Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unakua Unaomba utoke hai..Hali ikiendelea kua mbaya Kuna kuishiwa nguvu na kukata tamaa.Hiyo moment isikie kwa mwenzako
🥺🥺
Ungekua upo kwenye kifusi muda huu usinge fanya rubbish comment hapa.Ayo TV imepata Itambulisho wa Wahanga hao au ni bla bla tuu
@ that point ☝️ namwombea atoke salama.
Ayo TV imeongea kwa njia ya simu na mtu aliyepo chini na wenzake tangu asubuhi Novemba 16,2024 ghorofa lilipoporomoka ambapo amesema yeye na wenzie 10 wapo hai lakini hali zao ni mbaya.
Pia, Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Majeruhi 63 kati ya 70 waruhusiwa, uokozi bado unaendelea, zoezi halijasitishwa
"Tupo chini tupo 10 toka asubuhi, tuko upande wa Don Touch, piga hata kwa Mama Samia, tuko toka jana,"
Kwa upande mwingine amesikika Mwanamke mmoja akisema wana hali mbaya.
View attachment 3154074
Taarifa alizotoa mhanga zinatosha kabisa kumfanya msikilizaji yeyote anaejua hilo eneo akapafahamu wahanga walipo.Huo muda wa kumtafuta muokoaji ndio asikilize maelezo una uhakika simu ingeendelea kuwa hewani?Ingekata chaji?Tuache kukosoa kila kitu. Mwandishi ametekeleza wajibu wake ipasavyo. Hawa watu kumi wakiokolewa hizi ni moja kwa moja juhudi binafsi na ubunifu wa mwandishi. Sisi kazi yetu kukosoa tu tukiwa nyuma ya keyboard.Daaaaaa nimeskiliza iyo video adi jasho linanitoka..
Kwanza uyo mtangazaji ni mpumbavu eti anauliza mnahaligani huko?
Watu wapo njia panda ya uhai na kifo yeye anauliza swali la kichoko.
Huo muda anaompotezea chaj kupga nae story ni ilibidi atafute kiongozi wa jeshi la uokoaji na mwenyeji wa mitaa iyo( anaejua maduka) Kisha uyo muhanga awape maelezo wapo chini sehem gani maana naona alitaja upande waliopo adi jina la duka..
Na wangepata content km kawaida ya muokozi akiongea na muhanga sio mtangazaji aongee na muhanga..
Hao watu kadri muda unavyozidi kwenda miili inaishiwa nguvu wapo wengi na wanapambania hewa(oxygen) kidogo sana inayopenya huko, mwsho ataanza kuzima mmoja mmoja😭😭😭😭.
Hadi nawaza au sjui waandishi wanapenda kutangaza vifo kuliko manusura??
Ilipaswa na yy awe kwenye magwanda ya uokozi kuhamasisha. Hakuna point ya kuhutubia tena uhai na uchovu wa mwili ausubiri kwa watu walionaswa.Mimi usingizi umeshindikana kbs Kwa Leo!Kuna yule dada Instagram anaitwa bintimohammed28 ameniliza Kwa jinsi walivyo banwa!Hivi ule muda waziri mkuu anapoteza kuhutubia si ungefaa kuendelea na kazi?Yaan mtu anakuja kwenye majanga badala apige kazi ndio kwanza anakuja na msafara wa maV8 na kupoteza muda tu!Tunaongozwa na watu wa ajabu sana
Ndugu yangu haielezeki na hata kuifikiria sitaki. Mungu atujalie mwisho mwema!Hiyo moment isikie kwa mwenzako
🥺🥺
Dah,ya Allah watilie wepesi waja wako wapate kuokolewa salama watoke kwenye ilo janga lililowafika huko chini ya vifusi, kwa hakika baada ya uzito upo wepesi inshall'ahAyo TV imeongea kwa njia ya simu na mtu aliyepo chini na wenzake tangu asubuhi Novemba 16,2024 ghorofa lilipoporomoka ambapo amesema yeye na wenzie 10 wapo hai lakini hali zao ni mbaya.
Pia, Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Majeruhi 63 kati ya 70 waruhusiwa, uokozi bado unaendelea, zoezi halijasitishwa
"Tupo chini tupo 10 toka asubuhi, tuko upande wa Don Touch, piga hata kwa Mama Samia, tuko toka jana,"
Kwa upande mwingine amesikika Mwanamke mmoja akisema wana hali mbaya.
View attachment 3154074
CCM hawana hiyo akili. Akili zao ni kununua mashangingi na magoli ya Simba na Yanga.Leo nimesema silali, nawaombea wawe hai. Ninalia, namshukuru Mungu kuwa wako hai kweli 🙏
Jamani kila mmoja kwa Imani yake, tuwaombee. Wako wamechoka, kiu, hewa hakuna, giza na hofu. 💔
Mimi naona watu wengi, watakuwa pale kushoto kwenye kifusi kikubwa. Kama hatuwezi uwokozi, tungeomba hata mataifa mengine, waje waokoe jahazi. Wana vifaa na watu wenye uzoefu na majanga ya aina hii. Tufanye chochote, waokolewe. Tuna la kujifunza, tuwekeze vifaa vya kisasa vya uokozi, tuache kununua magari ya anasa serikalini.
Wananchi wameokoa watu wengi kuliko hao unaowaita Wataalamu.Idara ya zima moto na uokoaji, haina vifaa vya kufanya uokoaji. Crane kubwa na zenye nguvu zinahitajia eneo la tukio kuinua nguzo nzito zilizolaliana, Bulldozers za kutosha zifike eneo la tukio ziweze kuzoa kifusi, pia tunahitaji malori makubwa ya kubeba mchanga ili kuondoa vifusi eneo la tukio ili kurahisisha zoezi la uokoaji.
Tunahitaji kituo cha kuchukuli na kutolea taarifa, na tunahitaji kituo cha huduma ya kwanza chenye wahudumu wa kada zote za afya wanaohitajika kwenye majanga, na ambulace za kusafirisha wagonjwa kupelewa hospitali kwa waokolewaji.
Mwisho Jeshi la polisi lifukuze watu eneo la tukio au lipange utaratibu wa namna ya kufanya uokoaji kwa kushirikiana na wataalamu wa majanga, majengo ili kuzuia hatari kwa waokoaji na waokolewaji.
Mlundikano wa watu eneo la tukio bila utaratibu mzuri ni tatizo kwenye eneo la uokoaji, iwe majini au nchi kavu. Kuna paswa kuwe na utaratibu mzuri ili kufanikisha zoezi husika.
Watanzania waeleweshwe, hili ni tatizo siyo movie kila mtu anapaswa kushuhudia.
Wananchi wakae mbali, wachaguliwe watu wenye afya na uwezo wa kusaidia tu, wanawake na watoto wakae mbali.