#COVID19 Sayansi inazidi kutokomeza Corona

We unaonekana hujui kuhusu virusi kabisa. Hivi Mungu anaweza kuwa na majibu yanayoexpire kweli yani kipindi kile atusaidie leo atuache duu. Ukifuata sayansi utajua kwann sahiv tumepigwa kuliko mara ya kwanza achana na imani Mfu.
science ina require experiment and proof. sio uswahili.
utavijuaje virusi bila science?
Kama science ingekuwa fake..Mungu angeamua kuifutilia mbali isingekuwepo.
Ameruhusu iwepo ili tutumie kusolve mambo mbali mbali.

yes kuna imani.. imani bila matendo ni mfu.
hata siku moja Mungu hakupi jibu la direct bila kuonyesha jitihada.

huwezi omba Mungu akupe majibu ya mtihani wakati hukusoma.
 
tafiti tumeziweka kando. nchi haija invest kwenye science. ndio maana wasomi wetu wakitoka kusoma huko nje wanakimbilia ubunge.
 
Waisrael wamekufa 5526.
tangu mwaka Jana .
He Tanzania wanafika waliokufa na Corona hyo idadi?.
KWA MUNGU TUNATEGEMEA.na tutashinda.
Mganga MUNGU tu
tanzania mara ya mwisho kuchukua idadi ilikuwa lini?
sisi hatuhesab wao wanahesabu. huwez kujilinganisha nao
 
Sina haja hata kukujibu ila hii weka kumbukumbu siku mzee akiwa anapokea chanjo live kwenye TBC utakumbuka haya yote. Hujiulizi sababu ya kupiga marufuku kutangaza number? hakuna kupima, number ya wagonjwa imesimama watu 500 mwaka mzima unadhani watu wajinga halafu unasema tuliaga siku nyingi.

Watu wangapi tulizika. Wewe hupimi watu, hutaki data zitolewe halafu unasema hakuna corona, mbona data za shule ngapi mmjenga, zahanati ngapi, barabara ngapi zinatolewa.

Swali lako lingekuwa na mantiki kama data zingekuwa wazi kwa kusema corona ilikuwa hivi kabla tulivtofunga shule ikawa hivi labda ilisaidia au hapana ndio tungeamua hatua nzuri ya kuchukuwa.

Sasa hakuna data zozote utafanya vipi maamuzi? mambo ya kunawa mikono ni tabia zetu ila kama wewe unanawa sababu ya corona tu hiyo ni issue yako.
 
Mkuu punguza jazaba,hakuna niliposema kuwa Tz hakuna corona si mwaka huu wala mwaka jana. Kumbe unajua kuwa tulikuwa hatuna takwimu za corona kwa sababu tuliacha kupima,sasa nakushangaa kusema kwamba sijui kufunga mashule kuvaa mask na kunawa mikono ilisaidia hiyo mwaka jana wakati unajua hakukuwa na data za kuonesha hali ya corona ikoje nchini ili ndio tuweze kusema huko kufunga mashule kuvaa mask na kunawa mikono ilisaidia.

Mimi nilikuwa namuunga mkono mtu humu aliyesema corona huondoka yenyewe ila wewe ukaja na mambo ya hatua za kunawa mikono na kufunga mashule kwamba et zilisaidia pia, ndio maana nilikuuliza hizo hatua(kufunga shule,kuvaa mask n.k) zilidumu kwa muda gani hadi tuseme zilisaidia? na tena hatukuwa na data za corona.
 
Maambukizi ya awamu ya kwanza yaliondojaje vile,??
Kulikuwa na jitihada nyingi kuliko sasa. Kuna maeneo hukuruhusiwa kuingia bila barakoa. Kuna maeneo hukuruhusiwa kuingia bila kunawa mikono. Nilishuhudia baadhi wanaenda kwenye ATM wakiwa wamevaa gloves. Sanitizer mpaka ziliadimika. Makanisa mengi waliamua kufanyia ibada nje ya majengo.

Juhudi hizi kwa pamoja zilisaidia sana kupunguza masmbukizi.
 
Siyo 100m ni zaidi ya bilioni 100. Tulipewa pesa tupeleke kupambana na corona, kuna taarifa za uhakika tulipeleka kwenye uchaguzi, tukawadanganya watu kuwa uchaguzi wa 2020 tumetumia hela zetu!
 
Waisrael wamekufa 5526.
tangu mwaka Jana .
He Tanzania wanafika waliokufa na Corona hyo idadi?.
KWA MUNGU TUNATEGEMEA.na tutashinda.
Mganga MUNGU tu
Hatujui idadi lakini kwa hakika ni zaidi ya hao 5,526.
 
