasa Mbowe; lakini huelewi kitu!
Sasa tena unakubali hapa mwenyewe kwamba inawezekana tupo pamoja?

Binafsi, msimamo wangu juu ya CHADEMA unafahamika vizuri, kwa sababu kila mara ninaueleza humu.
CHADEMA ndiyo chama pekee cha upinzani ambacho tayari kilishaonyesha dalili za kuiangusha CCM. Hili pekee kwangu linatosha kuwaunga mkono CHADEMA bila hata kuangalia sera zao zikoje huko wakishafanikiwa kuondoa hawa CCM ambao sasa wanafanya kila mbinu ya kutotaka kutoka madarakani.
Kipaumbele kwangu ni kuwaondoa CCM, yeyote anayeweza kufanya hivyo nitamuunga mkono.
Na nilisha eleza humu, kwa nini Mbowe kwa msimamo wake baada ya kutoka mahabusu unahatarisha adhma hiyo ya kuiondoa CCM madarakani, hadi mada nikaianzisha juu yake. Halafu sasa wewe unakuja na hii habari ya mada inayoonyesha wazi mwelekeo wa kuondoa matumaini ya waTanzania, unataka tufurahie hilo?
 
Ninakokwenda ni kuiona CHADEMA inadumu ktk siasa za ushindani za Tanzania na ikibidi washinde chaguzi na kuchukua nchi hii ili tuwaone nao wataifanyia nini nchi hii..
Kwa hiyo inawezekana tofauti yetu kubwa ipo hapa.
Mimi nawaunga mkono CHADEMA wawaondoe hapo walipo CCM. Hicho ndicho kipaumbele kwangu. Matumaini ya inapokwenda CHADEMA baada ya hapo, ni hayo watakayofanya wakiwa madarakani.
Kama waTanzania hawayataki, wawaondoe kabla na wao hawajaota pembe kama wanazotuburuza nao CCM miaka yote hii.

Hii nadhani ni tofauti kubwa kati yetu, mimi na wewe.
Na kwa kujua hivyo, nadhani ndiyo maana hunielewi ninaposema Samia na Mbowe wanalo jambo kati yao. Hili ni fumbo usilolitilia maanani wewe; lakini kwangu ni jambo kubwa kabisa.
 
Hoja yako ni nini hasa?

Ndivyo unavyodhani siyo?

Yaani ni kuwa;

✓ Una macho, lakini huoni...

✓ Una masikio, lakini husikii...

✓ Kikubwa zaidi ni kuwa, kwa kuwa hujajaliwa yote hayo basi hata kuelewa huwezi kuelewa..!!

##Kwani hii story ya CHADEMA itakufa au imeuzwa, umezianzisha wewe leo kuisema? Ni zaidi ya miaka 30 lakini jamaa wapo..!!

##Unajisumbua bure. Ni kwamba, waambie Sauti ya Watanzania warudi mezani wapange mambo yao vyema, na kama wanataka kutumia jukwaa la CHADEMA kama mshirika wao, basi wana kazi ya ziada kujenga trust kwao na kwa wananchi. Kanuni kuu ya ushirika wowote ni TRUST..
Hiyo trust mnayoitaka mbona kwa lowas mlienda haraka haraka au kwa kuwa alitoa mpunga wa maana
 
You never know. Pengine hawa kina MISULI na huyu Kalamu na brazaj ndio hawa Sauti ya Watanzania wenyewe

Uchawa Kwa maana yake kamili ni kukosa uwezo wa kusimamia maoni yako kama binadamu wa kawaida tu. Wengine wakisema ni kama kushikiwa akili na mtu mwingine.

Machi 21, 2023 huko, niliandika uzi huu:

Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

Kabla mno ya hoja za kina Mwabukusi na wenzao leo.

Kwamba Leo ninasema hivi:

Kwanini Wakili Mwabukusi na wenzake wanastahili kuungwa mkono

Nikiwa nimesimama kama kidume cha mbegu, ambao ndiyo msimamo wa kina Mwabukusi na wenziwe leo, labda basi kama wao ni chawa wangu?

Nisiache kusema hapa. ninashawishika kukupuuza. kujibizana na poyoyo kama wewe kwa hakika ni kukupa mileage bure.

Wewe endelea na mabandiko yako ugolo. Ila kwa hakika, yanatia aibu.

Hivi hata hujihurumii ndugu?
 
