Sawa tunaokukosoa unatuita 'Mbwa Mwitu'. Je, sisi ndiyo tulikufanya uuache Ukuu wako wa Mkoa ili 'ukagaragazwe' Kigamboni?

Mbaya zaidi nchi inaenda kuwa chini ya Lissu
 
Makonda akili zake kama kondoo tu yaani anajionaga mkuubwa kumbe tembo wa mabua, niliwahi kusema nje ya U RC makonda ni mwepesi kuliko sufi
 
Nadhani kauli yake ilikua inawalenga baadhi ya watendaji wa mkoa na si wakazi wa mkoa
 
WEKENI AKIBA YA MANENO NDUGU ZANGU. JPM HAWEZI KAMWE KUMTUPA MAKONDA. MTASHUHUDIA HAYA MANENO YANGU 2021. NGAYO!
Thubutu, kama hawakuondoka wote. Heri asome alama za nyakati kwani dalili ya mvua ni mawingu. Ukiona mwenzio ananyolewa, nawe anza kutia maji. Hata vyombo vya usalama vitaweza kupumua na kuanza kutimiza wajibu kwa kufuata sheria. Huu ni mwaka mbaya sana kwa washamba wote na limbukeni kwani wote watapewa one way ticket!
 
Hakuna marefu yasiyo na ncha, amejikaanga mwenyewe kwa mafuta yake.
Atakuwa anaota sana burudani alizokuwa anapata.
Hahaha, inawezekana siyo mafuta yake, maana yangemuhurumia
Aliangiza kotanak kutoka ururuki.
Yakamuunguza kabisa badala ya kumkaanga
 
Nadhani anahisi hao watendaji walichangia anguko lake hapo Kigamboni.
yes true, lakini hakufanya POA jambo zuri ukitoka kwenye position utoke bila kinyongo Yani Kama alikua anampa ujumbe mkuu mpya kua usione wanakuchekea Hawa sio watu wazuri...unaacha position kwa kutengeneza uadui.
 
Akili yake ipo kwenye kupima tezi dume.
Nahisi atakuwa anapima tezi dume kila siku huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…