Sauti za waliofukiwa na Ghorofa Kariakoo: "Tuko hai lakini tunateseka, tusaidieni tutakufa"

Mbona mnatufokea hvo..
Tunataka kujua hali ipo vipi
Kuna maswali mengine ya kipuuzi sana . Ameuliza mko wa ngapi ni sawa mpo upande gani hajauliza halafu hayo maswali alitakiwa awe anauliza mbele ya waokoaji hakuna muda wa kupoteza yeye anauza sura kwenye kamera
 
Mungu aendelee kuwapa ujasiri wa kuvumilia,niliwahi kukwama kwenye lift dakika kama 5 nilihisi kuishiwa nguvu na kutaka kupoteza fahamu,japo kulikuwa na hewa,sasa kukaa zaidi ya masaa 10,nawaza sipati majibu,ni neema ya Mungu tu inahitajika...
Ameeen Mungu yupo pamoja nao mkuu..
Japo nikiwazaga ishu ya joto na kiu daaah napata wasi wasi..

Mkuu ndo wewe ulitoka kwenye lift ukiwa kifua wazi, ukavalia shart stend ya daladala sio
 
Mimi sisemi kila kitu ni perfect lakini kumbuka vijana waliotokea na kufanya kazi haraka ni vijana wametoka hapo hapo wengine ni jengo la pili tu na tumesikia kuna watu nusu saa tu wakaanza kutolewa ila Kariakoo ilajaa watu lakini watazamaji wengi na kuna walijotolea. Vyombo vya kuokoa vinakuwa viko sehemu na mkuu wa uokozi ndio anatoa mwongozo akijuwa nini kimetokea na nini kinatakiwa hii ni kawaida kabisa. Kuna ajali zinatokea barabarani watu ndio wanakuwa wa kwanza katika zoezi kabla ya vyombo vya usalama.

Point ya kujifunza ipo na kila siku lazima ujifunze ila miundombinu ya kariakoo kwa maana ufinyu wa barabara ni shida kubwa sana hata ukifiwa na mtu hapo ni shida kufika. Kikubwa hapa zoezi liwe na mafanikio kusiwe na mtu kapoteza maisha sababu tu alichelewa kutolewa au kupata msaada. Ila naamini zoezi limeenda vizuri.
 
Lucha acha kufokea wenzako....
Pale anauliza ili apate hali halisi ya kule chini mkuu
Unauliza watu hali zao wakati wamefukiwa na kifusi hizo ni akili au matope? Hiyo haina tofauti na dhihaka wewe unaona ni swali la kawaida kwasababu hauko ndani ya kifusi, ila ni swali la kijinga ni sawa mtu yupo kwenye meli alafu wewe upo kwenye boti inayozama alafu anakuuliza hali yako ikoje hapo
 
Nimekuelewa sana lucha...
Nimeelewa mno daaah..

Kuna ujumbe hapo juu umetumwa kwa picha aiseeee kweli life hii ndgu yangu
 
Emergency yoyote inayojitokeza Tanzania jua mmekwisha .
Vichwa vinavyowaza Teuzi, V8 na kuiba haviwezi zingatia Wala kunusa hatari even kuiona hata ikiwa imetokea.
Matatizo yapo kuzibua mashimo wanayoyafunika.
 
Ni swali la kipumbavu
 
Wananchi wameokoa watu wengi kuliko hao unaowaita Wataalamu.
Hiko hivyo dunia nzima, kwasababu wataaluma hawapo kila sehemu, ila kwasababu ajali inapotokea hupewa taarifa, na wanlipwa pesa za umma ni wajibu wao ku establish plan nzuri ili kuokoa na kupunguza vifo. Sikusema wananchi wasiokoe, nilitaka tuone value of our money, tunawalipa ili wajenge mbweni au watufanyie kazi?
 
Kijana Seba aliyeandika message kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho siku mbili zilizopita.




Mwili wake umeopolewa mda huu ukiwa tayari umeshaanza kuaribika kwenye jengo la Kariakoo.. Tayari mwili wake umepelekwa kwenye hospitali ya Amana kwa kwa taratibu nyingine za kuhustili..Roho ya marehemu ipumzike mahara pema peponi 😭😭 Inasikitisha sana jamani Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un💔🙏
 
Mara hii ishasahaulika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…