Chadema na Mbowe wanapambana vipi na hiyo Sauti ya Watanzania? Hivi hao wakina Slaa walishirikiana na Chadema kupanga hayo maandamano? Aidha, hivi kwa nini wanaamini kuwa bila Chadema kuungana nao hawatafika mbali? Mbowe amesema kuwa wao wana ratiba yao na wataendelea nazo. Na kuwa hana shida na wanachadema kushirikiana na Sauti ya Watanzania ila kichama wataendelea na ratiba yao. Kwa nini hiyo Sauti ya Watanzania wasijipange ku complement hiyo mipango ya Chadema? Kweli wanataka waache kila kitu wawafuate wao? Kweli stupid as stupid does.

Amandla...
Mkuu chama chochote cha SIASA kilicho serious huwa busy kutumia vikundi au watu wowote wanaoonekana ni mtaji kwao kisiasa. Sauti ya watanzania ulikua mtaji wa kisiasa kwa Chadema lkn kwakua Chadema wanatumika ndio maana unasikia hizi porojo. Tumeona CCM wakitumia bodaboda na makundi mengine wanayoona yanaweza kuwaongezea kura na ushawishi. Chadema ilitakiwa iwafuate na iwatumie sauti ya watanzania na sio sauti ya watanzania iwafuate Chadema na kuwaomba. Kuna kundi la sukuma gang, unaona ni jinsi gani CCM inataka ilimeze na kujihakikishia ushindi, Chadema pia ilitakiwa hili kundi waliteke pia kuongeza ushawishi na kuivuruga CCM ila kwakua hiki ni chama ni genge la wahuni liko busy kupambana nalo,ndio maana tunasema ukiwa smart kichwani utakubali kuwa Chadema inatumika na CCM kuhakikisha wanatawala milele
 
Utangulizi

Political propaganda ni taaluma kama taaluma zingine. Inapofanyika kwa umakini huleta matokeo. Lakini inapofanyika unprofessionally kama UWT wanavyofanya hapa kwa kuwatumia hawa wanaoitwa Sauti ya Watanzania kama nitakavyoonesha hapa, inamharibia kabisa badala kumjenga anayefanyiwa propaganda hiyo iwe mtu au taasisi au chama cha siasa..

Asikudanganye mtu. Amsha amsha ya , Operesheni na mikutano ya CHADEMA ya kuelemisha wananchi iliyopewa jina la +255, KATIBA MPYA, OKOA BANDARI ZETU iliyokuwa inahudhuriwa na maelfu ya wananchi kwa hiari yao iwe jua au mvua katika mikoa ya Katavi, Kigoma, Tabora, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara imewatia hofu CCM na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na kuwafanya walale vitandani na viatu...

Ilikuwa ni lazima waje na plan kabambe ili ku - neutralize mambo. Fuatana nami ktk uchambuzi huu..

Sauti ya Watanzania na agenda ya katiba mpya na mkataba wa bandari. Are they real?
Mtu asipokuwa makini anaweza kudhani ni wapinzani kweli dhidi ya sera na mipango ya CCM na serikali yao na wanatetea hii kitu. Ni uongo mtupu, ni kinyume chake kabisa. Hawa ni nyoka hatari ndani ya vazi la wakosoaji na wapinzani wa CCM..

Wanatumia agenda zilezile zilizobebwa na CHADEMA yaani Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, mkataba wa bandari kama ndoano tu ya kunasia samaki [CHADEMA] huku wakiuficha unyoka wao...

CHADEMA waliliona hili. Hawakufanya makosa kuwashitukia. Hongereni CHADEMA, mmejiokoa..

Igizo la Kukamatwa kwa Dr Wilbroad Slaa, Wakili Boniface Mwambukusi na Mdude Nyangali na kesi yao ya uhaini

Utadhani ni kweli. Lakini huo ulikuwa mwanzo na sehemu ya igizo la filamu yenyewe chini ya uratibu wa hovyo wa TISS ya CCM.

Kama kuna anayebisha, asubiri aone kama kuna kesi yoyote itaendelea na mtu asije akashangaa kwa baadhi ya wana Sauti ya Watanzania wakalamba teuzi mbalimbali iwapo watafanikiwa kuifanya kazi yao vyema..

Hizi kelele za mng'ako wa members wa kundi hili tunazozishuhudia sasa ni taharuki baada ya kuona mpango wao umeshindwa..

