Sauti za waliofukiwa na Ghorofa Kariakoo: "Tuko hai lakini tunateseka, tusaidieni tutakufa"

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Ayo TV imeongea kwa njia ya simu na mtu aliyepo chini na wenzake tangu asubuhi Novemba 16,2024 ghorofa lilipoporomoka ambapo amesema yeye na wenzie 10 wapo hai lakini hali zao ni mbaya.

Pia, Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Majeruhi 63 kati ya 70 waruhusiwa, uokozi bado unaendelea, zoezi halijasitishwa

"Tupo chini tupo 10 toka asubuhi, tuko upande wa Don Touch, piga hata kwa Mama Samia, tuko toka jana,"

Kwa upande mwingine amesikika Mwanamke mmoja akisema wana hali mbaya.
 
Kuna wadau humu mchana walisema wanaotuma ujumbe kutoka kwenye kifusi ni attention seeker, kwamba huwezi kutuma ujumbe ukiwa ndani ya kifusi na huo ujasiri inapata wapi, sasa hadi wanazungumza kwenye simu... Nadhani wameelewa kwamba kuna watu huko chini wanateseka....

Jinsi muda unavyokwenda na probability ya kuwakuta hai hao ndugu zetu nayo inapungua...
 
Toka ghorofa limeanguka saa 3 mpka mda huu watu hawajapata msaada wa kuokolewa

Unakufa kwa kukosa msaada sio jengo kuanguka.

Nasikitka sana, leo hii vijana wanakosa ajira wakati kuna sekta kibao ikiwemo hii ya uokoaji haina wafanyakazi wa kutosha, tujitafakari.
 
Daaah mkuu sijui umewaza nini kusema hivi. Ila ni kitu cha ukweli kabisa an mule mule..

Mwanzo nilikua nashangaa sana mtu anaye ilaumu serikali ila sasa kwa haya yanayo endelea aaaah wanipige tuu ukweli taswma
 
Tanzania! Tanzania! Tanzania! Nimekuita mara Tatu!
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania Tanzania
Watu wako ni wema sana
Nchi nyingi zakuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wa kukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa.

Tanzania Tanzania
Karibu wasio na kwao
Wenye shida na taabu
Kukimbizwa na walowezi
Tanzania yawakaribisha
Tuungane kiume chema wee
Tanzania Tanzania
Mola awe na we daima.
 
Leo nimesema silali, nawaombea wawe hai. Ninalia, namshukuru Mungu kuwa wako hai kweli 🙏
Jamani kila mmoja kwa Imani yake, tuwaombee. Wako wamechoka, kiu, hewa hakuna, giza na hofu. 💔

Mimi naona watu wengi, watakuwa pale kushoto kwenye kifusi kikubwa. Kama hatuwezi uwokozi, tungeomba hata mataifa mengine, waje waokoe jahazi. Wana vifaa na watu wenye uzoefu na majanga ya aina hii. Tufanye chochote, waokolewe. Tuna la kujifunza, tuwekeze vifaa vya kisasa vya uokozi, tuache kununua magari ya anasa serikalini.
 
Nasikitka sana, leo hii vijana wanakosa ajira wakati kuna sekta kibao ikiwemo hii ya uokoaji haina wafanyakazi wa kutosha, tujitafakari.

Daaah mkuu sijui umewaza nini kusema hivi. Ila ni kitu cha ukweli kabisa an mule mule..

Mwanzo nilikua nashangaa sana mtu anaye ilaumu serikali ila sasa kwa haya yanayo endelea aaaah wanipige tuu ukweli taswma
Kuna watu walikuw wanapiga simu toka asubuhi wako underground, na bado hawajaokolewa.

Kuna watu wanapost kutoa taarifa ili waokolewe ila bado zoezi linaendelea.

Hii sio mara ya kwanza ghorofa kuanguka mjini kariakoo na hata posta. Kuna haja ya kuweka nguvu kwenye uokoaji...
 
Kuna wadau humu mchana walisema wanaotuma ujumbe kutoka kwenye kifusi ni attention seeker, kwamba huwezi kutuma ujumbe ukiwa ndani ya kifusi na huo ujasiri inapata wapi, sasa hadi wanazungumza kwenye simu... Nadhani wameelewa kwamba kuna watu huko chini wanateseka....

