Sauti za waliofukiwa na Ghorofa Kariakoo: "Tuko hai lakini tunateseka, tusaidieni tutakufa"

Sauti za waliofukiwa na Ghorofa Kariakoo: "Tuko hai lakini tunateseka, tusaidieni tutakufa"

Hawa watu wengine wanaweza kupata nafasi ya kuokoa maisha ya mtu wakasema huyo ni attention seeker tu.
Kabisa, ni bora kufanya juhudi kutoa msaada kuliko kusema "huyo ni attention seeker"... Inauma sana... Ndio aina ya mtu akiwa kiongozi na matukio ya utekaji yanatokea atasema simply tu "ni maigizo" pasipo kujua watu wanaumia..
 
Idara ya zima moto na uokoaji, haina vifaa vya kufanya uokoaji. Crane kubwa na zenye nguvu zinahitajia eneo la tukio kuinua nguzo nzito zilizolaliana, Bulldozers za kutosha zifike eneo la tukio ziweze kuzoa kifusi, pia tunahitaji malori makubwa ya kubeba mchanga ili kuondoa vifusi eneo la tukio ili kurahisisha zoezi la uokoaji.

Tunahitaji kituo cha kuchukuli na kutolea taarifa, na tunahitaji kituo cha huduma ya kwanza chenye wahudumu wa kada zote za afya wanaohitajika kwenye majanga, na ambulace za kusafirisha wagonjwa kupelewa hospitali kwa waokolewaji.

Mwisho Jeshi la polisi lifukuze watu eneo la tukio au lipange utaratibu wa namna ya kufanya uokoaji kwa kushirikiana na wataalamu wa majanga, majengo ili kuzuia hatari kwa waokoaji na waokolewaji.

Mlundikano wa watu eneo la tukio bila utaratibu mzuri ni tatizo kwenye eneo la uokoaji, iwe majini au nchi kavu. Kuna paswa kuwe na utaratibu mzuri ili kufanikisha zoezi husika.

Watanzania waeleweshwe, hili ni tatizo siyo movie kila mtu anapaswa kushuhudia.

Wananchi wakae mbali, wachaguliwe watu wenye afya na uwezo wa kusaidia tu, wanawake na watoto wakae mbali.
 
acha unafiki yaani mwanahabari yupo tayari kufanya mahojiano na kurusha mtandaoni badala ya kurelay mawasiliano na waokoaji,??
Halafu unamtaja Mungu!!
unafiki kiwango cha SGR
Nakwambia hujuu unachozungumza, hata hiyo clip hujaisikiliza

Kama ungesikiliza ungejua kuwa wameshafikisha taarifa kwa mkuu wa mkoa

Pili ungesikiliza ungejua mwandishi kafikisha taarifa kwa mkuu wa mkoa

Tatu ungekuwa una uelewa hata kidogo, usingeropoka. Haya ni maisha ya watu ambao wamekwama kwenye kifusi toka asibuhi na matumaini yao yanapungua kadri mda unavyosogea. Hawajala, hakuna hewa ya kutosha, kwa sababu hawajakwama baba yako au mama yako, huoni kama wana haki ya kuokolewa.

Hao ni walipa kodi, wanalipa kodi ni haki yao kuuliza kwa nini inachukua nda kutolewa.

You are a bad energy, I dont get it why am arguing with you, sad
 
Uokoaji umesitishwa wakati watu wapo hai chini ya kifusi?

Viongozi wana amani kabisa wanaenda kulala wakati kuna raia wapo hai kwelii jamani kweliii?

Mbona barabara zinajengwa usiku, Mbona ma ujenzi na maandalizi ya masherehe yao wanaandaliwa hadi usiku?

Kweli uoakoaji umesimama wakati watu wapo hai cchini ya kifusi?

Hii sio SAWA hii ni mbaya najiskia kuumia sana najiskia uchungu nioweza uelezea.

huu ni uonevu, hakika hiii sio sawa
 
Nakwambia hujuu unachozungumza, hata hiyo clip hujaisikiliza

Kama ungesikiliza ungejua kuwa wameshafikisha taarifa kwa mkuu wa mkoa

Pili ungesikiliza ungejua mwandishi kafikisha taarifa kwa mkuu wa mkoa

Tatu ungekuwa una uelewa hata kidogo, usingeropoka. Haya ni maisha ya watu ambao wamekwama kwenye kifusi toka asibuhi na matumaini yao yanapungua kadri mda unavyosogea. Hawajala, hakuna hewa ya kutosha, kwa sababu hawajakwama baba yako au mama yako, huoni kama wana haki ya kuokolewa.

Hao ni walipa kodi, wanalipa kodi ni haki yao kuuliza kwa nini inachukua nda kutolewa.

You are a bad energy, I dont get it why am arguing with you, sad
Mahojoano na muhanga aliye chini kwenye kifusi yana faida gani kwa sasa kama sio kihatarisha juhudi za uokoaji na maisha ya wahanga ...huu ni uandishi wa wapi?
Tuache unafiki na uhuni inapokuja suala la dharura
 
Back
Top Bottom