Just try to think. Kesi inaanza kama uhaini. Hakuna dhamana hapo. Ghafla ikabadilika na kuwa uchochezi. Watu wakatoka kifungoni. Waliowakamata wala hawakujali kinga ya kibalozi ya Dr Wilbroad Slaa. Anatoka ndo wanakumbuka kuiondoa hiyo kinga ili acheze hiyo filamu vyema na kwa uhuru usio na maswali..

Je, TISS wanahusika kwenye mkakati huu?

Absolutely Yes, 100%.!!

Ushahidi wa kimazingira unathibitisha hili. "Sauti ya Watanzania" ni strategy ya TISS kuzima nguvu ya CHADEMA. Iko mikakati mingi ya gizani na ya wazi. Huu ulikuwa wa wazi lakini ulioandaliwa kishamba sana na kumpa kazi hii Dr Wilbroad Slaa mzee wa miaka almost 77 labda wakidhani anaijua CHADEMA na viongozi wake. Na anadhani CHADEMA ya sasa ni sawa na ile ya mwaka 2015. Amekosea..!

Masikini baadhi ya vijana wa vyama vya siasa hususani toka CHADEMA na vyama vingine wameingizwa humo kwa kujua au bila wao kujua..

Na kwa ustadi wa hovyo sana and unceremoniously wakajaribu kuivuta CHADEMA yote ishiriki kwenye mkakati wao. Thank God, wameshindwa...

CHADEMA wakauona mtego huo, wamekataa. Sauti ya Watanzania wakang'aka kwamba wametengwa na CHADEMA. Wakarusha kila aina ya shutuma. Wakasema ooh, hawa CHADEMA wanajidai kupigania maslahi ya nchi kumbe wana maslahi yao..

Msimamo wa CHADEMA uliotolewa na Mwenyekiti wao Mh. Freeman Mbowe ni simple and very clear...

Lakini jamaa hawa wanajifanya kutoelewa kabisa. Bila shaka ni wajinga hawa. Haraka haraka wameigeuza vita hii kuwa ya Freeman Mbowe personally. Wanatumia kanuni ya "mpige mchungaji, kondoo watawanyike". Wenye akili wameliona hili na wanawashangaa..

Hebu take time na sikiliza kipande cha hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kilichowakwaza hawa jamaa hapa👇👇
View attachment 2773537

Hebu mtu makini aniambie, hatuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA mpaka hapo ina shida gani hata hawa watu wakasirike kiasi hiki?

Kuhusu Dr Wilbroad Slaa kurudi CHADEMA iwapo alishatambua na kujutia kosa lake la mwaka 2015 Mwenyekiti alishamfungulia mlango siku nyingi. Msikilize👇👇
View attachment 2773562
Lakini cha ajabu huyu Mzee anatumia hila kurudi kwa mlango wa nyuma na nia yake ni kumaliza kazi aliyoshindwa kuifanya vyema mwaka 2015...

Siku 30 alizotoa Mdude Nyangali zimeisha?

Ndiyo. Mpaka jana sauti ya Watanzania walikuwa Mwanza kuanza maandamano yasiyo na ukomo. Waliendelea kujifunua na kueleweka kirahisi sana...

Kilichotokea Mwanza

Hatimaye siku 30 walizompa ndugu yao Samia Suluhu Hassan serikali zinaisha. Sauti ya Watanzania wakaenda Mwanza kuanza maandamano yasiyo na ukomo...

Huko wanatoa kichekesho cha ajabu sana. Eti walikuwa wanazuiwa hata kununua maji ya kunywa madukani au kwenye vioski, kula na kulala hotelini na kunyimwa kumbi za kufanyia mikutano yao...!

Hivi mtu mwenye akili sawasawa anaweza kuamini ujinga huu? Tangu lini maandamano yasiyo na ukomo yakafanyikia ukumbini au hotelini? Na Mwanza yote ikose wanaharakati wenye mrengo na itikadi yao wenye nyumba na hoteli za kula chakula na kuwalaza?

Inashangaza sana kuwa, Sauti ya Watanzania wana Wakili Msomi Boniface Mwambukusi. Ikawaje anakubali kuwa denied haki yake na za wenzake za msingi kama kula chakula, kunywa maji, kulala hotelini na yet asichukue hatua stahiki Kwa wanaomtendea hayo?