Jinsi muda unavyokwenda na probability ya kuwakuta hai hao ndugu zetu nayo inapungua...
Hawa watu wengine wanaweza kupata nafasi ya kuokoa maisha ya mtu wakasema huyo ni attention seeker tu.
 
Leo nimesema silali, nawaombea wawe hai. Ninalia, namshukuru Mungu kuwa wako hai kweli 🙏
Jamani kila mmoja kwa Imani yake, tuwaombee. Wako wamechoka, kiu, hewa hakuna, giza na hofu. 💔

Mimi naona watu wengi, watakuwa pale kushoto kwenye kifusi kikubwa. Kama hatuwezi uwokozi, tungeomba hata mataifa mengine, waje waokoe jahazi. Wana vifaa na watu wenye uzoefu na majanga ya aina hii. Tufanye chochote, waokolewe. Tuna la kujifunza, tuwekeze vifaa vya kisasa vya uokozi, tuache kununua magari ya anasa serikalini.
So sad aiseee hili joto tuu plass kiu daah Mungu awanusuru
 
Kuna watu walikuw wanapiga simu toka asubuhi wako underground, na bado hawajaokolewa.

Kuna watu wanapost kutoa taarifa ili waokolewe ila bado zoezi linaendelea.

Hii sio mara ya kwanza ghorofa kuanguka mjini kariakoo na hata posta. Kuna haja ya kuweka nguvu kwenye uokoaji...
Daaah mkuu hali hii inatisha mnooo..
Unajua joto la dar hapa

Sijui hiyo hali huko. Chini itakuaje
 
Ayo TV imeongea kwa njia ya simu na mtu aliyepo chini na wenzake tangu asubuhi Novemba 16,2024 ghorofa lilipoporomoka ambapo amesema yeye na wenzie 10 wapo hai lakini hali zao ni mbaya.

Pia, Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Majeruhi 63 kati ya 70 waruhusiwa, uokozi bado unaendelea, zoezi halijasitishwa

"Tupo chini tupo 10 toka asubuhi, tuko upande wa Don Touch, piga hata kwa Mama Samia, tuko toka jana,"

Kwa upande mwingine amesikika Mwanamke mmoja akisema wana hali mbaya.
View attachment 3154074
Hii serikali ya CCM ni ya hovyo sana
 
Najiuliza hii kasi ya kobe ya kuwaokoa wananchi wenzetu. Je ingekuwa ni jengo la Bunge ama lolote viongozi wamo humo, kasi ingekuwa hii hii?
Msione wengine, tunakuwaga wakali kwa Serikali humu. Unakuta umeshaona madudu wayafanyayo mengi.

Haya watu tangu asubuhi, wengine mpaka wanaaga kabisa kuwa hawaoni wakinusurika. Msisitishe kuwaokoa, hakukosekani taa kali, kazi iendelee mkitaka wa kujitolea wengine tuko tayari.
 
Ayo TV imeongea kwa njia ya simu na mtu aliyepo chini na wenzake tangu asubuhi Novemba 16,2024 ghorofa lilipoporomoka ambapo amesema yeye na wenzie 10 wapo hai lakini hali zao ni mbaya.

Pia, Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Majeruhi 63 kati ya 70 waruhusiwa, uokozi bado unaendelea, zoezi halijasitishwa

"Tupo chini tupo 10 toka asubuhi, tuko upande wa Don Touch, piga hata kwa Mama Samia, tuko toka jana,"

Kwa upande mwingine amesikika Mwanamke mmoja akisema wana hali mbaya.
View attachment 3154074
Ingekuwa ni busara kumuunganisha na muokoaji ili ampe maelekezo na sio kumpotezea charge ili uuze habari.
huyu muandishi ni kilaza mwingine anayecheza na maisha ya watu
 
Kuna watu walikuw wanapiga simu toka asubuhi wako underground, na bado hawajaokolewa.

Kuna watu wanapost kutoa taarifa ili waokolewe ila bado zoezi linaendelea.

Hii sio mara ya kwanza ghorofa kuanguka mjini kariakoo na hata posta. Kuna haja ya kuweka nguvu kwenye uokoaji...
weka majina ya watu hao vyombo vya uokoaji vifuatilie.
kuna mtu amepostiwa kafa kumbe hakufika kwenye biashara yake.Tuache kupotosha tusaidie watu kwa dhati na kweli
 
Back
Top Bottom