Ushauri wa Dr. Mwigulu Nchemba wa kuficha takwimu za maambukizi na hatimaye kuacha zoezi la upimaji ndio limetufikisha hapa!
Sasa hakuna anayejua ukubwa wa tatizo tulilo nalo na hata "Mabeberu" wakisema tuko kwenye Red List hatuna namna ya kupinga!
Halafu tunajidanganya elimu za bongo ni perfect!
Mtu wa level za PHD hajui umuhimu wa takwimu katika kukabili tatizo!
ACHA TUENDELEE NA MAZOEZI YA VIFUA!
 
Hii ni moja ya article nzuri amabazo zimeletwa hapa jukwaani kuhusu corona,Ahsante sana kwa maelezo yako.kwa mda sasa nilikuwa na mawazo kama haya kuwa hatujui tumeathirika vipi sababu hatuna data yeyote.kwa kuongezea tu nchi nyingi za ulaya na America zimeathiriwa sana na huu ugonjwa,lakini hawakati tamaa walifanya tafit,walifuatilia kwa kukusanya data, wakaelimisha jamii zao na walipokosea walirudi tena maabara na kujifunza tena.Wazungu wanaonyesha wanavyojari uhai na kutokubari kushindwa,na sasa wanaona mafanikio.Kuokoa maisha hata ya watu 5 si sawa na kuacha watu wajifie tu bila kufanya lolote,inabidi kuwe na njia ya kujua tz imeathirika vp na waanze ku manage haraka,otherwise mambo yatazidi kuwa mabaya ma itabidi hao mnaowaita mabeberu waje na waanze kukuzoleeni mavi mlo kunya nyie.
 
Propaganda tu kama zilivyo propaganda nyinginezo.
 
Hakukuwa na data lakini tuliona katika mitaa yetu au miji yetu vifo au wagonjwa mahospital kupungua haya mambo kwa ushuhuda. nakumbuka wakati naenda Hosp fulani wakati shida ndio imekuwa kubwa kulikuwa na ward imetengwa kwa corona sasa tatizo wakati ule hakukuwa na kipimo mgonjwa akija anahisiwa anawekwa kule ilikuwa watu wanakimbiana Hosp ila baada ya hatua kali kuchukuliwa kama kufungwa mashule, michezo, harusi na hatua zingine kama baada ya mwezi Hosp ileile nikwenda tena nilikuta hali fulani ya utulivu na hata vifo mitaani vilipungua sana sasa hiyo kwangu ni mambo yalikuwa yako wazi tunaona, sisemi 100% labda ndio sababu ila kwa mujibu wa wataalamu walikuwa wakitushauri hivyo na kila sababu ya kuamini kuna ukweli.

Tatizo hapa kujiuliza je ungonjwa ulipungua kwa sababu ya kuomba siku 3 kama tunavyoambiwa au zile hatua zilisaidia? kuomba ni imani maana unaomba lakini hujui kama umekubaliwa ni dhana ila vitendo ni bayana unaona.
 
Tayari nineiweka kwenye bandiko.
 
Nimesoma article moja, wao walicho fanya cha kwanza ni kufunga mipaka yao.
Na sio kupima raia wao .

Jingine ni hili hapa badala ya testing testing testing
i24NEWSIn this screenshot photo taken on Monday, February 24, 2020, Israeli Defense Minister Naftali Bennett speaks to i24NEWS


'We need to take care of grandma and grandpa, but from far away'
The key to defeating the global pandemic of coronavirus is isolating the elderly population in the hope that young people who are not in the risk group for complications would develop herd immunity, Israel's caretaker Defense Minister said Friday in a recorded statement.

Play Video

"The most important thing... is to separate old people from younger people. The single most lethal combination is when a grandma hugs her grandson," the right-wing politician said.
"What we need to over the following period of time is take care of grandma and grandpa, but from far away. Lots of Whatsapps and Skypes and you name it."
 
Walalahoi wanakufa wengi lakini hawasikiki kwa Taifa zima kwa sababu siyo watu maarufu.

Siku ukiugua au ndugu yako akiugua utalitafuta hili andiko. Management protocol nimeoweka kwenye bandiko baada ya kuombwa na wengi hapa jukwani na kwenye inbox. Chukua hiyo protocol, kuna siku itakuokoa wewe au ndugu au rafiki yako. Usishupaze shingo.

Mambo ya kusema eti ni vita vya kiuchumi, ni maneno yasiyo na backing yoyote. Ni upotoshaji.
 
Inabidi kuifahamu hii The Jewish Covid 19 Management Protocol. Siku zote Tujifunze kwa waliofanikiwa.
Nimeipandisha kwenye bandiko. Ichukue kuna siku itaokoa maisha ya mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…