Majibu ya maswali hayo ni rahisi tu kuwa, huu ni mchezo uliopangwa vyema na serikali hiihii Kwa kuwatumia watu hawa kuelekea kwenye lengo kuu yaani kumwangamiza Freeman Mbowe na CHADEMA....!

Poor strategy, poor planning and poor preparations. Kwa sababu hizi naweza kuelewa ni kwanini Sauti ya Watanzania mlikuwa mnawahitaji CHADEMA. Kosa lenu ni kufanya mambo kishamba na kwa pupa...!

Baada ya kila kitu kuonekana kushindikana, vijana wa Dr Wilbroad Slaa sasa wanajirekodi na kurusha shutuma hizi kwa CHADEMA akilengwa zaidi Mwenyekiti.

Msikilize huyu 👇👇👇kisha pima kama makalamiko yake yanaleta mantiki yoyote..
View attachment 2773528
Yaani mwanzo mwisho ni kujichanganya tu...

Ni kana kwamba CHADEMA ndio waliwazuilia kumbi za mikutano yao kule Mwanza, au barabara za maandamano yao au hoteli za kula chakula na kulala na maduka au vioski vya kununua maji ya kunywa..

CHADEMA chini ya ya u - Wenyekiti wa mwamba Freeman Mbowe mna akili sana, mmekomaa. Mmeweza kuukwepa mtego huu..!??

Aisee hongereni
Umeandika uchafu mtupu
 
Mimi naamini kuwa Chadema wanawahitaji zaidi akina Mwabukuzi kuliko akina Mwabukuzi wanavyowahitaji Chadema.Kwa hiyo,Chadema hawakuwa sahihi kukataa ushirikiano na akina Mwabukuzi.
 
Magu alikuwa akitekeleza sera za CDM ambazo Slaa aliziasisi kwenye Ilani.

SGR Magu alichukua CDM, Ununuzi wa ndege Magu alichukua CDM, Kupambana na Mafisadi alifanya KAZI nk nk.

Angeanzaje kupinga?
Naunga mkono hoja
 
At the end of the day, wote ni wanasiasa wanaofanya kazi za siasa kwa manufaa yao binafsi na vizazi vyao
 
Mimi naamini kuwa Chadema wanawahitaji zaidi akina Mwabukuzi kuliko akina Mwabukuzi wanavyowahitaji Chadema.Kwa hiyo,Chadema hawakuwa sahihi kukataa ushirikiano na akina Mwabukuzi.
Kinyume chake ni kweli...

Kuwa, Sauti ya Watanzania wanavihitaji zaidi vyama vingine vya siasa kwenye harakati hizi kuliko hivyo vyama wanavyoweza kuwahitaji Sauti ya Watanzania..

Na ukweli mwingine ni huu: Kwamba, wote wanahitajiana kwa sababu wana nia na malengo yanayofanana. Wanapigania kitu kimoja..

Tatizo lililo katikati yao ni moja, TRUST. Hakuna kuaminiana miongoni mwao. Na hii ni haki na ni sahihi kabisa kwa CHADEMA na vyama vingine vyenye nia njema na nchi hii, kuwa ukiwa katika vita yoyote, basi tembea ktk tahadhari kubwa wakati wote and never trust anyone unless you're satisfied that, he/she is a true friend who can stand by your side...
 
Maajabu ndiyo haya sasa.

Yaani imekuchukua muda wote huu kutambua kwamba inawezekana tukawa tunatetea jambo lilelile?

Hukumbuki kabisa nilichokueleza katika bandiko langu la kwanza au la pili kuhusu hili jambo?

Nilisema, heshima ya Dr Slaa aliivuruga yeye mwenyewe katika matamshi yake mbalimbali aliyofanya baada ya kuondoka CHADEMA; nikakueleza pia kwamba, siyo lazima CHADEMA na kundi hilo watofautiane kwa kila jambo, ni lazima kuna mambo wanayoweza kukubaliana kati yao; kwa hiyo hili lisiwe jambo la kung'ang'ania sana kwamba kundi hilo ni mpango wa CCM kama unavyong'ang'ania wewe.
Na hapo hapo nikakutahadharisha kuhusu mbinu anazotumia Samia kumnasa Mbowe; lakini huelewi kitu!
Sasa tena unakubali hapa mwenyewe kwamba inawezekana tupo pamoja?

Binafsi, msimamo wangu juu ya CHADEMA unafahamika vizuri, kwa sababu kila mara ninaueleza humu.
CHADEMA ndiyo chama pekee cha upinzani ambacho tayari kilishaonyesha dalili za kuiangusha CCM. Hili pekee kwangu linatosha kuwaunga mkono CHADEMA bila hata kuangalia sera zao zikoje huko wakishafanikiwa kuondoa hawa CCM ambao sasa wanafanya kila mbinu ya kutotaka kutoka madarakani.
Kipaumbele kwangu ni kuwaondoa CCM, yeyote anayeweza kufanya hivyo nitamuunga mkono.
Na nilisha eleza humu, kwa nini Mbowe kwa msimamo wake baada ya kutoka mahabusu unahatarisha adhma hiyo ya kuiondoa CCM madarakani, hadi mada nikaianzisha juu yake. Halafu sasa wewe unakuja na hii habari ya mada inayoonyesha wazi mwelekeo wa kuondoa matumaini ya waTanzania, unataka tufurahie hilo?
Vyema, sasa tunaelewana..

Ndiyo ni kweli imenichukua muda kukuelewa mpaka nilipogundua kuwa tunatetea kitu kimoja lakini ktk lugha na mtazamo tofauti..

Shida imeanzia kwa wewe pia kutonielewa kuwa mimi siwapingi wala kuwabeza Sauti ya Watanzania...

Andiko langu la msingi basically linatoa tahadhari tu kwa CHADEMA kwa kikundi hiki kinachoitwa Sauti ya Watanzania...

Na nikasema, msimamo wa CHADEMA uliotolewa na Mwenyekiti taifa wao ndugu Freeman Mbowe ni sahihi kwa kuanzia..

All in all, ndani ya Sauti ya Watanzania wako watu very potential kwa CHADEMA hasahasa Wakili Boniface Mwabukusi..

Lakini ndani humohumo tena wako watu ambao ni ngumu sana kuaminika tokana na historia ya mapambano ya kisiasa. Kati ya hawa ni Dr Wilbroad P. Slaa..

Huyu na wenzake wachache ndiye anayeifanya taasisi hii ya Sauti ya Watanzania iwe treated na wapigania uhuru wa pili wa Tanganyika toka kwa wakoloni weusi - CCM kwa tahadhari kubwa...

Na hii ndiyo ilikuwa maudhui ya ujumbe wangu..
 
Bado.

Huioni hatari, na wala hutoi tahadhari yoyote juu ya kunyemelewa CHADEMA....' upande huu naona wewe ni kipofu .
Tofauti yetu kubwa ipo hapo hapo.
Labda upeo wangu wa kuona ni tofauti na wako.

Unaweza kutoa wako labda utapanua namna yangu ya kutoa maoni ifanane ya yako maana mpaka hapa naanza kutokukuelewa tena..
 
Hatuwezi kuelewana kama tatizo la msingi kwa CHADEMA tunalitazama tofauti; hii ndiyo shida kati yetu, wewe na mimi.

Nimekwishaeleza sana, hofu yangu juu ya CHADEMA inayopelekwa kwa Samia na Mwenyekiti Mbowe; wewe hili si tatizo kwa upande wako.
Sasa unataka nikubaliane tu na wewe kwamba sioni tatizo lolote?

Wewe umeona tatizo la akina Mwambukusi kuwa vibaraka wa CCM, sijui CCM ipi hiyo; lakini uaamini kwa vile baadhi yao walishaonyesha kuwa watu wasioaminika, hiyo inatosha kabisa kuwasuta na kuwakataa hata katika yale yanayoonekana wazi ni ya kuwapinga CCM hao hao.
Hii ni tofauti kati yako na mimi. Mimi nitawaamini hawa kwa haya wanayoyafanya sasa, na nitawaunga mkono.

Na kama CHADEMA nao wakionyesha dalili za kukataa mpango wa Samia na Mbowe, CHADEMA hao pia nitawaunga mkono, hata kama hawataungana na kundi hili la waTanzania, akina Mwambukusi.
Nitawapinga CHADEMA, kama wataona mbinu za Samia na Mbowe ndizo sahihi. Kundi hilo halitakuwa na tofauti yoyote na CCM, mkoloni tunayemfahamu sisi sote.
 
Back
Top Bottom